Je, mavazi mafupi yanachochea uzinzi?

yuzazifu

JF-Expert Member
Oct 6, 2018
5,109
9,407
Natumai hamjambo wanabodi.

Wakuu kuna hii dhana imejengeka katika jamii kuwa wanawake wanaovaa nguo fupi ni malaya na huyatumia mavazi hayo kama kivutio na mtego kwa wanaume.

Binafsi nadhani hii dhana ni potofu sababu ukiangalia hata asilia yetu kabla ya mavazi haya mzungu wanawake walifunika uchi ila mambo haya ya uzinzi hayakuwepo.

Nadhani uzinzi unatokana na hulka ya mtu na wala hauhusiani na mavazi kabisa, ninao marafiki wa kike wanaovaa mavazi mafupi wanajiheshimu sana na huniambia wanavaa vile coz ndio hobi yao ya uvaaji.

Je, ni upi mtizamo wako katika jambo hili?
 
Ngoja nisome kwanza...

Binafsi naona kuna kaukweli fulani katika hili.

Kuvaa nguo fupi kunahamasisha akili kuhama kuhamia sehemu nyingine.

Kuhusu wanawake uliowauliza wao wanaweza kweli kuvaa kwa hobi zao,lakini hawa wanaowaona ndo watawaza hivyo.
 
Sasa na wavulana kuvaa singred na kutembea mtaani tunachochea uzinzi
Mi nahisi tu upendeleo wa mtu katika kuchagua mavazi wakati mwingine kutokana na hali ya hewa.!

Mwanaume unaweza vaa vest utembee mtaani uonekane shujaa Ila ngoja Mtoto wa kike avae nguo fupi utaskia she's a bitch
 
Sasa na wavulana kuvaa singred na kutembea mtaani tunachochea uzinzi
Mi nahisi tu upendeleo wa mtu katika kuchagua mavazi wakati mwingine kutokana na hali ya hewa.!

Mwanaume unaweza vaa vest utembee mtaani uonekane shujaa Ila ngoja Mtoto wa kike avae nguo fupi utaskia she's a bitch
right, nadhani hii mitizamo mingine tunapaswa tuipuuze
 
Ila kwa 90% ya wanawake wanaovaa nguo fupi ni malaya. Wanavaa kwaajili ya kumvuta mwanaume.
mkuu unatania, 3/4 ya wanake mijini wanavaa nguo fupi je wote hao wanajiuza? 95% ya wanafunzi vyuoni wanafaa nguo fupi wote wanajiuza? 3/4 ya watumishi wakike wanavaa nguo fupi je wote hao wanajiuza?

jaribu kutofautisha kati ya hobi na hulka, mavazi ni hobi bt umalaya ni hulka ya mtu na haijalishi anavaa nguo ndefu/fupi.
 
Labda na ladies wakuje hapa hoja hii ipate mashiko

Kuna wasichana wanaaga nguo fupi Ila unakuta kila anayemtongoza anamkataa na unakuta yupo single
 
Back
Top Bottom