Je, Meli ya Mv Victoria ni mbovu?

Je, Meli ya Mv Victoria ni mbovu?

Iinawez kuwa umetoa tahadhari nzuri sana lakini umendika kwa kifezuri, hata hivyo chombo chochote kuwa na hitilfu ni kawaida hata kama ni kipya muhimu wataalamu kufanyi uchunguzi, lakini punguza ujinga.
 
Hii habari imekaa kizandiki.. eti meli ilizima tena ikabidi watu wafaulishwe kwenye maboti. Kweli habari kama hii source pekee iwe jamaa wako wa karibu??!! SMDH!
 
Siyo kazi ndogo wanayoifanya kina Zitto na Lissu!!

Mwishowe mmeshika somo sasa!...

Unatukana ili iweje .. binafsi nilikuwa kwenye io meli siku io
Katukane ndugu zako sio kila kitu ulete dharau bana kama unaona huwezi kuandika bila kutukana watu pita katukane boda boda wa mtaani kwako
 
Kweli nmesikia hizo habari kwa Vijana wa chadema juzikati walikuwa wanaiponda saaana
Kwa vijana wa chadema? Waongo hao ndo unaamini habari zao? Hujui kuwa sera ya chama chao ni kuponda kila kitu? We ona tu wanavyoponda hata zahanati na health center zinazojengwa!
 
Huu uvumi ulianzia facebook, aliyeuweka akaukana na kusema account yake ya facebook ilidukuliwa, alichosahau pia kwenye account yake zipo picha na jumbe mbali mbali za ki- kamanda wa chama kile cha rais wa Ubelgiji....nadhani jamaa atakuwa anasaidia TCRA, ujinga huo naona umeletwa hapa na Mods wapo kimya tu! Tunampa shida Melo kulinda ujinga wetu huu!
 
Hahaha inaelekea kuna abiria wanapanda meli na misumari wanatoboa hizo meli.

Baadaye waanze kutumia kadi za ccm kupanda meli, wapande ccm tu ili wakifa kwa maelfu isiwe tatizo la taifa liwe la ccm pekee.

Wapinzani mnatoboa meli mpya hiyo!?
 
Hii meli ilipark pale bandari ya Mwanza kusini(Mwanza South Port) kwa miaka mingi

Hivi karibu kwenye utawala wa Magufuli meli hii imekarabatiwa kwa kupakwa rangi na kutengenezwa baadhi ya sehemu ,inasemekana hadi Injini ilibadilishwa

Hivi majuzi kuna jamaa yangu wa karibu alisafiri na hii meli kwenda Bukoba, kwa kweli kwa maelekezo yake hii meli ni Kimeo, ilizimika Mara kadhaa njiani wakati Mvua inanyesha na baadhi ya maeneo kupitisha maji

Siku kadhaa nyuma meli ilizima tena ikabidi watu wafaulishwe kwenye maboti

Meli imekaribia bandari ya kemondo ikazima tena

Sasa muhimu kuchukua tahadhali mapema ili kuepusha majanga

Serikali isipende sifa kwamba imetengeneza meli kumbe meli yenyewe mtego tu wa kuua watu

Source: abiria wa kwenda BkView attachment 1633137
Inatafutwa kafara
 
hebu muelimishe kwa fact.
Kufaulishwa kwenye boti (Lifeboat)au Life raft ni pale meli inapopatwa na majanga makubwa sana kwamba kuishi ndani ya meli ni hatari kwa maisha ya binadamu hao.
Sababu kubwa ni moto,ikiwa meli itaunguwa kiasi hakuna jinsi ya kuuzima moto, AU meli imekumbwa na majaga makubwa yanayoipelekea kuzama.
Katika hali kama hiyo kingora maalumu kitapulizwa na watu wote watakusanyika kwenye eneo salama.
Baadae itatolewa AMRI na Nahodha kama bado yupo hai au Msaidizi wake na kutamka neno ABADON THE SHIP.Ndipo hapo boti zitatelemshwa majini na kufaulisha watu kwa kasi.
Kwa kesi ya New Victoria kuzimika kwa meli hakuleti hatari ya kufaulisha watu kwenye boti kama alivyodai mtoa hoja.
 
Wewe dogo Mungu anakuona,wewe hujui meli,wala hujui unalosema ETI MELI ILIZIMIKA WAKABIDI WAFAULISHE WATU KWENYE BOTI.
Tupe wewe basi ukweli maana inaonekana kuna kitu unajua
 
zile kesi za akina Melo zilisababishwa na taarifa kama hizi lakini ni habari muhimu kwa wananchi
 
Acha upuuzi ndugu..
Meli ilizima mara 3
Siyo kazi ndogo wanayoifanya kina Zitto na Lissu!!

Mwishowe mmeshika somo sasa!

Yaani mnaamua kuwa waongo mchana kweupe kuwashinda hata walimu wenu siyo?

Yaani mzigo unaobebwa na Meli ufaulishwe kwenye boti??

Pumbavu Hadi walimu wenu!!
 
Ni kweli ndugu
Hili sina uhakika nalo, ila kuwa miundombinu mingi ni substandard ili kusaka political millage, hilo halina mjadala. Inawezekana mzigo haukifaulishwa bali watu ili kuokoa maisha yao. Lakini kwakuwa vyombo vya habari haviko huru, huwezi kusikia hili kwenye vyombo rasmi vya habari zaidi ya huku mitandaoni. Hivyo wangalau tunaona 50% kuna ukweli, na 50% tunasubiri udhibitisho.
 
Back
Top Bottom