Yani kifupi ni kuwa huyo aitwaye shetani ameshinda, Mungu anawachukuwa watu kuwakimbiza mbinguni coz tayari shetani amejimilikisha dunia, dunia iliyoumbwa na Mungu.Kwa namna hiyo mkuu hizi dini tunapoteza mda tu hakuna logic ukiwaza sababu za watu kuokoka na kwenda mbinguni!
Yaani MUNGU awapeleke wanadamu mbinguni baada ya shetani kuitwaa dunia kwa uwezo wake.
@sakayo kumbuka amri za Mungu zilikuja baadaye sana.Sisi sote tu wake, ila tunaamua kukaza shingo kwa kutokuzifuata amri zake! Kwa maana hiyo tunajitenga wenyewe[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji120]
Maana hata atheists nao ni hivyo hivyo,ukiangalia huu mjadala utagundua hilo.Kwasababu wengi wamelelewa na kukulia kwenye ukristo
Hahaaaaa!! Unaambiwa mbinguni zilichapwa kinoma mpaka jamaa likaamua kushuka duniani lenyewe,Yani kifupi ni kuwa huyo aitwaye shetani ameshinda, Mungu anawachukuwa watu kuwakimbiza mbinguni coz tayari shetani amejimilikisha dunia, dunia iliyoumbwa na Mungu.
Halafu ujue hawa wawili wanakutana sana, tangu shetani afukuzwe huko juu.Hahaaaaa!! Unaambiwa mbinguni zilichapwa kinoma mpaka jamaa likaamua kushuka duniani lenyewe,
Halafu MUNGU akamtuma Yesu kuhubiri injili akarudi tena mbinguni.
Bado linachanja mbuga tu.
Mpaka sasa naamini kuna mpango mkubwa kati ya shetani na MUNGU.
Dini ni mpango wa shetani.
Halafu tunahenyeshwa sisi, mda huo anasema anatupenda sana.Halafu ujue hawa wawili wanakutana sana, tangu shetani afukuzwe huko juu.
~Walikutana kipindi Ayoub anataka kujaribiwa, wakakubaliana kuwa Ayoub ajaribiwe tu ila asiuwawe...WALIKUBALIANA.
~Walikutana tena Yesu alipokuwa akijaribiwa huko nyikani, ila Yesu akamfukuza baada ya shetani kufanya mzaha na utani.
Kumbe bwana wanakutana na kukubaliana kabisa...Dah!!
Ahahahaahaahahahhahahah vikao vya kamati kuuHalafu ujue hawa wawili wanakutana sana, tangu shetani afukuzwe huko juu.
~Walikutana kipindi Ayoub anataka kujaribiwa, wakakubaliana kuwa Ayoub ajaribiwe tu ila asiuwawe...WALIKUBALIANA.
~Walikutana tena Yesu alipokuwa akijaribiwa huko nyikani, ila Yesu akamfukuza baada ya shetani kufanya mzaha na utani.
Kumbe bwana wanakutana na kukubaliana kabisa...Dah!!
Dini gani unakusudia?Dini ni hofu ya wanadamu!
Shetani yupo ili watu wamjue Mungu na nguvu zake Bila dhambi ni vigumu kujua mema ni yapi, na Bila shetani uwezi kujua Mungu Ana nguvu zipo, so vyote havikutokea kwa bahati mbaya, mwisho Mungu hafanyi makosa wala haijawai kukosea wala hata kosea yupo juu ya sheria yeye ndio sheria yenyewe, kuhusu kufa baada ya dhambi, je ni kweli kama dhambi isingefanya tungeishi milele hapa dunia na kujaa watu la, kifo kipo tu kwa kuwa yote yalipangwa kuwa tokea si kwa bahati mbaya, je Ana upendo ndio kwa herufi kubwa maisha yangekuwa sio matamu kama tusingepewa nafasi ya kuchagua mema na mapya,Wakuu hamjambo!
Kama kichwa cha Uzi huu kinavyouliza, Mimi nikiri kuwa naamini uwepo wa Mungu mmoja aliyeumba vyote vinavyoonekana na visivyoonekana pia.
Katika vitabu mbali mbali vya dini, tunaelezwa kuwa dhambi ilitokana na uasi alioufanya shetani dhidi ya Mungu, biblia inaenda mbali kwa kudai kuwa vita vilipiganwa huko mbinguni na shetani alishindwa na akatupwa duniani akiwa na theluthi ya malaika wakawa upande wake.
Maswali:
1. Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile, tena alikuwa mbinguni kwenye utakatifu wa MUNGU, je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi Ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?
2. Kama MUNGU hujua mwanzo hata mwisho wa viumbe vyake, INA maana alikuwa anajua kuwa shetani atakuja kuasi baadae na kusababisha dhambi, kwanini alimuumba?
Jambo la kufikiria hapa ni kuona kwamba MUNGU alimuumba shetani/Lucifer ( dhambi) mahususi ili kuja kuwa upande maovu. Dhana hii inadhihirisha kuwa MUNGU ndie aliyeumba dhambi.
3. Je, lengo la MUNGU lilikuwa mwanadamu aishi milele bila kufa?
Hapa kuna mazoea yalishajengeka hasa kwa wakristo na waislamu kuamini kuwa isingekuwa Eva/Hawa kudanganywa na Shetani basi Leo hii wanadamu wasingekuwa wanakufa ( immortal). Hii dhana haina mantiki hasa ukiwaza kuwa wanadamu wangezaliana na kuishi milele bila kufa nadhani dunia ingekuwa imejaa mabara na visiwa vyote.
Hivyo MUNGU akaamua kuleta mauti ili kudhibiti ( control) idadi ya wanadamu duniani isizidi uwezo wa rasilimali zilizopo, fikiri Leo hii watu wanauwana kugombania ardhi je ingekuwaje akina Adam na bibi yetu Eva wangekuwepo wote?
4. Je, Dini ni matokeo ya mwanadamu kumhofia shetani?
Tunaishi katika jamii ambazo kila MTU ana juhudi za kujikwamua kuondokana na shida Kama magonjwa, njaa, vita, ambazo Mara nyingi wanadamu wanahesabu kuwa hayo yote ni sababu ya shetani, na dini wanaona ndio kimbilio ili kumkwepa shetani asiwadhuru.
Lakini wao wanaamini kuwa wanasali ili kumtukuza MUNGU, lakini kiukweli dini ni hofu ( fear of unknown) isiyo na ithibati yoyote.
5. Je, Mungu anawapenda wanadamu? Hapa jibu laweza kuwa ni ndiyo, bahati mbaya sana ukiangalia uhalisia toka zamani kuna ugumu wa kusema ndiyo au hapana.
Tunaambiwa kuwa mbinguni kulikuwa na vita Kali sana, mwaishowe malaika aitwaye Mikaeli alimshinda shetani, Mungu akamtupa ibilisi huyo huyo duniani kwa wanadamu anaowapenda sana. Mungu hakuona sehemu nyingine ya kulitupa hilo joka ila duniani ambako ndio wanadamu aliwaweka. Hii ni sawa na kuwarushia watoto wako furushi lenye nge wengi huku umewafungia chumbani na kuwataka wajikinge wasing'atwe hata kidogo.
Nimekuja kuamini kuwa: MUNGU yupo ila dini zote ni michezo ya kukamata fikra za wanadamu tu, inawezekana kabisa kuwa dini ziluletwa na shetani mwenyewe ili kuwachonganisha wanadamu wasiishi kwa upendo na amani.
Angalia jinsi Palestine na Israel, syria , Iraq n.k wanavyouana kwa misingi ya dini.
Niishie hapo, naomba waumini/maswahaba mje mtueleze hizi hoja.
Cc: Mshana Jr
Cc: Kiranga
Na wanajamvi wote karibuni.
Kuzaa na kuumba ni vitu viwili tofauti.Huwezi jipangia nizae mtoto mrefu au mfupi,lkn Mungu aliamua aumbe mfupi au mrefuJiulize, Ukizaa mtoto kisha akawa jambazi, Je unakuwa ulizaa jambazi?
Akiwa malaya, Je, Unakuwa ulizaa malaya?
Halafu tunahenyeshwa sisi, mda huo anasema anatupenda sana.
Nimefungua huu uzi mida hii nimesoma comments zote, one at a time.....haki Nimeogopa watu mnavyomkana Mungu!! Muumba wa Ardhi na Mbingu mbele yenu amekua si lolote si chochote?! Hatari sana dunia inaenda kasi ya ajabu!!
***Sorry sina maana ya kuwakwaza ila nimeshangaa sana, hadi usingizi umekata! !!!
UnajidanganyaHapa ndipo unapopata jibu kuwa hakuna mungu