Samwel Maleka.
Pole kwa hali ya maisha unayopitia, mie niko kwenye ndoa for almost miaka 16 yrs, nafahamu changamoto nyingi sana za ndoa na zingine inakubidi uwe na busara na hekima ya Mungu kuzitatua.
Changamoto unazopitia ni matokeo ya maamuzi ambayo uliyafanya huko nyuma bila kufuata hekima kama zilivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu, ngoja nikupe siri ambayo naamini inaweza isikusaidie sana wewe lakini itawasaidia wale ambao wanatafuta wenzi wa maisha.Kwa asili wanaume tumetawaliwa na tamaa za ngono, na ndizo zinazotufanya tuangukie kwenye mapenzi na wanawake wazuri. ambao wanaitesa mioyo yetu maisha yetu yote,,mfano Samson na Delila
Katika kuoa inabidi uangalie mwenza ambaye anakutii tangia mwanzo wa uchumba wenu, na ukipata ambaye hajawahi kuwa na mahusiano na mtu mwingine akuwa the best kushinda yeyote.
Nasikitika sana uliachana na mchumba wako ambae umekiri ulimtoa usichana wake, if it was me! that was the best woman to be my wife..naomba nikueleze ukweli ni vigumu sana kumbadilisha tabia mkeo kwani ndani ya moyo wake haupo wewe, na tambua kwamba mwanamke anajua kupenda sana, na hayumbishwi na mazingira yanayomzunguka. hivyo basi ana mtu wake ambaye yuko moyoni mwake tangu mwanzo. Pili huenda ni mdogo sana kiumri hivyo bado hajajua ktk maisha ya ndoa ni nini wajibu wake kama mke, na chakusikitisha zaidi kama anakunyima unyumba sipati picha kwani mwishowe utajikuta unahangaika na wanawake wengine wa nje ili kutuliza tamaa zako, na lile lengo la msingi la kuwa mke na mume, kutulizana tamaa zenu linakuwa limepotea kabisa..
Mawazo yangu kwako ni ongea na mkeo in very friendly manor wanawake sio waongo pale wanapokuwa na mtu wanayemwamini, atakueleza yaliyoko moyoni mwake then kuanzia hapo ndio utajua cha kufanya.
Pili mnaweza kutengana kwa muda yeye akarudi kwa wazazi wake au wewe ukarudi kwa wazazi au katafuta mahali pa kuishi kama miezi 3, hiyo itawapa muda mzuri wa kutafakari na kuona kama kila mmoja anamhitaji mwenzake.
Unaweza ukaongea na watumishi wa Mungu ambao wanakulea kiroho wakusaidie mawazo ila tambua, ndoa ni makubaliano kati ya watu wawili, na kwa msingi wa bibilia ndoa inaweza kuvunjika japo sio mapenzi ya Mungu, endapo mtafanya zinaa nje ya ndoa, kumtendea matendo ya hiyana mkeo mfano kuomba bando la halichachi.
Ukitaka ushauri aidi njoo pm nitakuapitia mawasiliano, hapa nimeandika kifupi sana
Nakutakia kila la kheri.....