Je mawaziri wetu wana mgomo baridi? | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mawaziri wetu wana mgomo baridi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanahabari Huru, Mar 20, 2017.

 1. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 12,710
  Likes Received: 21,981
  Trophy Points: 280
  Naanza kuitafakari hofu yangu niliyokuwa nayo wiki kadhaa zilizopita, maana nilikuwa nahisi kuwepo Kwa mgomo baridi wa Baraza la Mawaziri, ama kile kinachoitwa 'Mawaziri kususa', ambacho hivi sasa nakiona wazi wazi.

  Ari na kasi waliyokuwa wameanza nayo Mawaziri ilikuwa ni kubwa sana, ilikuwa waziri akiingilia mlango huu, naibu waziri anatokea Kwa huku, yaani ofisi za umma zilichangamka na kila mtumishi wa umma alikuwa anasema "sasa hivi kazi tu, anaweza akaja waziri wakati wowote" yaani Waziri yupo mmoja, nchi ina mikoa zaidi ya 28, kila mtumishi katika kila mkoa alikuwa anadhani waziri anaweza kufika hapo Kwa muda huo huo, Kwa ufupi taifa liliingiwa na hofu kwamba awamu hii ssio ya mchezo, inachunguza na inafahamu kila kitu, wakati wote ukikosea unaonekana na utachukuliwa hatua papo Kwa papo..

  Lakini, katika awamu zote, awamu hii imekuwa ndiyo awamu ya kwanza kuingia madarakani na kuanza kuzodolewa na wananchi ndani ya muda mfupi sana. Ile mihemuko yote imepotea, matumaini yamekufa, ndoto ya mabadiliko imeyeyuka, Kwa ufupi ni kwamba Tanzania mpya iliyozungumzwa imeota mbawa na kupeperukia kusikojulikana.

  Mawaziri wamerudi nyuma, wamegundua kwamba wanafanya kazi ya MTU na sio ya nchi tena. Mawaziri wengi wamejisikia vibaya kudharauliwa nanushauri wao kupuuzwa, ilhali Mawaziri wetu wengi wao ni wasomi wazuri, wanauzoefu Mkubwa wa kiuongozi na hata baadhi yao walijiandaa kuongoza nchi, walichukua fomu za kugombea urais na kampeni za awali walifanya, hivyo watu Hawa wanapojihisi kudharauliwa na kupuuzwa, kwamba waendeshwe wote Kwa akili ya MTU mmoja, imewawia vigumu sana. Ndiyo maana tunasikia kwamba kuna masuala yanaamuliwa na Mawaziri mmoja mmoja bila kupitia kwenye vikao vya baraza la Mawaziri.

  Leo nchi inaendeshwa na watu wawili: yaani Rais wa nchi na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, katika shughuli za maendeleo anayeonekana ni Rais na Mkuu wa mkoa wa DSM, hata katika uzinduzi wa miradi ya maendeleo, ni Rais mwenyewe na mkuu wa mkoa was DSM, hata waziri akiwepo, uwepo wake hautambuliki, Bali wanaoonekana nankusikika vizuri ni Rais na mkuu wa mkoa wa DSM. Hii inawavunja mioyo Mawaziri ambao ndiyo wasimamizi wa Sera katika mawizara yote, na watendahi wao makatibu wakuu.

  Nikirejea aya iliyotangulia, ni kwamba utendaji kazi wa Mawaziri umedhoofika na umeshuka Kwa kiwango kikubwa sana, mshawasha waliokuwa nao kuhusu Tanzania mpya haupo tena, ziara za kushitukiza zimeonekana ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, siasa za ukali na visasi zimetawala, Mawaziri kama chombo cha kumshauri Rais kimegeuka na kuwa chombo cha kuelekezwa na kushauriwa na Rais.

  Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali Kwa mujibu wa katiba, na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, amekuwa akifanya shughuli zake kama kivuli cha Rais, haonekani kutekeleza majukumu yake kama Mawaziri wakuu waliotangulia, Kwa ujumla sasa nchi inaendeshwa Kwa akili moja.

  Watanzania ninawashauri kuwa wavumilivu lakini wenye kuitazama nchi inaelekea wapi na sio serikali inaelekea wapi, watanzania wafahamu kwamba sio hasara serikali ikianguka, Bali ni hasara nchi ikianguka, kwani serikali kuwepo madarakani ni Kwa makusudi ya wananchi wenyewe na wanao uwezo wa kuiweka madarakani serikali yoyote ile madhali wao wameamua, kwani Umma ndiyo wenye mamlaka ya mwisho katika nchi.
   
 2. Kkimondoa

  Kkimondoa JF-Expert Member

  #41
  Mar 20, 2017
  Joined: May 31, 2014
  Messages: 4,417
  Likes Received: 4,713
  Trophy Points: 280
  Naona mnaendelea kupungua kila siku kidogo kidogo , kwa sasa kambi inaongozwa na lizaboni,wakudadavua, laki si pesa, mwasita moja ila kundi kubwa limeingia mitin ,wacha tusubiri ingawa kuna wengine mna ID kama 10 hivi
   
 3. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #42
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,316
  Likes Received: 2,506
  Trophy Points: 280
  Najiuliza kwa sauti. SImbachawene anaweza kumpa maagizo Bashite akayatekeleze?
   
 4. Socratic

  Socratic JF-Expert Member

  #43
  Mar 20, 2017
  Joined: Dec 18, 2014
  Messages: 554
  Likes Received: 201
  Trophy Points: 60
  Fomu nilichukua mwenyewe na kura nilijipigia mwenyewe
   
 5. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #44
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,316
  Likes Received: 2,506
  Trophy Points: 280
  Najiuliza kwa sauti. SImbachawene anaweza kumpa maagizo Bashite akayatekeleze?
   
 6. Kkimondoa

  Kkimondoa JF-Expert Member

  #45
  Mar 20, 2017
  Joined: May 31, 2014
  Messages: 4,417
  Likes Received: 4,713
  Trophy Points: 280
  Wamemwachia waziri wa wizara zote tanzania bara achape kazi
   
 7. Kkimondoa

  Kkimondoa JF-Expert Member

  #46
  Mar 20, 2017
  Joined: May 31, 2014
  Messages: 4,417
  Likes Received: 4,713
  Trophy Points: 280
  Lazima mkubali kwamba kuna makabila si ya kupewa madaraka makubwa na nyerere aliliiona hilo lakin ccm wakalipuuza maana hawajui hulka za makabila .wengine wanatakiwa waachwe waendelee kuwa wa majarubani tu.
   
 8. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #47
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,963
  Likes Received: 1,712
  Trophy Points: 280
  ..wacha wagome ili huyu jamaa nchi imshinde...wacha mambo yawe doro watanzania wazidi kujua magumashi ya utawala huu....mtu anayesema hadharani kuwa hakuna wa kumwambia kitu unategemea nini??mawaziri wake wanamjua tangu huko kwenye vikao vya baraza la mawaziri anavyowapelekesha ki one man show...

  ...wacha wazire.....maana hata mwigulu ungetegemea aseme kitu kwenye uvamizi wa clouds lakini ame mute...wacha wawe hivyo hivyo....wadondoke pamoja na boss wao....ikifika 2020 kitaeleweka tu....btw...imebaki miaka 2 tu zianze pilika za uchaguzi....na kudai tume huru....hapo hadithi ya nchi ya viwanda itakuwa zilipendwa....na atakuwa amemaliza muda wake madarakani akikimbizana na wapinzani.....labda kwake chato ndio atakuwa amejenga.....na tutahoji.....ni muda tu utasema...
   
 9. Mpunilevel

  Mpunilevel JF-Expert Member

  #48
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 14, 2015
  Messages: 3,150
  Likes Received: 1,831
  Trophy Points: 280
  Sema baadhi sisi wengine tunaikubali kle mbaya.
  Acha kusemea nafsi za watanzania milion 50,ebo!
   
 10. xav bero

  xav bero JF-Expert Member

  #49
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 24, 2016
  Messages: 4,832
  Likes Received: 6,246
  Trophy Points: 280
  Sasa mnataka waseme nn zaod
   
 11. Titicomb

  Titicomb JF-Expert Member

  #50
  Mar 20, 2017
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 3,871
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa tangazo lile la Mwakyela mmh bora tu alivyopigwa stop. Mimi nilijiuliza sasa hivi huyu waziri anakunywa kinywaji gani kinamsababisha atoe matamko ya kutatanisha? 1. Serikali itaifuta TLS. 2. Kuanzia mwezi mei hakuna kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa.!!!!!! Kwa kauli hizi acha tu mkulu aingilie kati.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #51
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,544
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  Siasa zimefika mahala pake.. .tunavuna tuliyopanda. What else?
   
 13. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #52
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 14,311
  Likes Received: 3,265
  Trophy Points: 280
  Division Zero kawa waziri asiye na wizara maalumu,hata Kassim ana shangaa
   
 14. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #53
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,299
  Likes Received: 2,168
  Trophy Points: 280
  Mwehu huyo..anadhani walivyompa jk jina la dhaifu basi na huyu atawaendekeza..huyu anafyeka tu
   
 15. Alinda

  Alinda Platinum Member

  #54
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 1,542
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tatizo la hii serikali ya Magufuli ni kitohaminiana, unaona kabisa katika timu yake hakuna umoja, hakuna kuaminiana na hii inafanya kazi ya urais kuwa mgumu na kufanya viongozi wote kuanzia Maakamu wa rais mpaka kwa maawaziri kumuachia Magufuli afanye kile anachoona kinafaa.

  Na nafikiri Magufuli ni mtu wa visasi, hasira za haraka na maamuzi ya kukurupuka na mara nyingi watu wa visasi ni watu wanaopenda umbea, majungu kukomoana na wafitini..Tukifika hapo ndo tunakuta nafasi ya Bashite maana ukiangalia historia ya Bashite amefika hapo halipo kwa njia ya kujikomba kwa watoto wa wakubwa na katika kujikomba huko kuna majungu na uongo ndaniyake. Na hii ndo siri ya Magufuli na Bashite maana anafahamu kuwa akimtosa majungu hayapo.

  Kwa hali hii mawaziri wake wanazidi kuwa wayonge wanakosa ujasiri na wanazidi kujitenga na kumuacha yeye na Makonda wake. Makonda anamfanya hata waziri mkuu hakose ujasiri ukifatilia yule waziri mkuu wa mwanzo aliyejaa ujasiri aliyependa kuona Taifa linasonga mbele si Waziri mkuu huyu anayefikia kufokewa wa Makonda masikini. Mwangalie Mwigulu wa Jk na Mwigulu wa sasa, Mwangalie Makamba wa Jk na Makamba wa sasa wote wamekosa ujasiri maana hawana ukaribu na mkulu.

  Kitu kimoja Mafuguli anapaswa kufahamu huwezi kujenga taifa na kupata mafanikio bila kuwa na timu nzuri, umoja katika timu, ushirikiano katika timu, kujenga uaminifu katika timu, kuwa uhuru wa kutoa mawazo katika timu ndo msingi pekee wa mafanikio, huwezi kupata mafanikio unapojenga matabaka katika timu yako na huwezi kufanikiwa bila kuwa na wazo tofauti.
   
 16. J

  Jakamoko Senior Member

  #55
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 14, 2017
  Messages: 157
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kianyago??? Hahahahaha, alikuwa anatania bila shaka
   
 17. g

  gpastory JF-Expert Member

  #56
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 11, 2016
  Messages: 337
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 60
  Wewe kalia bavicha utakalia kidole
   
 18. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #57
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 10,599
  Likes Received: 5,822
  Trophy Points: 280
  Na kura alijipigia! Pole yao wapiga kura
   
 19. Mlyuha

  Mlyuha JF-Expert Member

  #58
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 27, 2015
  Messages: 238
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  nchi haiwezi kuanguka kwa sababu ya kina bashite. wataanguka wao wataiacha nchi kama walivyoikuta. rejea Gambia na kwingineko mwisho wa siku nchi itabaki kama nchi..
   
 20. d

  dev senior JF-Expert Member

  #59
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 339
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 80
  mwanaharakati Mwanahabari Huru

  huu ni uzi wako wa nne ninaopata kuusoma siku ya leo.... hii ni ishara kuwa siku ya leo ilikuwa ngumu kwako, pole sana....

  hao jamaa hawako kwenye mgomo, wala si hivyo unavyoamini.... hao watu wako kwenye pepo isiyo kifani...

  na raha wanayoipata inatokana na kukingiwa kifua na raisi mwenyewe linapokuja swala la fitina na majungu kazini...

  leo wameshuhudia mwenzao kwa namna anavyojengewa ukuta wa makombora kumzunguka, vivyo hivyo kama ilivyofanyika kwa waziri mkuu majaliwa siku chache zilizopita.... na tena kama JPM alivyofanya kwa muhongo....

  kwa kifupi mawaziri hawako katika kipindi kigumu kama unavyofikiri, tayari wana uhakika wa kazi na hata wakiharibu watatafutiwa sehemu nyingine...
   
 21. abudist

  abudist JF-Expert Member

  #60
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 754
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 180
  Nchi hii sasa inaendeshwa kama movie na ma-starring wawili lakini wote watakwama njiani.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...