SHIEKA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,244
- 4,258
Kwenye redio na tv nimesikia watu wakitumia sana hili neno 'either' kwenye mazungumzo, akimaanisha 'ama.....au....' Mtu atasema hivi: "Umaskini wetu unaletwa na either uvivu wetu au kutowajibika kwetu" Matumizi ya hilo neno si sahihi hata kidogo, badala yake angeweka neno la Kiswahili 'ama'. Matumizi ya neno either yameshamiri sana na kwangu mimi naona kama kero ya lugha. Je yawezekana ni uelewa mbaya wa neno 'aidha' ambalo hata hivyo lina maana tofauti? Wana JF, hebu tupieni uzoefu wenu tafadhali.