Elections 2010 Je; Mtanzania Limeshikishwa Adabu na CHADEMA?

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Sipati picha imekuwaje leo Mtanzania linawafagilia Chadema kiasi hiki ambacho si cha kawaida?

Pata udondozi wa Kichwa Kikuu Cha Habari:

KAMPENI SI MCHEZO

Dk. Slaa Naye "Afunika"
- Ataanza kushughulikia Uzalendo
- Akosoa Sera ya CCM ya Kilimo Kwanza
- Aahidi Kupandisha Kima Cha Chini Hadi Sh. 350,000/=

attachment.php

.
Lazima kutakuwa na namna, si kawaida? ama wameadabishwa na Umati wa Jana hasa baada ya Marina kuponea Kipigo?
 
Attachments

  • DSC00033.jpg
    DSC00033.jpg
    50.8 KB · Views: 307
Hapana ni tatics zao mafioso wa CCM kujaribu kuthibitisha methali ya If you cant beat them, love/ join them.

Pia ile kashfa ya Mhariri mtendaji wao kuwa kinara wa kampeni za ccm na onyo walilotoa MCT kuhusu unazi wa wanahabari naamini kuna kitu wameambizana majambazi hawa kwamba tulegeze mwendo kwa sasa kisha soon our true colors will emerge.

Shetani hawezi kuongoka, sana sana atajifananisha na malaika wa nuru
 
Kwa kawaida gazeti hili huwa na mrengo wa kuipendelea CCM na kuiponda CHADEMA. Hata ile hoja ya Ukatoliki/Udini na Slaa ulianzia huko.

Pia imedaiwa Mhariri Mtendaji wa New Habari Bw. Mahigo Rweyemamu ni moja kati ya Waratibu wa Kampeni wa CCM.

Picha iliyotolewa pia inatia changamoto ya pekee kutoka gazeti hili.

Hii ni tofauti kabisa na Gazeti la Mzalendo linalomilikiwa na CCM ambalo nimedai watu walikuwa wachache huku kukiwa na kichwa cha habari kidogo kilichojinadi
- "Uzinduzi wa Kampeni CHADEMA Vurugu Tupu"
- "Mtangazaji TBC Nusura Adundwe"
 
Hapana ni tatics zao mafioso wa CCM kujaribu kuthibitisha methali ya If you cant beat them, love/ join them.

Pia ile kashfa ya Mhariri mtendaji wao kuwa kinara wa kampeni za ccm na onyo walilotoa MCT kuhusu unazi wa wanahabari naamini kuna kitu wameambizana majambazi hawa kwamba tulegeze mwendo kwa sasa kisha soon our true colors will emerge.

Shetani hawezi kuongoka, sana sana atajifananisha na malaika wa nuru

Ila ipo kazi bado watanzania wengi kuelimika . . .

Asubuhi nilikuwa naongea na sister wangu moja na jirani yake, bado wanaamini CHADEMA ni watu wa vurugu na watavuruga amani. Nilipowadodosa hawana hoja ila tu wao wanaona bora CCM pamoja na kuwa wanajua nini Slaa kafanya.

Bado CHADEMA wanayo kazi ngumu ya kuwashawishi watu kama hawa waelewe.
 
mkuu hapo tambua namna sumu ya ccm ilivyowadumaza na kuwapofua watanzania.
Watanzania wapo radhi watoto wao wawe manamba baada ya kukosa elimu bora ilimuradi wamtumikie baniani mbaya. kaaaz kweli kweli.

Jana nilikutana na kanali mmoja mstaafu (mzee) anaiponda chadema akisema kuwa hawana lolote zaidi ya kukosoa tu. Nadhani kuna tatizo ktk mfumo wa elimu nchini kuanzia ngazi ya chini mpaka elimu ya juu.
 
Ishu kubwa ipo kwa akina mama wengi wao wanaogopa mabadiliko na ni wanachama na wapeleka habari wakubwa wa CCM (sio wote lakini wako majemedari humo). Na nimekuja kugundua kikubwa kinachowafanya wasibadilike mtazamo ni woga kwamba vurugu ikitokea Tanzania watoto wao, waume zao au wanaume zao na ndugu zao watadhuriwa. Kazi bado ipo sana kuwaelemisha kwani katika itikadi za kisiasa ni mtazamo na sio vita na tofautiano za kimtazamo haimaanishi sie ni maadui.
 
kushoto hapo kwenye gazeti wameandika BOB MAKANI ADONDOKA JUKWAANI DAR...!
 
Kamanda Mahesabu, huwezi kuamini, hata habari hii ya Bob Makani ukiisoma imeandikwa in a positive way. Hakika uandishi wao wa leo umekuwa ni tofauti kabisa.
 
Sipati picha imekuwaje leo Mtanzania linawafagilia Chadema kiasi hiki ambacho si cha kawaida?

Pata udondozi wa Kichwa Kikuu Cha Habari:

KAMPENI SI MCHEZO

Dk. Slaa Naye "Afunika"
- Ataanza kushughulikia Uzalendo
- Akosoa Sera ya CCM ya Kilimo Kwanza
- Aahidi Kupandisha Kima Cha Chini Hadi Sh. 350,000/=

attachment.php

.
Lazima kutakuwa na namna, si kawaida? ama wameadabishwa na Umati wa Jana hasa baada ya Marina kuponea Kipigo?

Washenzi hawa usishangae wakatoa copy chache tu ....Check kama limefika mikoa yote
 
mkuu hapo tambua namna sumu ya ccm ilivyowadumaza na kuwapofua watanzania.
Watanzania wapo radhi watoto wao wawe manamba baada ya kukosa elimu bora ilimuradi wamtumikie baniani mbaya. kaaaz kweli kweli.

Jana nilikutana na kanali mmoja mstaafu (mzee) anaiponda chadema akisema kuwa hawana lolote zaidi ya kukosoa tu. Nadhani kuna tatizo ktk mfumo wa elimu nchini kuanzia ngazi ya chini mpaka elimu ya juu.

Mimi nashauri CHADEMA kama wakiweza, wawe wananunua strategic Airtime katika TV na Redio ambazo Watanzania wengi wanasikiliza. Vipindi hivi viambatane na Muziki ambavyo Watanzania wengi wanapenda.

Kupitia vipindi hivi Sera za CHADEMA na Elimu ya kutosha itolewe ili wengi waweze kushawishika.

Magazeti pia yatumike kila siku kuelezea sera kwa lugha nyepesi na hata ya picha au cartoon bila kuleta hadithi nyingi. watanzania wengi si wasomaji. Zitengenezwe DVD zilizoambatana na Muziki safi na zigawiwe kwa wingi huku vijarida vidogo vinavyoonyesha vipaumbele kwa lugha nyepesi vikigawiwa.
 
Ishu kubwa ipo kwa akina mama wengi wao wanaogopa mabadiliko na ni wanachama na wapeleka habari wakubwa wa CCM (sio wote lakini wako majemedari humo). Na nimekuja kugundua kikubwa kinachowafanya wasibadilike mtazamo ni woga kwamba vurugu ikitokea Tanzania watoto wao, waume zao au wanaume zao na ndugu zao watadhuriwa. Kazi bado ipo sana kuwaelemisha kwani katika itikadi za kisiasa ni mtazamo na sio vita na tofautiano za kimtazamo haimaanishi sie ni maadui.

Unajua mfumo wa CCM wa kuwa na balozi wa nyumba kumi umeimarika sana. Katika mitaa tunayoishi, ikitokea issue katika mtaa inayoitaji ufumbuzi lazima watu waende kwa "Mjumbe" na huyu Mjumbe happens kuwa wa CCM. Imekuwa kana kwamba hawa ni viongozi wa Mtaa.

Ukienda Bbaadhi ya enki au Polisi katika issues mbali mbali, lazima utaje kwanza Mjumbe wako ni nani ili mambo mengine yaendelee.
 
mtu66
nimeshawishika kukubaliana na hoja yako
wahuni hawa

Hivi kuna uwezekano kama huo? Si itakuwa hasara kwao? Au ndo wameshapata mgao?

Maana kwa sasa hata ukiangalia quality ya gazeti hili ni ya juu sana almost full colours hadi ndani both picha na some texts tofauti na ilivyokuwa zamani.
 
Unajua mfumo wa CCM wa kuwa na balozi wa nyumba kumi umeimarika sana. Katika mitaa tunayoishi, ikitokea issue katika mtaa inayoitaji ufumbuzi lazima watu waende kwa "Mjumbe" na huyu Mjumbe happens kuwa wa CCM. Imekuwa kana kwamba hawa ni viongozi wa Mtaa.

Ukienda Bbaadhi ya enki au Polisi katika issues mbali mbali, lazima utaje kwanza Mjumbe wako ni nani ili mambo mengine yaendelee.
Nadhani ni vyema tukiomba ufafanuzi kuwa mjumbe huyu anachaguliwa kwa kupitia njia zipi? Kama anachaguliwa ndani ya chama basi tuna kila haki kusema kuwa mjumbe wa nyumba kumi hawezi kuwa official wa serikali... nadhani ni vyema kuanzisha thread nyingine ili tuichambue mada hii vizuri.
 
Kiongozi,

Naungana na wewe katika hili. lakini bila ya shaka huu ni ukweli usiopingika na ulio zoeleka.

Ni vema vyama vya Ushindani vikabuni muundo mbadala wa kuipiku CCM kama kweli tunataka wananchi wengi wafungue akili zao.
 
SUPERMAN, MSANII NA MDONDOAJI- kama kweli tumeamua kuhakikisha tunapambana na ufisadi kwa kuiletea Tanzania mabadiliko, ni lazima tuwafikishie wananchi walio wengi hususan akina mama na wote wanaogopa vurugu, machafuko vita n.k namna matatizo hayo elimu ya Political Science tuliyobahatika kuipata kuhusu mchango wa mfumo huu tulio nao wenye kujenga matabaka katia ya walio nacho na wsio nacho na mchango wake katika kusababisha vurugu, machafuko na hata vita.

Kila mmoja wetu ajielimishe vyanzo vya machafuko hayo katika nchi mbali mbali na kuwaelimisha wananchi walio nyimwa elimu hiyo. Na hiyo mkazi haiwezi kufanywa na Dr Slaa, Zitto, Mbowe, Mnyika peke yao.

Ni kazi inayotakiwa kufanywa na kila mmoja wetu na sio hapa kwenye JF ila ni kwa wananchi.

Kwa upande wangu wananchi hususan akina mama wana haki ya kutilia shaka hali hii kwa kuwa ndio wanavyofundishwa, nani amejitolea kuwapatia upande wa pili wa shilingi kwa mifano kutoka mataifa mbali mbali?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom