Je mmesikia kuhusu MATOPONI Network?

Msindima

JF-Expert Member
Mar 30, 2009
1,018
33
Habarini wadau wa JF,je mmewahi kusikia kuhusu Matoponi network?
Hii ni kampuni imeanzishwa hapa Arusha,wanavyodai waanzilishi ni kwamba ukitaka kujiunga u have to buy a form kwa shs 5000,then in that form u will find three people,wa kwanza atakua step 1,namwingine step 2,na watatu atakua step 3,baada ya kupata hiyo form utakwenda bank na kumwekea pesa aliyepo top position (step 1) utamwekea shs 20000 na 20000 nyingine utaweka katika account ya hao Matoponi network,then utatengenezewa form zako tano nawe itabidi utafute watu wengine watano ili uwauzie na wakaweke pesa kwenye account za watu ambao wamewakuta wako top position kwa madai yao ukifanikiwa kuuza form zote utapata shs 2,500,000,sijaelewa kuhusu haka kamchezo
naomba mwenye data atuwekee tupate kuelewa zaidi.
 
Hii ni ile ile micheozo ya pyramid scheme, ni upatu kama dollar jet. wakwanza wanapata, wa mwisho wanaliwa. ni ya kuogopa kama ukoma!.
 
heheheh,hiyo kali,,,,,,watu wanapenda dezo kwelikweli,easy money business
 
Huo mchezo kama ndiyo umeanza let say hauna zaidi ya mwezi jaribu kufuatilia then jiunge, michezo hii ya upatu huwa wanafaidika watu wa mwanzo....ila kama una zaidi ya miezi mitatu kaa mkao wakuliwa.
 
Habarini wadau wa JF,je mmewahi kusikia kuhusu Matoponi network?
Hii ni kampuni imeanzishwa hapa Arusha,wanavyodai waanzilishi ni kwamba ukitaka kujiunga u have to buy a form kwa shs 5000,then in that form u will find three people,wa kwanza atakua step 1,namwingine step 2,na watatu atakua step 3,baada ya kupata hiyo form utakwenda bank na kumwekea pesa aliyepo top position (step 1) utamwekea shs 20000 na 20000 nyingine utaweka katika account ya hao Matoponi network,then utatengenezewa form zako tano nawe itabidi utafute watu wengine watano ili uwauzie na wakaweke pesa kwenye account za watu ambao wamewakuta wako top position kwa madai yao ukifanikiwa kuuza form zote utapata shs 2,500,000,sijaelewa kuhusu haka kamchezo
naomba mwenye data atuwekee tupate kuelewa zaidi.

Best ungejaribu kuingia ili utupatie uzoefu ili tuzidi kucheka....
 
Huo mchezo kama ndiyo umeanza let say hauna zaidi ya mwezi jaribu kufuatilia then jiunge, michezo hii ya upatu huwa wanafaidika watu wa mwanzo....ila kama una zaidi ya miezi mitatu kaa mkao wakuliwa.
Hii yote ni matokeo ya umaskini wa WaTZ,ni sawa na DECI ni wizi mtupu.
 
Tunahitaji kitu kama "Security and Exchange Commission" ku- regulate hivi vitu, yaani mtu anatangaza Pyramid scheme bila kificho kabisa.
 
NDUGU TAFADHALI EPUKA HAYO MADUDU YA PESA ZA HARAKA..... Hata kwa Mungu tumekatazwa
 
Mwaka 2007 kulikuwa na FAIDA Investiment,ilikuwa kama hii ila yenyewe ilikuwa na watu wanne kwenye fomu na watano ilikuwa ni kampuni yenyewe.Kiwango chao ilikuwa ni shs 10elfu kwa kila mmoja.So ililazimika kudeposit tsh 50elf.Walikuwa wanakupa kadi ukishadeposit ksha unaendelea kuzisambaza.Ilishtukiwa na CRDB bank ile ambao ndo walikuwa banker wao.Ilipovunjika watu wengi(hasa wanavyuo vya elimu ya juu) walibaki na kadi zao mikononi na jamaa wakatokomea.
 
Last edited:
Matoponi network!!! hii ni upatu full stop... kama kuna asiyejua upatu, aangalie similarities na upatu uliofungwa mwaka 1994 pale posta ya zamani ....baada ya hapo ujajua nini maana ya kuuza form hizo..
 
Naona hawa hawajafanya hata effort yoyote ya kuficha kuwa ni Pyramid Scheme, hehe! Angalau DECI wanawadangaya watu kwa "Mbegu" na "Mavuno" na "Siri za Kibiashara".
 
Mwaka 2007 kulikuwa na (FAIDIKA au FAIDA),ilikuwa kama hii ila yenyewe ilikuwa na watu wanne kwenye fomu na watano ilikuwa ni kampuni yenyewe.Kiwango chao ilikuwa ni shs 10elfu kwa kila mmoja.So ililazimika kudeposit tsh 50elf.Walikuwa wanakupa kadi ukishadeposit ksha unaendelea kuzisambaza.Ilishtukiwa na CRDB bank ile ambao ndo walikuwa banker wao.Ilipovunjika watu wengi(hasa wanavyuo vya elimu ya juu) walibaki na kadi zao mikononi na jamaa wakatokomea.

You are right 911, Huo mchezo wa UPATU kama wengi walivyosema wanaofaidika ni watu wa kwanza , baadaya ya hapo utasikia hooo Polisi wamewakamata wahusika, ukienda ofisi zimefungwa , ukitaka kudai pesa zako humwoni wa kumdai kwani mara zote huwa wahusika hawana mahali maalum wanapopatikana.

Mwaka 1994 wengi waliokuwa pale Chuo kikuu cha Dar e s salaam mtakumbuka ulikuwepo huo mchezo na tulikuwa tunatuma pesa kwenye Money Order ilikuwa siyo nyingi mia tano tu, lakini by that time it was much. Ulikuja ukafungwa na Polisi kwa minajiri ya kuwa mchezo wa kitapeli, na pesa zetu hazijarudishwa hadi leo. Mwaka juzi 2007 nimeona tena Dar mchezo huo wakiita FAIDIKA, nikaamua kufanya uchunguzi nikakuta ni kama ule ule wa zamani, na nimekutana na watu wengi wanacheza na wameweka pesa zao, Nikajaribu kuwa tahadharisha lakini sikio la kufa ........ Wiki iliyofuata Polisi wanatangaza kuwakama wahusika na kuwaweka ndani, mara wengine wamekimbia. Lakini pesa za watu hazijarudi hadi leo!!!!

Na sasa kuna mchezo mwingine unaitwa PUFDEA ofisi zao zipo pale Manzese Tip Top wanajitangaza kwenye vyombo vyote vya redio kuwa wanasaidia kutoa mikopo isiyo na riba na kutoa misaada ya pesa za kujenga shule, na kutoa ajira. Nimefanya juhudi za kufika na kuongea nao, inaonekana kama jamii ya Upatu kwani ukifika pale unaambiwa kwanza nunua FORM ( 2000) single page, Pili utalipa kiingilio 300,000/- then kama ni mwanafunzi atasaidiwa kusoma hadi chuo kikuu. Nikauliza kama kuna watu wameanza waliniambia wanasubiri wawe wengi, thata was last year 2008 by August. Nimekwenda tena last month baada ya kusikia bado wanaendelea kutangaza, wanazidi kufungua branches mikoani na kukusanya pesa za watu, but No one ameshapewa hizo pesa.

Mikoani wanawambia wananchi wanawasomesha kwa wiki mbili , then wanawapa ajira za kuelimisha wengine wajiunge, na wanawambia ili wasome hiyo course ya wiki mbili walipe ada ya 540,000/=

Kama kuna aliyepata kufaidika naomba atuambie hapa ili tumwulize maswali ya msingi.

SWALI HAPA: Kwa nini vyombo vya dola vinaanza kufuatilia baada ya watu kuibiwa """1!!!!!! na kwa nini wakati mchezo unaanza tu wasifuatilie?? Au kun wakubwa wapo behind ?? . Najua if you are an intellegent people trained to do so, You MUST be aware of what is going on katika society zetu. Na kwa kuwa tunaishi nao hawa watu ni dhahiri wanajua haya.
 
Back
Top Bottom