Unaambiwa kosea kujenga na sio kuoa...
Bila kupepesa macho kosa ni lako wewe. Sijui huwa mnakuwa na maana gani kusema huyu mke hakuwa wa ndoto zangu, halafu bado ukamtia mimba na kumuoa. Huo ni upuuzi uliopitiliza.
Umesema mwanzoni kabisaa alikuwa a nawasiliana na ☓ halafu ulivyo na akili nyingii ukamwambia chagua mmoja, huku ukijua fika una mchumba wako umpendae mkuu hapo ndo ulianza kujipika mwenyewe....
Baadae mchumba wa ndoto zako akarudi, bado yule uliyempa nafasi ya kukuchagua unampa kipigo kitakatifu sababu tu eti ana wivu na wewe?????!
Maumivu yake yalianzia hapo sababu alijua fika humpendi na hilo ulimtamkia mwenyewe ingawa sio sahihi anavyolipiza kisasi lakini chanzo ni wewe apo...
Msiwe mnaendeshwa na hisia, fuata moyo wako. Huko kuna uliyempotezea muda kwa miaka 7,unafikiri machozi yake yatakuacha salama???!
Kaa na mkeo ongea nae na ikiwezekana mpe mipango yako ya talaka, sioni ndoa hapo mie naona mafahali wawili wako kwa boma moja