Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,681
- 1,698
Wakuu,
Mpaka sasa ukisikiliza Radio One pana tangazo la mkuu wa mkoa wa Kagera akiomba mchango kwa ajili ya janga la tetemeko la ardhi lililotokea huko.
Bahati njema nchi yetu inatembelewa sasa hivi na mfalme wa nchi ya Morocco na tumetiliana mikataba takribani 20 hivi na nje ya hapo bwana huyu kajitolea kujenga msikiti mkubwa hapo Mzizima achilia mbali ombi la Rais wetu la kujengewa uwanja mkubwa wa michezo Dodoma.
Sasa najiuliza kama mheshimiwa mfalme kaambiwa kuhusu tetemeko hilo ni tegemeo langu angetoa pesa ili kumaliza kabisa zoezi la michango kwa jambo hili.
Maadam bado yupo nchini kwani ni jana tu kaelekea Zanzibar basi taarifa apelekewe au mkuu huyo wa Kagera aruhusiwe kumuona na kumweleza jambo hilo. Tuwe na utaratibu wa kufikia tamati kwa kila jambo.