Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,669
- 272,507
Inasemekana kwamba hata ambaye amenyimwa macho basi angalau anapewa uwezo wa kunusa na kupapasa, hanyimwi vyote.
Ukweli niliouona (maana macho ninayo) ni kwamba wananchi wengi wamelipuuza na kulidharau kabisa bunge jipya linaloendelea Mjini Dodoma, wadau hawana habari nalo wala hawataki hata kufuatilia yanayojiri, taarifa zinaonyesha kwamba namna wabunge hao walivyopatikana na namna uchaguzi wa 2020 ulivyoendeshwa ndio sababu kubwa ya wananchi kulipuuza bunge hili.
Hawaoni kama wabunge walioingizwa bungeni kwa mbeleko ya chuma huku wengine wakiingizwa ndani ya bunge bila kuwakilisha chama chochote cha siasa kama Katiba ya nchi inavyotaka, kuna mashaka mazito kama wabunge hawa wa kutengeneza maabara wanaweza kuhoji masuala ya msingi , kwa ujumla wananchi wameamua kujitenga na bunge hili japo juhudi za kulitangaza zimekuwa kubwa mno !
Nakulilia Tanzania .