Je mawaziri wetu wana mgomo baridi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mawaziri wetu wana mgomo baridi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanahabari Huru, Mar 20, 2017.

 1. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 11,419
  Likes Received: 17,320
  Trophy Points: 280
  Naanza kuitafakari hofu yangu niliyokuwa nayo wiki kadhaa zilizopita, maana nilikuwa nahisi kuwepo Kwa mgomo baridi wa Baraza la Mawaziri, ama kile kinachoitwa 'Mawaziri kususa', ambacho hivi sasa nakiona wazi wazi.

  Ari na kasi waliyokuwa wameanza nayo Mawaziri ilikuwa ni kubwa sana, ilikuwa waziri akiingilia mlango huu, naibu waziri anatokea Kwa huku, yaani ofisi za umma zilichangamka na kila mtumishi wa umma alikuwa anasema "sasa hivi kazi tu, anaweza akaja waziri wakati wowote" yaani Waziri yupo mmoja, nchi ina mikoa zaidi ya 28, kila mtumishi katika kila mkoa alikuwa anadhani waziri anaweza kufika hapo Kwa muda huo huo, Kwa ufupi taifa liliingiwa na hofu kwamba awamu hii ssio ya mchezo, inachunguza na inafahamu kila kitu, wakati wote ukikosea unaonekana na utachukuliwa hatua papo Kwa papo..

  Lakini, katika awamu zote, awamu hii imekuwa ndiyo awamu ya kwanza kuingia madarakani na kuanza kuzodolewa na wananchi ndani ya muda mfupi sana. Ile mihemuko yote imepotea, matumaini yamekufa, ndoto ya mabadiliko imeyeyuka, Kwa ufupi ni kwamba Tanzania mpya iliyozungumzwa imeota mbawa na kupeperukia kusikojulikana.

  Mawaziri wamerudi nyuma, wamegundua kwamba wanafanya kazi ya MTU na sio ya nchi tena. Mawaziri wengi wamejisikia vibaya kudharauliwa nanushauri wao kupuuzwa, ilhali Mawaziri wetu wengi wao ni wasomi wazuri, wanauzoefu Mkubwa wa kiuongozi na hata baadhi yao walijiandaa kuongoza nchi, walichukua fomu za kugombea urais na kampeni za awali walifanya, hivyo watu Hawa wanapojihisi kudharauliwa na kupuuzwa, kwamba waendeshwe wote Kwa akili ya MTU mmoja, imewawia vigumu sana. Ndiyo maana tunasikia kwamba kuna masuala yanaamuliwa na Mawaziri mmoja mmoja bila kupitia kwenye vikao vya baraza la Mawaziri.

  Leo nchi inaendeshwa na watu wawili: yaani Rais wa nchi na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, katika shughuli za maendeleo anayeonekana ni Rais na Mkuu wa mkoa wa DSM, hata katika uzinduzi wa miradi ya maendeleo, ni Rais mwenyewe na mkuu wa mkoa was DSM, hata waziri akiwepo, uwepo wake hautambuliki, Bali wanaoonekana nankusikika vizuri ni Rais na mkuu wa mkoa wa DSM. Hii inawavunja mioyo Mawaziri ambao ndiyo wasimamizi wa Sera katika mawizara yote, na watendahi wao makatibu wakuu.

  Nikirejea aya iliyotangulia, ni kwamba utendaji kazi wa Mawaziri umedhoofika na umeshuka Kwa kiwango kikubwa sana, mshawasha waliokuwa nao kuhusu Tanzania mpya haupo tena, ziara za kushitukiza zimeonekana ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, siasa za ukali na visasi zimetawala, Mawaziri kama chombo cha kumshauri Rais kimegeuka na kuwa chombo cha kuelekezwa na kushauriwa na Rais.

  Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali Kwa mujibu wa katiba, na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, amekuwa akifanya shughuli zake kama kivuli cha Rais, haonekani kutekeleza majukumu yake kama Mawaziri wakuu waliotangulia, Kwa ujumla sasa nchi inaendeshwa Kwa akili moja.

  Watanzania ninawashauri kuwa wavumilivu lakini wenye kuitazama nchi inaelekea wapi na sio serikali inaelekea wapi, watanzania wafahamu kwamba sio hasara serikali ikianguka, Bali ni hasara nchi ikianguka, kwani serikali kuwepo madarakani ni Kwa makusudi ya wananchi wenyewe na wanao uwezo wa kuiweka madarakani serikali yoyote ile madhali wao wameamua, kwani Umma ndiyo wenye mamlaka ya mwisho katika nchi.
   
 2. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  Hawasikiki,

  Si umesikia kwamba siku ya kuchukua fomu alienda peke yake,wao mawaziri hawakuwepo!!!!???
   
 3. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  kama kuna ukweli
   
 4. j

  jembe afrika JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2017
  Joined: Jan 15, 2014
  Messages: 7,108
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  Kuna ukweli hapa
   
 5. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 16,927
  Likes Received: 60,387
  Trophy Points: 280
  Mimi mtu hanipangii njia ya kupita. Hata fomu nilichukua peke yangu.

  Tafakari hiyo kauli, hata ungekuwa wewe ndio waziri ungekaa kimya tu.

  Nape na ile tume yake aliyounda kwenye sakata la Clouds ni sawa na kusubiria basi la kwenda Zanzibar kutokea Dar.
   
 6. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,405
  Trophy Points: 280
  Ukweli upo mkuu, mawaziri ni kama wapo wapo tu, hakuna hats wanalofanya likathaminika.
   
 7. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,929
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Hii nchi anaipeleka sehemu kusikojulikana..

  Lakin kama inaenda hivi wacha tuh iangukilie mbali...potelea mbali akifeli ndiyo bora zaid
   
 8. CHARMILTON

  CHARMILTON JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2017
  Joined: May 30, 2015
  Messages: 6,323
  Likes Received: 8,745
  Trophy Points: 280
  Makamba ndiye mwasisi.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,831
  Trophy Points: 280
  Bavicha bhana hahaha
   
 10. Roger Sterling

  Roger Sterling JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2017
  Joined: May 10, 2015
  Messages: 11,105
  Likes Received: 9,586
  Trophy Points: 280
  Ni wazi serikali hii haifanyi kazi kwa pamoja. Kumbuka Nape alipinga mbinu zilizotumika kwenye vita ya madawa, japo ilikuwa na baraka za bosi wake; ya Mwakyembe, kila mtu anayajua; Leo tena Nape anaonyesha ushirikiano na kuahidi kufanyia kazi drama iliyotokea Clouds, bosi akasema mengine kabisa. Kwa vaishiria hivi, ni waziri asiye na self respect ndiye atakayebaki kushirikiana na bwana yule.
   
 11. mr mkiki

  mr mkiki JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 22, 2016
  Messages: 1,833
  Likes Received: 3,404
  Trophy Points: 280
  Asante
   
 12. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  Nchi inaendeshwa kama lori la maji taka
   
 13. cephalocaudo

  cephalocaudo JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 5,940
  Likes Received: 6,621
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa kiitifaki anaanza
  Sizonje anafuatia Makonda

  Kingne Makonda ana hudumia wizara zote unazozijua
   
 14. jery tarimo

  jery tarimo JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 11, 2016
  Messages: 211
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
   
 15. L

  Leopold Rwegoshora JF-Expert Member

  #15
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 29, 2016
  Messages: 331
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Wacha tuendelee kutopata furaha
   
 16. karugila

  karugila JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 6, 2014
  Messages: 1,170
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  We ukiwa na mihemko kwa utawala huu si unapoteza muda tu
   
 17. Nyundooo

  Nyundooo Member

  #17
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 28, 2017
  Messages: 35
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 25
  Naipenda Sana JF, napata nondo tu hapa.
   
 18. habari ya hapa

  habari ya hapa JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2017
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 10,127
  Likes Received: 5,425
  Trophy Points: 280
  Ha ha haaaa mkuu hiyo kauli imekuumiza sana nakuona kila pahala wairudia rudia, pole sana
   
 19. K

  Kibehe JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 11, 2017
  Messages: 890
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 180
  Wanapata mishahara ya bure. .kz zote kuna anae wafanyia so mmeona bw, nape kaunda tume asubuhi saa 4.majibu tayari. Mwakyela kapiga marufuku ndoa bila cheti akapewa za uso. Sasa yupi tena. Wa chakula kasemewa kipo tatizo nn tena ?
   
 20. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,991
  Likes Received: 3,740
  Trophy Points: 280
  mkuu, wacha waipate fresh bana.
  hawa ndiyo walikuwa wakimpigia debe sana JPM na wengine walikuwa wakiigiza hadi zile push up na kumtwisha matusi mazito sana Lowassa!

  kajisemea Musukuma kinyago wamekipamba sebuleni wenyewe afu kinawapiga mkwara. safi sana!
   
Loading...