NgomaNgumu
Senior Member
- Nov 20, 2010
- 194
- 24
cha msingi ni je ulipewa kibali cha kujenga eneo hilo? Kuwa na hati halali hakumaanishi kuwa eneo hilo unaruhusiwa kujenga chochote unachotaka. Kama ulipewa kibali cha kujenga na hati ya kuruhusu kuhamia kwenye jengo basi una haki ya kushtaki mamlaka iliyokupa vibali hivi.
Amandla......
Kwann upewe hati wakati unaona ni eneo la wazi au hifadhi ya barabara?acheni ujinga nyie ndo mnatapeliwaga kwa kuuziwa misikiti na makanisa
Mategemeo yangu makubwa yalikua ni kwamba utatoa mawazo ya maana ktk kutatua hili tatizo, badala yake umeamuamua matusi. Naomba ujibu hoja zilizo tolewa kwani sio kua maeneo yote ya wazi kila mtu anajua yeye mwenyewe tu kua hili eneo ni la wazi na ndio maana tuna wizara ya ardhi. Haina haja ya ya raia kua mjinga au mjanja ili apate haki yake.
Tunampongeza Mh Tibaijuka kwa kazi anayoifanya ya kujribu kufuata taratibu zinazohusiana na plan ya jiji kama lilivyotakiwa liwe na wizara ya ardhi. Ambalo linatia wasiwasi kidogo ktk shughuli yake ni pamoja na kukumbushana kua kunatofauti kubwa kati ya mazingira ambayo waziri huyo alichukua experience yake ya kazi na yale yaliyopo Tanzania. Hilo linaweza kumfanya awe muangalifu zaidi wakati anaposhughulikia baadhi ya kesi. Kwa mfano mwananchi anapokua na hati halali ya kumiliki ardhi ktk eneo fulani, baadae akafahamishwa kua eneo hilo halikupaswa kujengwa.
Kwa haraka kinachofahamika ni kua uwezekano wa makosa unaweza kua umetendeka ktk pande mbili, upande wa mnunuzi au wizara ya ardhi. Sasa uamuzi unaochukuliwa hivi sasa wa kumvunjia mwananchi nyumba unaonekana kama umeadhibu pande moja tu kua ndio yenye makosa ambayo ni upande wa mwananchi. Swali linalojitokeza ni kua kama mfanyakazi wa ardhi nae alihusika na tatizo hilo ima kwa kula rushwa au kitu kingine chochote, hakuna adhabu yoyote anayoipata na hivyo kumuhamasisha kuendelea kufanya hivyo tena na tena.
Ukirudi ktk hali ya nchi, waTanzania waliowengi kama amebahatika anaweza kupata nafasi ya kujenga nyumba mara moja tu ktk umri, sasa utakapomvunjia nyumba ktk sehemu ambayo alielezwa kua ni halali yeye kujenga, baadae ikabainika vinginevyo, je atakua kweli huyu mwananchi ametendewa haki? Na kweli itakua hii ni kumsaidia mwananchi au kumkandamiza? Tunanomba mchango wenu ktk hili.
Ivi Mkuu umetumwa kumtetea mtu humu???
Mkondo wa sheria mkiupindisha kwa faida yenu mwasema hawa ni kuwapa kidogo tu na watanimalizia kazi yangu sasa pale sheria inapo jirudi na kujiangalia kama ilichokitoa ni sawa na ulijua fika ilikuwa sio sawa sasa waaanza lalama kwa vyombo vya habari ati ni hati halali kivipi?
Na tatizo lingine pale sheria inapo fuata mkondo wake bado mwalalama mwataka iweje sasa si mliisema hiyo wizara imeoza na ianarekebishwa sasa mwaanza kulia kumbe ndio nyie mlioshiriki kuichafua hiyo wizara si ndio maana machungu yanatokea wapi kama hukua muhusika mkuu wa kuifanya hiyo wizara kunuka rushwaaa.
Ardhi ni mali ya serikali kwa hiyo hata ukiwa na hati 100, serikali ikiamua inakunyanganya na inabomoa sio lazima kiwe cha magumashi, la msingi ni watu wa ardhi kuwa wastarabu na waadilifu na pia na sisi tusitoe rushwa ili tupendelewe ndio mwanzo wa haya yote.
Kama ulinunua iyo ardhi kihalali utalipwa fidia kwa mujibu wa sheria, lakini leo hii ununue kiwanja kwenye eneo la wazi/hakijapimwa/hifadhi ya barabara kwa rushwa kikichukuliwa usitegemee fidia. Kuna mchezo niliuona miaka ya nyuma watu wananunua viwanja karibia na barabarani alafu wanakimbilia kujenga haraka haraka wanategea pindi nyumba zitakapowekewa alama ya x walipwe fidia ya mamilioni.Tunakubali wote kua ardhi ni mali ya serikali lakin kama waliuza ardhi kihalali baadae wakiihitaji hiyo ardhi kwa maslahi ya taifa ni lazima watoe fidia ili huyo mwananchi ajenge sehemu nyingine au apatiwe sehemu ya kuishi. Vingenevyo kusingekua na maana kutaja kua kuna maeneo ya wazi na yasiokua wazi. Ambacho watu wanajribu kukijadili ni uwezekano wa kutendeka haki kwa pande zote.