Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,712
- 830,726
Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga ametoa taarifa ya kifo cha Dickraka Mwamakula (24) aliyekuwa askari wa Jeshi la Magereza katika Mkoa wa Njombe. Na kwamba, kijana Mwamakula alipotea tarehe 7 Septemba 2025.
Lakini baadaye mwili wake umepatikana ukiwa amefukiwa shambani baada ya kuchomwa moto na wauaji wake. Na kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni Erasto Mlelwa (26) ambaye pia alikuwa ni askari wa Jeshi la Magereza amejiua akiwa chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi.
Maelezo ya Kamanda ni kuwa Mlelwa aliruka kutoka katika gari la Polisi akaangukia kichwa na hivyo kupoteza maisha. Hapa nina hoja kadhaa ambazo zinaelekea kulituhumu Jeshi la Polisi.
1. Mtuhumiwa wa mauaji au hata mtuhumiwa yeyote akikamatwa na Jeshi la Polisi hufungwa pingu katika mikono yote.
2. Mtuhumiwa aliyekamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi, akifungwa pingu huzungukwa na askari Polisi.
3. Mtuhumiwa anaposafirishwa akiwa chini ya ulinzi mambo matatu hufanyika kwa wakati mmoja: hufungwa pingu; huzungukwa ama huwekwa kati na askari wenye silaha; mwisho hufungwa kamba katika nguzo yeyote ya gari. Kuna wakati anaweza pia kufungwa kitambaa usoni ingawa huu ni unyama usiokubalika.
Sasa hoja yetu ni hii:
1. Inakuwaje mtuhumiwa aliyefungwa pingu mikononi, akafungwa kamba katika nguzo ya gari, akawekwa kati na askari wenye silaha au akafungwa kitambaa akaweza kuruka kutoka ndani ya gari hiyo?
2. Je, huyo mtuhumiwa hakufungwa pingu na hayo mengine? Kama hakufungwa pingu, kama hakufungwa kwenye nguzo ya gari na pia kama hakuzungukwa na askari, ni kosa la nani?
Hoja yangu ya pili inahusu kauli ya Kamanda Banga. Ana sema wakati anaruka kulikuwa pia na askari wa Magereza. Kamanda anajenga pia hoja kuwa huyo askari magereza ameshuhudia tukio hilo na hivyo anataka tuamini kuwa kweli Mlelwa amejiua.
Kamanda anataka tumtilie shaka zaidi. Je, nani amehoji hadi yeye aanze kuthibitisha? Kwa nini Kamanda Banga anajitetea mapema kabla hata hatujamhoji! Hata sababu ya kuwa Mwamakula ameuawa kwa wivu wa kipandishwa cheo nayo pia haina mashiko. Kamanda Banga hajasema kuwa Mwamakula alikuwa na cheo gani na pia hao wauaji walikuwa na cheo gani!
Kauli ya Jeshi la Polisi Njombe inazua utata mkubwa. Inatufanya tuamini kuwa kifo cha Mwamakula na 'kujiua' kwa Mlewa. Natoa wito kwa mamlaka zilizo juu ya Kamanda Banga ili zifanye uchunguzi katika mambo matatu: kifo cha Mwamakula, kifo cha Mlelwa na utata wa kauli za Kamanda Banga.
Je, ni nani hasa kamuua Dickraka Mwamakula? Kwa nini amemuua? Je, ni kweli Mlewa kajiua? Kama hajajiua, ni nani kamuua na kwa nini? Ni hatari kuchepusha hoja kwa sababu aliyeuawa ni Mwamakula na anayetetea ni Mwamakula. Tumalize kwanza hili ndipo tujue marehemu ni nani kwa Askofu Mwamakula.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 21 Septemba 2025; Saa 10:37 jioni