Je, mila hizi zina maana gani?

Saidama

JF-Expert Member
Jun 10, 2022
500
944
Kuna vitu mpaka kufkia utu uzima wangu huu nimeshaviona ila sijawai kujua maana yake. Bila kupoteza muda;

Cha kwanza ni hii ya wauza maduka kutokuuza sindano majira ya usiku. Hii niliithibitisha mimi kwenyewe siku moja. Nilitoka usiku kwenda dukani kununua sindano, nikaenda duka la kwanza(kwa MUHA) akaniambia hana sindano, nikaenda maduka mengine mawili(kwa MSUKUMA na MCHAGA) majibu yakawa yale yale hamna sindano.

Sasa wakati narudi hom nikawa nimeongozana na bro mmoja napiga nae stori. Katika stori stori nikamwambia "mi nilikua nimeingia shop apo kununua sindano nimekosa, nimeona nirudi hom tu". Uyo bro ndo akaniambia "sindano haziuzwagi usiku" ila hakunambia kwanini. Hili ni swali najiuliza mpaka leo.

Swala jingine ni hili hua naskia tu ila sijawai kushuudia madhara yake wala kujua ni kwanini. Mara nyingi mama yangu alikua akinieleza kua kukata kucha usiku ni vibaya na kunizuia kila nilipokua nataka kufanya hivyo. Je kuna ubaya gani kukata kucha usiku?

Watalamu wa mambo nisaidieni majibu kwenye haya
 
Kuna vitu mpaka kufkia utu uzima wangu huu nimeshaviona ila sijawai kujua maana yake. Bila kupoteza muda;

Cha kwanza ni hii ya wauza maduka kutokuuza sindano majira ya usiku. Hii niliithibitisha mimi kwenyewe siku moja. Nilitoka
Huyo muuza duka pesa zake za uchawi
 
Endelea kuzidumisha mila hizo bila kuziacha, huku ukiendelea kuuliza kwanini iwe hivyo!
Nalog off  Z
 
Hayo yote ni sahihi kabisa ila ndo hivyo hadi leo cjafanikiwa kujua sababu za haya

Jambo jingine ni ukienda dukani usiku ukamwambia muuza duka naomba CHUMVI hupewiii, ukirudi nyumbani unaambiwa nenda kaseme dawa ya mboga hapo shwari kabisa

Mshana Jr
 
Imani za kusadikika zilizojaaa vichwani mwa mitanganyika mingi. Watu walioelimika wanauza na kununua hizo bidhaa muda wowote bila wasiwasi wowote ule.
 
Madukani unauziwa vyote hivyo muda wowote unaotaka labda kama ulienda kwenye vioski na magengeni

Kucha tunakata mpaka usiku wa manane na wala hakuna shida yoyote

Kwa kukuongezea tu...

Tunashona mpaka tunakesha hasa vipindi vya sikukuu na wala hakuna tatizo

Baada ya kula usiku tunafagia na tunazoa uchafu usiku huohuo ili asubuhi tukiamka tuwe tumepunguza majukumu tuwahi mihangaikoni

Tunataja sana nyoka na wanyama wakali wakali wengine (mpaka kutishiana) pindi tuwapo maporini na wala hakuna shida yoyote

Tunageuza sana nguo (nje ndani) hasa tisheti ili kuzuia isipauke na wala hakuna shida kabisa

Tunashonea nguo (vifungo na kadhalika) huku tumezivaa ili kuokoa muda na kweli muda hautuachi

Lakini...

Hatushoni nguo huku tumevaa wala hatumshonei nguo mtu akiwa amevaa siyo kwasababu ni uchuro kwamba ni kama unashona sanda laa bali ni kujihadhari na kudhurika kwa vifaa vya kushonea

Hatushoni usiku wala kufagia/kumwaga uchafu usiku kwajili ya kuepuka kujidhuru kwa sindano kwa kutokuona vizuri pia kuepuka kudhurika na taka ngumu jalalani kama chupa na wanyama hatari majalalani kama mbwa

Hatupokei watoto mlangoni maana ni uchuro inakuwa kama unapokea maiti pia kuepusha kuanguka au kumwangusha mtoto wakati wa kupea au kupokea kwajili ya vikwazo vya mlangoni (ngazi, urefu wa mlango nk)

Hatuli chakula kwa (ncha ya) kisu si kwamba kwajili tutapata kichomi bali ni tahadhari tusije kujidhuru kwa kisu

Hatupitishi sufuria ya chakula nyuma ya wazee (watu wazima) si kwajili ni mwiko bali kuepusha tusije chafua watu hao kwa masizi

Hatuli kwenye sufuria si kwajili ya mwiko wa wawindaji ila ni kwasababu tukila kwenye sufuria maana yake ndo chakula chote kimetengwa tukila je wengine watakula wapi? (hasa watoto wakihisi njaa baadae)

Hatuli kwenye sahani siyo kwajili ni sheria bali chakula cha kwenye sahani kimepoa na sisi tunataka cha moto (huku zamani hakuna hotpots)

Hatutajiani wala kutishiana vitu vya hatari kama chui na nyoka tuwapo porini kwani kuna wengine wana kiwewe na presha plus uoga wanaweza kufa kabla ya siku zao

Hatupigi winja/mluzi usiku si kwajili eti ni kumwita shetani bali ni kuepusha kelele za mwitikio wa sauti ambapo kwa usiku itasikika sana

....

Yapo mengi sana lakini hayo nimeweka kama mifano watu wa zamani waliyafanya mwiko kulingana na kipindi hicho na mazingira waliyokuwa nayo... kwa sasa kuna yanayobaki hivyohivyo na mengine yanabatilika kwakuwa mazingira yanaruhusu kubatilisha

Kwenye hoja yako kuna mjumbe hapo juu amejibu vizuri sana, kama ni kinyume na hadhari mfano wa hizo hapo juu basi WAUZAJI AU WANUNUAJI HAO WANAHUSISHA NA UCHAWI
 
Back
Top Bottom