Je, Ndoa ya kikristo yaweza kuvunjika?

Je, Ndoa ya kikristo yaweza kuvunjika?

Ndoa ya Kikristo huvunjwa na kitu kimoja tu; kifo peke yake. Hakuna kingine chochote kinachoweza kuivunja. Biblia haijichanganyi. Neno la Mungu linasema; Alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe, Full Stop.
Ushauri. Kabla hujaingia kwenye taasisi hii alioianzisha Mungu, fikiri kwanza. Tena mnaojifurahisha atii ni UZINZI unaoweza kuwatenganisha. Huko ni kujifurahisha. Kila mtu hupenda kujitafsiria apendavyo bora tu iwe vyema upande wake. Neno la Mungu linasimama lenyewe.
Kuhusu mawifi na wakwe. Umeolewa na mwanamume suruali. Hajijui wala hajui wajibu wake. Mume ndo kichwa cha nyumba, sio wakwe/mawifi/mashemeji. Tatizo ni kujikusanyia kwa baba na mama mkwe. Unaoa huna nyumba wala kitanda. Huna kipato unatarajia kula na kunywa kwa baba na mama. Huwezi sema lolote weye ni kudhalilishwa tu.
Mwanamume, mpende mkeo, kama Kristo alivyo lipenda kanisa hata akautoa uhai wake kwa ajili yake. Huyo mwanamume wako aweza kweli kuutoa uhai wake kwa ajili yako?? Kwa kuwa ulimpenda mwenyewe, vumilia. Ila vikikushinda, tafuta mahali ukae hapo, ila bila kidume kingine. Mumeo akikuwinda, asikupate kwa lolote. Iko siku, atakufuata, nawe mwambie; Hama kule, kuja hapa tuishi pamoja.
Zama zimebadilika sana, ndoa zote zinasimamiwa na serkali na chombo chenye mamlaka kuvunja ndoa ni mahakama peke yake. Soma sheria ya ndoa ya Tanzania. Kuna ndoa nyingine watu wanaishi kwa unafiki, wanakuwa ndani ya nyumbamoja lakini kila mmoja ana mtu wake na anazini naye, kipi bora hapa kuvunja ndoa au kuishi kwa unafiki. Ndoa nyingi za kikiristo zimevunjwa na watu wamelewa na kuoa kibao
 
Back
Top Bottom