SI KWELI Picha inayodai kuonesha timu ya taifa ya Korea Kusini ikitangaza kususia vyombo vya habari

SI KWELI Picha inayodai kuonesha timu ya taifa ya Korea Kusini ikitangaza kususia vyombo vya habari

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu, Je picha halisi ni ipi hapa kati ya hizi mbili?
1783250761961.png
1783250775669.png
 
Tunachokijua
Madai

Mitandaoni imesambazwa picha ikidai kuonyesha wachezaji wa timu ya taifa ya Korea Kusini wakitangaza kusitisha mawasiliano na vyombo vya habari kufuatia madai kwamba baadhi ya waandishi walimkejeli nahodha wa timu hiyo, Son Heung-min.

Uhalisia

Uchunguzi umebaini kuwa picha hiyo si ya kweli. Ingawa ni kweli wachezaji wa Korea Kusini walisitisha kwa muda mahojiano na vyombo vya habari vya ndani baada ya mchezo wao wa Kombe la Dunia dhidi ya Czech Republic tarehe 11 Juni 2026, hakuna tangazo rasmi, picha wala video inayoonesha timu hiyo ikitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari.

Aidha, picha inayosambazwa ina viashiria kadhaa vinavyoonyesha kuwa imetengenezwa kwa kutumia Akili Unde (AI).

Katika picha hiyo kuna makosa kadhaa ya kimuonekano yanayodhihirisha kuwa si halisi, ikiwemo:

Mchezaji Hwang Hee-chan anaonekana mara mbili ndani ya picha moja akiwa na rangi tofauti za nywele. Nahodha Son Heung-min ameongezewa mchoro (tattoo) kwenye mkono wa kulia, ilhali picha rasmi za Kombe la Dunia zinaonyesha hana tattoo hiyo.

Nembo ya Korea Football Association (KFA) inayoonekana nyuma ya wachezaji ni toleo la zamani ambalo halitumiki tena.

Zaidi ya hayo, picha hiyo inafanana kwa kiwango kikubwa na video ya mwaka 2016 iliyoonyesha timu ya taifa ya Argentina ikitangaza kususia vyombo vya habari vya nchi hiyo, jambo linaloashiria kuwa imetengenezwa kwa kuiga tukio hilo.

Hivyo madai kwamba picha inaonyesha timu ya taifa ya Korea Kusini ikitangaza kususia vyombo vya habari Inapotosha. Picha hiyo imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Mnemba (AI), na hakuna ushahidi rasmi unaothibitisha kuwahi kutolewa kwa tangazo hilo mbele ya waandishi wa habari.​
Back
Top Bottom