Je, ndoto za Godbless Lema ni utabiri au sayansi ya uchawi katika siasa?

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Kuna mambo siyo ya kuyaletea mzaha hata kidogo, Wengi yamewakuta na wengine wametwaliwa moja kwa moja kutokana na kile kinachoitwa ndoto anazooteshwa Godbless Lema iwe kwa kutamka hadharani au kutoa meseji kupitia akaunti yake ya twitter

Mwanzoni nilifikiri Godbless Lema anaangalia afya za wahusika yaani physical appearance na kuwatabiria Kifo na majanga, Hii ya kumuangalia mtu jinsi alivyo, anayoongea hata mimi nikiwa na umri wa utoto kabla ya kuanza kujihusisha na dhambi nilikuwa na uwezo wa kujua huyu ana shida na hata Chukua raundi ataondoka moja kwa moja yaani Kwaheri ya kuonana na Nilitamka kwa ndugu na hata wazazi waliona kama ninatisha tisha hivi lakini niliwaambia nimeota ndoto tu kuwa fulani ataondoka soon na yalitokea hivyo

Naongea haya kwa kuwa kuna wakati alimtabiri kiongozi wetu kifo na kusema ameoteshwa, Lema alikamatwa na kufungwa kwa mashtaka ya uchochezi lakini alipotoka jela bado alisema ndoto yake inajirudia rudia kuwa lazima huyo afe kama hajabadilika tabia

Godbless Lema Yeye haogopi anamwambia muhusika moja kwa moja kuwa yatamkuta matatizo mazito na Wengine anawaambia utakufa moja kwa moja, Nikiwaangalia baadhi naona hata afya zao zina mashaka makubwa sana

Uchawi ni sayansi kama sayansi zingine onyefu, Kuna baadhi ya watu wana maruani na viumbe vya kutisha wanatembea navyo huku wao wenyewe hawajijui ambavyo vinawapa nguvu kuona mambo ya hatari na yasiyoweza kuonekana kwa macho haya ya kawaida, Hawa wanapata taarifa ya msiba wako na ugonjwa wako kabla hata wewe huna dalili wala hujui lakini wao hufahamu na wanakuonea huruma

Utabiri upo karne na karne, Hata kwenye maandiko tunaambiwa kuna watu walikuwa na uwezo wa kusoma nyota na maandishi ya ajabu ajabu yasiyokuwa na maana lakini wao walitumia kutoa onyo au kutoa mawazo yao nini kinakwenda kutokea mfano wale Mama Jusi wa mashariki walipoona nyota tu wakahisi kuna kitu tofauti kabisa

Je anachofanya Godbless Lema ni uchawi au utabiri?

Kama ni utabiri kwanini utabiri wake unawakumba wale tu anaowatamkia uovu Wanaofanya na wala atabiri mambo ya Furaha kama mvua kunyesha vizuri na mengine mazuri

Kama ni sayansi ya uchawi kwanini tusimuombee aondokane na hayo maruani ya kutabiri vifo na mambo mabaya

Nimeanza kutishwa baada ya kuona Godbless Lema bado anawang'ang'ania watu fulani na mtu fulani kuwa ataondoka soon, Sasa ndoto hizi zinatufanya wana ccm kuanza kumuogopa maana akikutabiria unaweza ukapata presha kabla ya ndoto kutumia na watu wakatumia ndoto ya Lema kumbe tatizo ni Presha
 
Ngoma ya Magu ilivuma sana, kwa vyovyote vile lazima ingepasuka!

Hata Ndugai ilifikia mahali anaongoza kitu kisichokuwa na uelekeo, halijulikani ni bunge au kijiwe cha kahawa au kamati ya mazishi, yaani lilikuwepokuwepo tu!
Asingeweza kufika mbali, alishatoka kwenye misingi
 
Matendo ya Magufuli yalikuwa ya HOVYO sana na yalikuwa hayamfurahishi Mungu. Kwa mfano anawatoa kazini wenye vyeti FEKI na kuwanyima mafao, huku unambakiza Makonda mwenye cheti feki kama Mkuu wa mkoa.

Unawabomolea nyumba bila kuwalipa watu wa Kimara, halafu nyumba za wasukuma wa Mwanza unasema zisibomolewe.

Watu wanatoa Kodi lakini wana mbunge wa UPINZANI Magufuli anasema hapekeki maendeleo.

Anawanyanga'anya matajiri fedha kwa kisingizio cha ufisadi kisha kuwatupa rumande.

Halafu Jumapili anakwenda Kanisani na kusema "niombeeni". Tukuombee nini shetani mkubwa Magufuli?

Kwa kweli tulimuombea afe. Na ndiyo maana hata Lema akayaona maombi yetu
 
Sasa ndoto hizi zinatufanya wana ccm kuanza kumuogopa maana akikutabiria unaweza ukapata presha kabla ya ndoto kutumia na watu wakatumia ndoto ya Lema kumbe tatizo ni Presha
Kumuogopa Lema bila kubadili matendo haisaidii.
Mihimu ni kuogopa matendo maovu na kutenda yaliyo mema.

Si vema kutabiria wenzako mabaya, lakini kuonesha mahali ubaya ulipo ili kutafuta mabadiliko chanya sioni kama ni tatizo.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
Matendo ya Magufuli yalikuwa ya HOVYO sana na yalikuwa hayamfurahishi Mungu. Kwa mfano jnawatia kazini wenye vyeti FEKI na kuwanyima mafao, huku unambakiza Makonda mwenye cheti feki kama Mkuu wa mkoa.

Unawabomolea nyumba bila kuwalipa watu wa Kimara, halafu nyumba za wasukuma wa Mwanza unasema zisibomolewe.

Watu wanatoa Kodi lakini wana mbunge wa UPINZANI Magufuli anasema hapekeki maendeleo.

Anawanyanga'anya matajiri fedha kwa kisingizio cha ufisadi kisha kuwatupa rumande.

Halafu Jumapili anakwenda Kanisani na kusema "niombeeni". Tukuombee nini shetani mkubwa Magufuli?

Kwa kweli tulimuombea age. Na ndiyo maana hata Lema akayaona maombi yetu
Vyeti feki apewe mafao ya nini kwanza alitakiwa apelekwe mahakama kwa makosa ya udanganyifu
 
Hakuna mtabiri hapo, wahuni wenzie wanamfikishia mipango inayopangwa dhidi ya watu fulani.

Siasa za kiafrica kazi kubwa iko nyuma ya pazia na haya tunayooneshwa kwa nje ni maigizo tu.
 
Kuna mambo siyo ya kuyaletea mzaha hata kidogo, Wengi yamewakuta na wengine wametwaliwa moja kwa moja kutokana na kile kinachoitwa ndoto anazooteshwa Godbless Lema iwe kwa kutamka hadharani au kutoa meseji kupitia akaunti yake ya twitter

Mwanzoni nilifikiri Godbless Lema anaangalia afya za wahusika yaani physical appearance na kuwatabiria Kifo na majanga, Hii ya kumuangalia mtu jinsi alivyo, anayoongea hata mimi nikiwa na umri wa utoto kabla ya kuanza kujihusisha na dhambi nilikuwa na uwezo wa kujua huyu ana shida na hata Chukua raundi ataondoka moja kwa moja yaani Kwaheri ya kuonana na Nilitamka kwa ndugu na hata wazazi waliona kama ninatisha tisha hivi lakini niliwaambia nimeota ndoto tu kuwa fulani ataondoka soon na yalitokea hivyo

Naongea haya kwa kuwa kuna wakati alimtabiri kiongozi wetu kifo na kusema ameoteshwa, Lema alikamatwa na kufungwa kwa mashtaka ya uchochezi lakini alipotoka jela bado alisema ndoto yake inajirudia rudia kuwa lazima huyo afe kama hajabadilika tabia

Godbless Lema Yeye haogopi anamwambia muhusika moja kwa moja kuwa yatamkuta matatizo mazito na Wengine anawaambia utakufa moja kwa moja, Nikiwaangalia baadhi naona hata afya zao zina mashaka makubwa sana

Uchawi ni sayansi kama sayansi zingine onyefu, Kuna baadhi ya watu wana maruani na viumbe vya kutisha wanatembea navyo huku wao wenyewe hawajijui ambavyo vinawapa nguvu kuona mambo ya hatari na yasiyoweza kuonekana kwa macho haya ya kawaida, Hawa wanapata taarifa ya msiba wako na ugonjwa wako kabla hata wewe huna dalili wala hujui lakini wao hufahamu na wanakuonea huruma

Utabiri upo karne na karne, Hata kwenye maandiko tunaambiwa kuna watu walikuwa na uwezo wa kusoma nyota na maandishi ya ajabu ajabu yasiyokuwa na maana lakini wao walitumia kutoa onyo au kutoa mawazo yao nini kinakwenda kutokea mfano wale Mama Jusi wa mashariki walipoona nyota tu wakahisi kuna kitu tofauti kabisa

Je anachofanya Godbless Lema ni uchawi au utabiri?

Kama ni utabiri kwanini utabiri wake unawakumba wale tu anaowatamkia uovu Wanaofanya na wala atabiri mambo ya Furaha kama mvua kunyesha vizuri na mengine mazuri

Kama ni sayansi ya uchawi kwanini tusimuombee aondokane na hayo maruani ya kutabiri vifo na mambo mabaya

Nimeanza kutishwa baada ya kuona Godbless Lema bado anawang'ang'ania watu fulani na mtu fulani kuwa ataondoka soon, Sasa ndoto hizi zinatufanya wana ccm kuanza kumuogopa maana akikutabiria unaweza ukapata presha kabla ya ndoto kutumia na watu wakatumia ndoto ya Lema kumbe tatizo ni Presha
Jina lake tu ni ishara tosha ya kumuwezesha kunena kwa lugha yaani "God bless Lema".
"Mwenyezi mbariki Lema"
 
Hakuna utabiri wowote amewahi kuutoa huyo Lema.

Anachofanya ni KUWAOMBEA MABAYA tu WABAYA wake kwa kujifanya anawatahadhalisha.

Mfano Magu kafa kwa kudharau COVID-19 na siyo kwasababu eti kawadhibiti wapinzani.

Sabaya ni system imemtema nje baada ya aliyekuwa anamlinda kufa. Ila hata sasa anaweza kusamehewa na akarudi kawaida.

Ndugai kapishana tu na Rais na wala hakuna uadui huo mkubwa maana ataendelea kuwa spika mstaafu.
 
Hakuna mtabiri hapo, wahuni wenzie wanamfikishia mipango inayopangwa dhidi ya watu fulani.

Siasa za kiafrica kazi kubwa iko nyuma ya pazia na haya tunayooneshwa kwa nje ni maigizo tu.
Kwahiyo vile vile alipewa taarifa na watu kuwa magufuli atakufa?
 
Hakuna utabiri wowote amewahi kuutoa huyo Lema.

Anachofanya ni KUWAOMBEA MABAYA tu WABAYA wake kwa kujifanya anawatahadhalisha.

Mfano Magu kafa kwa kudharau COVID-19 na siyo kwasababu eti kawadhibiti wapinzani.

Sabaya ni system imemtema nje baada ya aliyekuwa anamlinda kufa. Ila hata sasa anaweza kusamehewa na akarudi kawaida.

Ndugai kapishana tu na Rais na wala hakuna uadui huo mkubwa maana ataendelea kuwa spika mstaafu.
Sasa akiwaombea mabaya na kweli yanakuwa yamewapata hii unaitaje?

Hizo zinakuwa sababu kuelekea kutimilika kwa jambo.
 
Back
Top Bottom