Elections 2010 Je, Mtanzania gani anafaa kuwa Rais wetu 2010?

Nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2010-2015?

  • Jakaya Mrisho Kikwete (CCM)

    Votes: 591 23.9%
  • Willibrod Slaa (CHADEMA)

    Votes: 1,785 72.1%
  • Ibrahim Lipumba (CUF)

    Votes: 89 3.6%
  • Hashim Rungwe (NCCR-Mageuzi)

    Votes: 7 0.3%
  • Mutamwega Mugahywa (TLP)

    Votes: 7 0.3%

  • Total voters
    2,475
  • Poll closed .
this poll does not reflect the actual image of presidential votes, coz majority of tanzanian does not have opportunity to access internet and ICT skills, and many of them lives in the remote areas.:confused2:
 
Ni kama ushabiki wa mchezo,let's say football.Anayeonekana ni mfungaji,lakini bila teamwork hamna kitu.Rais ataonekana ni mzuri iwapo tu supporting sructures zinazounda serikali zitakuwa ni nzuri kiutendaji kwa maana ya real committiment ya mtu mmoja mmoja mpaka ngazi ya juu.Yeyote anaweza.
 
ukiangalia kila kiongozi tanzania ni fisadi.na kila siku humu watu tunakaa na kujadili na kulalamika sana kuhus viongozi wetu hawa.

Swali ni je tumekaa na kufikiria ni nani atafaa kuingoza tanzania kunako 2010?.maana hiyo 2010 siyo mbali atii, hivi sasa tupo tunaingia april 2009 inamaana sasa hivi ni wakati muafaka wa kuandaa wagombea wa kiti cha uraisi 2010 (iwe ccm or chadema,cuf etc).

Mimi nadhani ni wakati muafaka akijitokeza mwanamke hii 2010 kugombea hicho kiti cha raisi, it doesnt matter anatokea chama gani.wako smart women kwenye tanzanian politics wengi tuu ambao wana qualify.mfano akina anna makinda (very smart and strong woman) na wala siyo fisadi.

ukiangalia kwenye uchaguzi wa marekani watu wengi walikuwa hawaamini kabisa marekani ingeweza kuongozwa na mwanamke.look at hilary alikuwa kidogo tuu achukue uraisi,she never back down no matter what ali-stand up strong.i believe kuna wamawake tanzania wako strong and smart kama hilary clinton.


jamani binti maringo - dont be so sure - hivi inawezekana asiwe fisadi huyu??? Amehodhi ardhi nyingi tu katika mfumo wa viwanja (wala sio shamba) na hadi leo ameweka tofali tele na kwa vile kuna miti - imekuwa kichaka cha vibaka - kama ni mwadilifu kweli na anafaa kuwa rais - hivyo viwanja kapataje na vimemzidi??? So far wengi wana ccm waliokuwa madarakani wana tamaa sana - akipata urais ..................kama leo ana tamaa hivyo basi ataishia nayeye kuruka na ndege kutembelea nchi ambazo alikuwa hajawahi kuziona maishani mwake - ....................... Unless mungu aingilie kati - najua umedhania hivyo lakini mpendwa mh! Wala ............ Wenye spirit ya nyerere wachache sana - wanaume kwa wanawake!!!
 
ANAYEFAA KUWA RAIS KWA 2010 NI DR. W. SLAA - AT LEAST AMEFICHUA MAOVU YALIYOKUWA TUMEFICHWA WATANZANIA - KWA KUASHIRIA KUWA YAMEMWUMIZA HATA YEYE - AT LEAST RAIS ANATAKIWA AWE NA UCHUNGU NA MALI ZA NCHI YAKE - SIO AWE WA KWANZA KUFUJA, KUWAPA MARAFIKI VYEO KWA UPENDELEA HATA KAMA HAWAWEZI, KUWALINDA MAFISADI NA KUFUMBIA MASIKIO KILIO CHA WANANCHI WAKE

KWA MTAZAMO WANGU NADHANI DR. SLAA ANAWEZA KUITWA BABA WA TAIFA na Watanzania tukiwa WATOTO WAKE - hawezi kutupa JIWE BADALA YA MKATE; NYOKA BADALA YA SAMAKI -............................ IFIKE MAHALI NA SISI PIA TUFAIDI UTAJIRI WA TANZANIA ALIOTUPA MUNGU AMBAYE NDIYE ALIYETUWEKA TANZANIA

INAWEZEKANA IF WE AGREE FOR CHANGE 2010 -
 
Mimi kutokana na mchakato wa kiamaisha na jinsi awamu ya sasa ilivyopelewa kwa kweli mimi nampigia Dr. Wilbroad Slaa.
 
Nionavyo mimi hatuna sababu ya kupiga chenga nyingi kwenda kwenye jibu. Ukweli ni kuwa nchi hii kwa sasa haina mwelekeo. Sababu ya kusema hivyo ni kuwa hakuna sheria hata moja inayotekelezwa. Kuanzia sheria za barabarani, usafi, mipangomiji, uhalifu wa ulevi wa madawa na bangi hadi chochote ukijuacho. Hii ina maana kuwa sheria zimekosa usimamizi na wale waliopewa DHAMANA ama kazi imewashinda au ni wababaishaji. Sababu kubwa ya hali hii ni kuwa hata yule anayewateua wasimamizi hawa ameshindwa kuwawajibisha. Nionavyo mimi hakuna sababu nyingine ila ni kuwa kama ni samaki basi ameoza kuanzia kichwani. Hapa tunachohitaji sio rais pekee bali tunataka mfumo mzima ufumuliwe. Tunahitaji taasisi ya urais yenye mwelekeo mpya isiyolinda wahalifu kwa kigezo cha aina yoyote ile. Jibu ni rahisi kwani wananchi wenye uchungu na nchi hii wanaenda kumchagua rais mbadala. Msijali sana haya maneno ya kijinga ya wavaa T-shirt na kofia za kifisadi kwa vile wamejaliwa unafiki mkubwa na kwa bahati mbaya hawana uwezo wa kusoma alama za nyakati. Kwa kifupi nchi inahitaji mabadiliko makubwa na wanaoweza kuyaleta sio hawa waliopo madarakani kwa sasa. Tunahitaji massive overhaul.
 
Ndani ya JF kuuna UHURU wa mawzo na maoni, ila nafikiri uuhuru huu usitupeleke mahali tukawa watu w "FUNY" hasa inapofika mustakabali wa nchi! Sio lazima kila MADA utakayoikuta uichangie. Kukaa nkimya SOMETIMES ni HEKIMA hasa kama utakuwa huna cha kusema.

Luv you guys

Regards

Albert
 
Sio unaona. Ndivyo ilivyo. hivi katika wagombea waliojitokeza yupo aliyeonyesha dhamira ya kuwatumikia watanzania kidhati kama Dr. Slaa kihistoria ya maneno na utendaji? Rais atufaaye ni yule ajuaye utajiri wa nchi hii, ni yule aliye tayari kutumua utajiri tulionao kuleta maendeleo na si ategemeaye kuomba omba kwa wahisani (wanyonyaji)
 
Kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja kati ya hao waliopendekeza anasifa muafaka za kuwa Rais wa Tanzania.
Watanzania tuna matatizo makuu yafuatayo:
(1) Kudorola kwa huduma za afya.
(2) Elimu: shule za secomdary na vyuo vikuu bado ni vichache na hata curriculum zetu bado hazikidh international standard,
(3) Njia kuu za uchumi zimeporwa na wageni watanzania wamebaki mikono mitupu
(4) Ajira
haya ndiyo matatizo yetu
 
Mpenda watu, mchukia mafisadi, anaesema elimu bure, matibabu bure, asietaka kufanya kazi kwa shinikizo
 
NO LEADERSHIP CHANGES NO ECONOMIC CHANGES.

Mabadiliko yanakuja pale unapoyahitaji,Huwezi ukasema eti unategemea mabadiliko yoyote wakati wewe mwenyewe hutaki kubadilika.
Ili uweze kuona mbele zaidi pengine yakupasa usimame palipoinuka zaidi.....!!
Wakati huu ni lazima tuangalie mtu mwenye uwezo wa kuona mbali zaidi ya maraisi waliopita ktkt awamu zote.!
Mwenye uwezo wa kutenda kazi kisomi zaidi. atajalije Elimu iwapo tutachagua mtu ambaye kwake yeye Waganga wa jadi ,wachawi na wanajimu ndio dira yake....! Uliona wapi mganga wa kienyeji mwenye mafanikio.....
 
mtanzania anayefaa kuwa Raisi ni yule aliyeonyesha kulisimamia vema taifa lake katika nyanja za maendeleo ya jamii kwa muda wa miaka mitano tumeona jinsi mabadiliko ya maendeleo yalivyopiga hatua ambayo haikutegemewa ndani ya kipindi hiki kifupi cha miaka miaka mitano.mimi sio mwana siasa ila sitaki kuwa mnafiki kwa kujifanya eti sioni kazi kubwa aliyoifanya JK yenye kuonekana ambayo haiitaji hata maelezo mtu aanze kukuelezea.hivyo mimi kama mtanzania mzalendo moja kwa moja nataka JAKAYA KIKWETE ndiyo awe Raisi wa Tanzania kwa mara nyingine ili aifikishe nchi inapotakiwa iwe kama alivyoianza.
 
Kwangu mimi ninataka mageuzi katika nchi hii. Tatizo tulilonalo ni kwamba CCM wameshinda hata kabla ya kura kupigwa. Kwanini nasema wameshinda? Mipango yote ya upigaji kura wameratubu wao kupitia kibaraka wao TEC. Kibaraka wao Tendwa naye ndivyo alivyo amekuwa akitoa statement za hapa na pale za kuonyesha upendeleo dhahiri kwa CCM. Jeshi na Polisi nao wameingia kwenye mkumbo wa kuwakumbatia CCM. Kwa vyovyote vile, kuna kila dalili kuwa hata kama kura hazitafika lakini kwenye matangazo wataongeza namba na kabla ya hapa na pale tayari JK keshaapishwa. Tunahitaji kuwepo na transparent system kuanzia uandikishaji wa wapiga kura na wakati wa kupiga kura. Wananchi wanahitaji pia elimu ya uraia ili wajue kuwa maendeleo yote ni haki yao kupata, lakini tunahitaji kuwa na kiongozi atakayesimamia sera na siyo kiongozi wa kwende kutoa ahadi za kujenga barabara za kata and daraja za kata. Sasa diwani na mbunge watatoa kauli zipi? Tunahitaji mtu anayeweza kuikemea system nzima na atakayeweza ku'overhaul" system nzima iliyooza na kuweka system yenye transparency katika utendaji wake. Kwangu mimi Dr. W. Slaa angeweza kuwa kiongozi huyo ninayemtarajia lakini infrastructure zilizopo haziwezi kumwezesha kuingia Ikulu kwa sasa. Lakini Nawasihi wapenda mageuzi wote wapige kura za ndiyo kwa kiongozi toka kwenye chama mbadala halafu tuone hawa jamaa wanavyoamua kuiba wasi wasi.
 
Hapa swala la muhimu ni kuchagua kiongozi mwenye sera za kueleweka na sio mbabaishaji.
 
Back
Top Bottom