SI KWELI Je, mchanganyiko wa Papai na Asali ni hatari?

SI KWELI Je, mchanganyiko wa Papai na Asali ni hatari?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wakuu

Nimesikia kutoka kwa mdau mmoja akieleza kuwa amewahi kusikia ama kuambiwa kuwa mchanganyiko wa asali na papai ni hatari.

Je, uhalisia upoje?

1763965567144.png
 
Tunachokijua
Kwa mujibu wa makala ya afya iliyochapishwa na MedicalNewsToday inaeleza kuwa Papai ni miongoni mwa matunda yenye virutubisho vingi. Papai lina virutubisho kama vile viambato vya kupambana na Oxdants (antioxidants) na Potasium. Faida zinazowezekana za kula papai ni pamoja na kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari, saratani, na mengineyo.

Hata hivyo, papai bichi lina utomvu wa papai (papaya latex) ambao una kimeng’enya kinachoitwa papain. Kumeza kiasi kikubwa cha kimeng’enya hiki kunaweza kuharibu umio, lakini hatari hii ni ndogo sana unapokula papai lililoiva.

Zaidi ya hapo, watu wenye mzio wa utomvu (latex allergy) wanaweza pia kuwa na alerji kwa papai, hivyo wanahitaji kuwa waangalifu wanapokula tunda hilo au kutumia bidhaa zinazotokana na papai.

Usalama wa mchanganyiko wa Papai na Asali

Dr. Yu Yongchao kupitia makala yake iliyochapishwa na Cainiu Health itwayo "Can honey and Papaya be aeten together?" anaeleza kuwa asali na papai ni mchanganyiko ambao unaweza kutumika kwa pamoja.

Dr. Yu anaeleza pia kwamba Papai na Asali vyote kwa pamoja vina utajiri wa virutubisho vyenye faida nyingi, mathalani asali ikiwa na virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kikohozi.

Kwa watu wengi mchanganyiko huu hauna madhara huku ukiambatana na faida mbalimbali ikiwemo kusaidia mmeng'enyo wa chakula au wale waliotoka kufanyiwa upasuaji.

Baadhi ya tafiti pia zinaonesha ufanisi wa juisi yenye mchanganyiko wa Asali na Papai katika kutibu baadhi ya magonjwa, mathalani utafiti uliofanywa na Dali pamoja na wenzake mwaka 2022, wenye kichwa "The Effect of Giving Mixed Juice of Papaya (Carica papaya) and Honey(Lyopercisum Esculentum) on Intensity of Stomach Pain in Patients withGastritis" Unabainisha kuwa


Matokeo ya utafiti uliofanywa kwa washiriki 60 waliokuwa wanaugua gastritis (uvimbe wa tumbo) yalionyesha kuwa kulikuwa juisi iliyochanganywa ya papai (Carica papaya) na asali (lycopercisum esculentum) ilikuwa na faida kubwa katika kupunguza kiwango cha maumivu kwa wagonjwa wa gastritis katika Kituo cha Afya cha IHC, Kijiji cha Talia.
Tahadhari

Mchanganyiko huu unaweza kuwa na athari kwa watu wenye mzio (Allergy) wa Asali ama Papai, wanaweza kupata wekundu kwenye ngozi ama uvimbe.
Back
Top Bottom