WABALLA Inc
JF-Expert Member
- Sep 2, 2014
- 2,711
- 1,015
Habari wana jamvi?
Kwa wale wenye uelewa na kanuni za Idara za Maji, ninatumia maji ya bomba kutoka Mamlaka ya Maji ya Mji mmoja. Ninavyojua kisheira hairuhusiwi kuuza maji bila idhini ya mamlaka husika. Nina jirani yangu amabye aliomba kutumia/ kuwa anachota maji. Kama mnavyojua jirani yako ndio ndugu yako sikumkatalia akawa anachota. Kwa sasa sipo eneo hilo ila wamekuja mafundi wa idara na kunikatia maji kwa kigezo kuwa ninauza maji. Nimejaribu kuongea nao kwa njia ya simu ila wamenikomalia kuwa lazima wakate kwa kusisitiza kuwa nauza maji. Mbaya zaidi wanasema kuna jirani yangu kapiga simu (yeye ana kiali cha kuuza maji) na analalamika kuwa namuharibia biashara hivyo itaonekana wamenipendelea wasipokata maji.
Swali langu ni , je hairuhusiwi kumpa jirani yako maji kisheira?