Je, Neno 'either' ni la Kiswahili?

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Kwenye redio na tv nimesikia watu wakitumia sana hili neno 'either' kwenye mazungumzo, akimaanisha 'ama.....au....' Mtu atasema hivi: "Umaskini wetu unaletwa na either uvivu wetu au kutowajibika kwetu" Matumizi ya hilo neno si sahihi hata kidogo, badala yake angeweka neno la Kiswahili 'ama'. Matumizi ya neno either yameshamiri sana na kwangu mimi naona kama kero ya lugha. Je yawezekana ni uelewa mbaya wa neno 'aidha' ambalo hata hivyo lina maana tofauti? Wana JF, hebu tupieni uzoefu wenu tafadhali.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Sio either ni aidha sikiliza vizuri tafadhali

Aidha haina maana sawa na either.

Either ina maana sawa na "ama", wakati aidha ina maana sawa na "na" au "zaidi ya hivyo".

Naweza kusema "Aliporudi nyumbani hakumkuta mama yake, aidha, hata baba yake hakuwapo"
 
Back
Top Bottom