Je mawaziri wetu wana mgomo baridi? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mawaziri wetu wana mgomo baridi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanahabari Huru, Mar 20, 2017.

 1. Mwanahabari Huru

  Mwanahabari Huru JF-Expert Member

  #1
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 9, 2015
  Messages: 12,302
  Likes Received: 20,494
  Trophy Points: 280
  Naanza kuitafakari hofu yangu niliyokuwa nayo wiki kadhaa zilizopita, maana nilikuwa nahisi kuwepo Kwa mgomo baridi wa Baraza la Mawaziri, ama kile kinachoitwa 'Mawaziri kususa', ambacho hivi sasa nakiona wazi wazi.

  Ari na kasi waliyokuwa wameanza nayo Mawaziri ilikuwa ni kubwa sana, ilikuwa waziri akiingilia mlango huu, naibu waziri anatokea Kwa huku, yaani ofisi za umma zilichangamka na kila mtumishi wa umma alikuwa anasema "sasa hivi kazi tu, anaweza akaja waziri wakati wowote" yaani Waziri yupo mmoja, nchi ina mikoa zaidi ya 28, kila mtumishi katika kila mkoa alikuwa anadhani waziri anaweza kufika hapo Kwa muda huo huo, Kwa ufupi taifa liliingiwa na hofu kwamba awamu hii ssio ya mchezo, inachunguza na inafahamu kila kitu, wakati wote ukikosea unaonekana na utachukuliwa hatua papo Kwa papo..

  Lakini, katika awamu zote, awamu hii imekuwa ndiyo awamu ya kwanza kuingia madarakani na kuanza kuzodolewa na wananchi ndani ya muda mfupi sana. Ile mihemuko yote imepotea, matumaini yamekufa, ndoto ya mabadiliko imeyeyuka, Kwa ufupi ni kwamba Tanzania mpya iliyozungumzwa imeota mbawa na kupeperukia kusikojulikana.

  Mawaziri wamerudi nyuma, wamegundua kwamba wanafanya kazi ya MTU na sio ya nchi tena. Mawaziri wengi wamejisikia vibaya kudharauliwa nanushauri wao kupuuzwa, ilhali Mawaziri wetu wengi wao ni wasomi wazuri, wanauzoefu Mkubwa wa kiuongozi na hata baadhi yao walijiandaa kuongoza nchi, walichukua fomu za kugombea urais na kampeni za awali walifanya, hivyo watu Hawa wanapojihisi kudharauliwa na kupuuzwa, kwamba waendeshwe wote Kwa akili ya MTU mmoja, imewawia vigumu sana. Ndiyo maana tunasikia kwamba kuna masuala yanaamuliwa na Mawaziri mmoja mmoja bila kupitia kwenye vikao vya baraza la Mawaziri.

  Leo nchi inaendeshwa na watu wawili: yaani Rais wa nchi na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, katika shughuli za maendeleo anayeonekana ni Rais na Mkuu wa mkoa wa DSM, hata katika uzinduzi wa miradi ya maendeleo, ni Rais mwenyewe na mkuu wa mkoa was DSM, hata waziri akiwepo, uwepo wake hautambuliki, Bali wanaoonekana nankusikika vizuri ni Rais na mkuu wa mkoa wa DSM. Hii inawavunja mioyo Mawaziri ambao ndiyo wasimamizi wa Sera katika mawizara yote, na watendahi wao makatibu wakuu.

  Nikirejea aya iliyotangulia, ni kwamba utendaji kazi wa Mawaziri umedhoofika na umeshuka Kwa kiwango kikubwa sana, mshawasha waliokuwa nao kuhusu Tanzania mpya haupo tena, ziara za kushitukiza zimeonekana ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu, siasa za ukali na visasi zimetawala, Mawaziri kama chombo cha kumshauri Rais kimegeuka na kuwa chombo cha kuelekezwa na kushauriwa na Rais.

  Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali Kwa mujibu wa katiba, na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, amekuwa akifanya shughuli zake kama kivuli cha Rais, haonekani kutekeleza majukumu yake kama Mawaziri wakuu waliotangulia, Kwa ujumla sasa nchi inaendeshwa Kwa akili moja.

  Watanzania ninawashauri kuwa wavumilivu lakini wenye kuitazama nchi inaelekea wapi na sio serikali inaelekea wapi, watanzania wafahamu kwamba sio hasara serikali ikianguka, Bali ni hasara nchi ikianguka, kwani serikali kuwepo madarakani ni Kwa makusudi ya wananchi wenyewe na wanao uwezo wa kuiweka madarakani serikali yoyote ile madhali wao wameamua, kwani Umma ndiyo wenye mamlaka ya mwisho katika nchi.
   
 2. leodigardcyrilo

  leodigardcyrilo JF-Expert Member

  #21
  Mar 20, 2017
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 1,736
  Likes Received: 772
  Trophy Points: 280
  Sasa hapa ndo uone kichwa kinavyo jieleza uelewa wa mtu kupitia matamshi
   
 3. Obuma

  Obuma JF-Expert Member

  #22
  Mar 20, 2017
  Joined: Dec 28, 2015
  Messages: 2,685
  Likes Received: 4,988
  Trophy Points: 280
  Huwezi Kufanya kazi na Mtu asiefuata taratibu ukawa na fulani ya kufanya kazi!!! Kama ukiendelea kuona Waziri anatoa matamko holela huyo bado hajajitambu labda akamuulize Mwakyembe na Nape yaliyowakuta!!!!
   
 4. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #23
  Mar 20, 2017
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,453
  Likes Received: 14,128
  Trophy Points: 280
  Ndio maana alikaa muda mreeeefu bila kuteua mawaziri,hata alipowateua,alikaa muda mreeeeeefu bila kuwapa instrument

  Siku ya kuchukua fomu hawakuwepo,alienda peke yake
   
 5. mwanamichakato

  mwanamichakato JF-Expert Member

  #24
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 20, 2015
  Messages: 700
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 80
  "In a democracy, every citizen has certain basic rights that the state cannot take away from them. These rights are internationally recognized and guaranteed. Everyone has the right to have their own beliefs, including their religious beliefs, and to say and write what they think. Everyone has the right to seek different sources of information and ideas. Everyone has the right to associate with other people, and to form and join organizations of their own choice, including trade unions. Everyone has the right to assemble and to protest government actions. However, citizens have an obligation to exercise these rights peacefully, with respect for the law and for the rights of others."
   
 6. Bata Mzee

  Bata Mzee Member

  #25
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 20, 2016
  Messages: 22
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 5
  nipo getto nakula mziki tu.. oooooh dayana eeeh.. sister dayana... mmmmh alima.. sisy alimaeeee...!!!
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #26
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,388
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  Bashite ana nguvu zaidi ya PM....shangaa pia ana nguvu zaidi ya Mama wa Kwanza!!! Kijana wa kwanza amzidi Mama wa Kwanza!!!
   
 8. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #27
  Mar 20, 2017
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,559
  Likes Received: 886
  Trophy Points: 280
  Huu ndo mtindo mya wa kuleta maendeleo kwa haraka.
   
 9. U

  UPINZANI NOMA JF-Expert Member

  #28
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 24, 2015
  Messages: 457
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 60
  Kuna maneno niliambiwa na wazee wangu ambao pia walisimuliwa na mababu zao,mnifuate jukwaa la historia msome penye kichwa MJEE WA MAJITA(MUSOMA). Nitaendelea na utawala ulio tabiliwa hapa nchini,yote niliyosimuliwa mengi yalishatkea na bado ninaona tunakoelekea mengine yatatokea
   
 10. ngalakeri

  ngalakeri JF-Expert Member

  #29
  Mar 20, 2017
  Joined: Jul 17, 2014
  Messages: 883
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nafuatilia jinsi mawaziri wanavyoongea kwa unyenyekevu kwa Rais hata leo pia imejidhihirisha. Ongea ya Makonda sio ethical, huwezi kuongea na Rais kisanii tena unamwambia Rais ambaye pia ni Amir jeshi mkuu usiogope, dah! Jamani hata kama ni mwanangu mpendwa nipendezwaye nae haipaswi kuwa hivyo, nahisi hata mawaziri wanajiona inferior kwa makonda .
   
 11. L

  Livejr JF-Expert Member

  #30
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 1,004
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kwani Nape sio Waziri..?
  Si ameunda kamati ya watu watano ..?
  Wakitoa matamko ya msioe mpaka muwe na vyeti vya ndoa mnasema anakurupuka wakikaa kimya wamesusa. Daah
   
 12. L

  Livejr JF-Expert Member

  #31
  Mar 20, 2017
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 1,004
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Ulitaka amuambie "Aogope"..?
   
 13. N

  Negongo Senior Member

  #32
  Mar 20, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Waziri nape achana na hiyo tume yako, ni kupoteza muda tu, kwanza najua haitapata ushirikiano wa kutosha, pili najua itakuja na majibu yanayoeleweka kuwa hakuna kosa lolote alilo lifanya, na huo ndio utakuwa mwisho wa mambo yote, kwa hiyo unachofanya ni usanii tu.
   
 14. successor

  successor JF-Expert Member

  #33
  Mar 20, 2017
  Joined: Oct 25, 2012
  Messages: 1,860
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya zaidi hiyo akili moja na yenyewe haina akili. Kazi tunayo Watanzania, tuendako sio kuzuri.
   
 15. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #34
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 2,166
  Likes Received: 2,669
  Trophy Points: 280
  Mimi naona ilipofikia Magufuli ampe Makonda u-Waziri Mkuu tujue moja!
  Kama mtakumbuka sekeseke la SHISHA nilimsikia Makonda akimtuhumu PM Majaliwa kuwa karuhusu Shisha na alikuwa ana shirikiana nao na pengine alishapata mgawo wa milioni 5!
  Kitendo hicho cha kumtuhumu PM mbele ya media kwa kujiamini kiasi hicho ni dalili kwamba ana. BARAKA zote za JPM!!!
   
 16. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #35
  Mar 20, 2017
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,713
  Likes Received: 3,513
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 17. NIYOMBARE

  NIYOMBARE JF-Expert Member

  #36
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 26, 2016
  Messages: 3,382
  Likes Received: 3,771
  Trophy Points: 280
  Mi nauliza ishafika namba ngapi mpaka sasa?
   
 18. swamy

  swamy Senior Member

  #37
  Mar 20, 2017
  Joined: Aug 25, 2012
  Messages: 185
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Politics
   
 19. sheiza

  sheiza JF-Expert Member

  #38
  Mar 20, 2017
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,159
  Likes Received: 2,034
  Trophy Points: 280
  Masuala muhimu yanashughuliwa..kwa magufuli ni bora kuacha kuliko kugoma..maana daily anahitaji ripoti na anafuatilia..unaanzaje mgomo baridi hapo
   
 20. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #39
  Mar 20, 2017
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,213
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  Wewe ni sawa na fisi anayesubiri mkono wa msafiri udondoke tahamaki msafiri kafika kwake na mkono haujadondoka .
   
 21. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #40
  Mar 20, 2017
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 8,213
  Likes Received: 1,806
  Trophy Points: 280
  Achana na huyu kinyonga
   
Loading...