TALAKA KATIKA UKRISTO
Katika kitabu cha Mathayo Yesu aliulizwa juu ya talaka aksema Mussa aliruhusu kwasababu ya ugumu wa mioyo yenu na alitoa ruksa kwa sababu ya uzinzi na kuikana imani. ..ingawa msamaha ni msistizo kwa mkristo.
(Mst. 6-8) – Hakuna talaka katika ukristo. Mwanadamu YEYOTE iwe ni Mchungaji, Askofu, Jaji wa Mahakama Kuu ya Rufaa au yoyote hana ruhusa kumtenganisha mtu na mkewe, na cheti chochote cha talaka ni batili, hakitambuliwi na Mungu. Mungu alichukuliana na watu wa Agano la Kale kwa ugumu wa mioyo yao, lakini hachukuliani na yeyote katika Agano Jipya kwa suala la talaka. Hata kama mke ameachwa kwa talaka potea, hana ruhusa kuolewa na mwingine (1 WAKORINTHO 7:10-11).
KUMWACHA MKE KWA SABABU YA UASHERATI (Mst. 9) – Hiki ni kisingizio cha watu wengi wasio na maarifa kuwaacha wake zao. Nyakati za Biblia mtu alipotoa posa kwa mchumba wake, hata kabla hawajaoana, waliitwa mtu na mkewe (KUMBUKUMBU 22:23-24; MATHAYO 1:18-20). Katika uchumba, kama mke huyo alithibitishwa kuwa amefanya uasherati kwa kuwa na mimba au vinginevyo ilikuwa ni halali kumwacha maana ni dhahiri kwamba siyo mwaminifu. Ni kwa sababu hiyo Yusufu alitaka kumwacha Mariamu kwa kudhani alifanya uasherati. Vivyo hivyo, katika Kanisa, watu ambao bado ni wachumba, hata kama posa imekwisha kutolewa; mmojawapo anapothibitika kuwa amefanya uasherati, huyo mwenzake ana ruhusa ya kumwacha kwa sababu inadhihirisha kwamba hajaokoka. Lakini mtu na mkewe wakiisha kuoana, uzinzi siyo sababu ya kuwaruhusu kuachana. Mume anapaswa kumsamehe mkewe mara saba mara sabini makosa YOTE kama Mungu katika Kristo alivyotusamehe sisi. Je, tulisamehewa dhambi zote kasoro uzinzi? Jibu ni la! Basi uzinzi siyo kisingizio cha kumwacha mke (WAEFESO 4:32).
Mathayo 19