Je mzee punch alikufa lini?

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,886
1,193
Kwa wale tuliofaidi elimu ya bure kwenye University of Dar-es-salaam, enzi tulipokuwa tunakula makuku, mayai na maziwa yaliyokuwa yanatoka kwenye mabomba, tutakumbuka kwamba kulikuwa na kiumbe kilichokuwa kinaitwa Mzee Punch. Hiki kiumbe kilikuwa na kazi moja kubwa sana ya kudiscipline wanafunzi, wafanyakazi wa chuo na viongozi wa serikali wale ambao hawakupata bahati ya kufunzwa na wazazi wao. Kwa kuelezea maisha yao yote tangu walipozaliwa, mikasa mbali mbali waliyokumbana nayo na mengineyo. Kwa ufupi mtu alikuwa anavuliwa nguo kwenye ukuta. Mtu alikuwa anapewa jina la utani lakini picha anachorwa copyright.

Mzee Punch anaaminika alikuwepo tangu wanaweka jiwe la msingi la chuo. Alikuwa anasoma lakini alikuwa ha-graduate wala harudii mwaka. Mzee punch alianza kupotea wakati University ilipoanza kuwa "Choo Kikuu cha Dar-es-salaam". Wakati wanafunzi walipoanza kula kwa mama ntilie, kulala kitanda kimoja wanne nk. Je Wana JF waliomfahamu mzee Punch wanaweza kunisaidia kufahamu kama alikufa lini au aliamua ku-graduate na kuondoka? Maana vijana wa chuo sasa hivi wameporomoka sana kimaadili kwa sababu hawapati "Ten commandments za Punch" wanapojiunga na chuo
 
ah huenda aligraduate na kuondoka.
<br />
<br />. Acha kusifu upuuzi, nyie mliosoma miaka hiyo hapo UDSM, mkapata kazi straight serikalini, na mkapata kuishi na huyo panchi wenu, mmeifirisi serikali kwa uizi na ufisadi wenu. Pamoja na kwamba mlikuwa mna pitia JKT kujifunza uzalendo, hamna chochote nyie wazee mlicholifanyia taifa zaidi ya uizi na ufisadi,mmeinyonya serikali kama kupe, mpaka tumefilisika. Hebu tueleze elimu uliyopata UDSM wakati wa pechi, sijui pachi, imesaidia vipi Taifa. Acha vijana walete mabadiliko mmefilisi vya kutosha. Inawezekana, inawezekana mlitoka na patch za PANCHI wakati mnamaliza UDSM, ndio maana mnatoa tu upepo mtaani. Hamna kitu,hamna uzalendo mmeangamiza taifa tu.
 
Punguza munkari kijana, kumbuka sisi ni wazazi wako!!
 
Back
Top Bottom