Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,601
Ingekuwa vyema sana uwapinge kwa vitendo. Si maneno tu.Mkuu umeandika point, hakuna average mind zitakazokuelewa ulichokiandika, lakini kwa watu wanaofuatilia mambo kwa undani Marekani its allies hawa watu ni watu wa kupingwa kwa nguvu zote, kwasababu hawana nia njema hata kidogo na binadamu.
Acha kutumia internet waliyoianzisha kwa sababu wana i control.
Anzisheni yenu.
Hii Jamiiforums yenyewe ni tovuti iliyosajiliwa Marekani.
Kama hutaki vya Wamarekani hata hapa Jamiiforums hutakiwi kuwepo.
Ukitembelea Jamiiforums habari zako zinakwenda kwa Wamarekani. Kama huwataki Wamarekani jiondoe hapa.
Acha kutumia Whatsapp nao ni mfumo wao. Facebook, Instagram nazo pia.
In fact hata email usitumie.
Usiangalie movies za Hollywood wala kusikiliza muziki wa Kimarekani.
Jiondoeni Umoja wa Mataifa unaochangiwa sana na Wamarekani na ambao Makao Makuu yake yako Marekani.
Nduguzenu wanaotaka kuja kuishi na kusoma Marekani wakatazeni.
Misaada ya Wamarekani kataeni.
Watalii wa kutoka Marekani msiwakubali.
Jiondoeni kwenye mfumo wa kibenki wa dunia unaotawaliwa na Marekani.
Kataeni kununua bidhaa zozote za Kimarekani.
Mkifanya hivyo na kusema Mmarekani mbaya, nitawaelewa.
Siyo mtu umevaa Nike na Polo, unaandika kwenye internet JF, unapost picha instagram, unawasiliana na ndugu zako Facebook, una chat groups za Whatsapp, serikali yako imepewa misaada na Marekani, halafu kelele nyiingi Wamarekani wabaya.
Kataeni Umarekani kwa vitendo.
Kabla hamjafanya hivyo mtakuwa mnacheza tu mchezo wa "Baniani mbaya, kiatu chake dawa".
Unafiki.