Je, kuzaa ni hitaji la msingi katika ndoa?

Je, kuzaa ni hitaji la msingi katika ndoa?

Nafikiri kuzaa ni hitaji Ila unabidi kuzaa watoto ambao unao-wamudu na kimkakati .

Maana dunia ya sasa IPO simplified I term of technology , hivyo inahitaji watu wachache Ila ambao wapo well occupied and visionary.

Ikiwa utaangalia Sana waweza kuzaa mtoto aje aendeleze kile ulichonacho na siyo mtoto aje awe ur game changer.

Kwakuwa I have some experience MTU mmoja alizaa 17 kids Ila hakuwapa Elimu wala skills zozote at the end wototo wote 17 wamekuwa broke financially na unproductive.

Kuhusu hofu ya kusaidiwa uzeeni kikubwa ni kufocus ukiingia uzee uwe na affordability ya kupata BIMA na msaidizi ambaye atakuwa in ur payroll all over the living days.
Kwa mazingira haya, mtoto ni 'asset' au 'liability'?
 
Wewe unaliona hilo likiwezekana?

Kwamba wakati wanafanya tendo manii ziende kwenye fahamu za mama yako na baba yako kuwaambia “mimi sitaki kwenda huko dunian”,unaona ikiwezekana hii?
Je, inawezekana ata kuzaliwa kwetu ilitokea tu bila kupangiliwa?
 
Sio tu la msingi, ni hitaji hadi la ukita na paa. Unaingia kwenye ndoa iweje sasa? Kuzaa ndo matokeo tarajiwa na. 1
Ikitokea wanandoa wakakosa uwezo wa kuzaa, je hiyo ndoa ivunjike?
 
Wazazi wasingeleta watu duniani hata dunia isingekuwepo.
Aliyekwambia dunia inahitaji watu ni nani?

Dunia haihitaji binadamu ili iwepo.

Ikatokea Binadamu wote tutoweke sasa hivi, Dunia itaendelea kuwepo na itanawiri sana.

Kwa sababu muharibifu mkuu wa mazingira "Binadamu" hatokuwepo.
 
Kuzaa katika ndoa ni kama maua kwenye bustani si lazima uyapande ili bustani iwepo, lakini yakiwepo huifanya bustani ipendeze zaidi. Hivyo kupata watoto ni jambo la heshima na baraka, lakini si sharti kwa ndoa/wanandoa.
Je ni sahihi kutengeneza tegemezi?
 
KUZAA NI KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME BURE TUU!HAKUNA UMUHIMU WA KUZAAZAA,tena kwenye ndoa hakuna umuhimu kabisa ya kuwa na watoto kwani watoto watawazuia wewe na mkeo kula bata😎
Unahisi hii inaweza kuwa sababu ya msingi kwa wengine kuzaa mtoto mmoja au kutozaa kabisa?
 
Kwa hiyo, kizazi cha leo kinaweza kuamua kuhitimisha mwisho wa dunia kama hawatozaa?
Hakuna mwisho wa Dunia.

Kuna mwisho wa viumbe.

Hata ikatokea viumbe wote watoweke sasa hivi, Dunia itabaki yenyewe ikiwa na ardhi, mawe, milima, mabonde, maji, anga n.k

Viumbe ndio vinahitaji Dunia.

Dunia haihitaji viumbe.
 
Hapo uliposema '' wanakuwa na mji wao '' ni jambo la kufikirisha sana ,tena ni ujinga nkubwa...Leo mtoto wake akishakuwa basi anakuwa na mwenza wake ,wanakuwa karibu kuliko wewe ,kikubwa familia yake imekula sio wewe mzee..

Kimahesabu , mtoto mpaka amalize chuo ni miaka 22 na kuendelea ,sasa wewe miaka 20 unapambania mtoto ambaye hajaanza kijitegemea hapo lazima sura yako ipate makunyazi ..Mpaka akishaanza kujitegemea wewe ushapotea kabisa ,umeshakuwa mzee hauna tena bata unasubiria kufa tu.
Hoja yako ina mashiko, kwa hiyo kuliko kuzaa na kuingia gharama, unashauri ni bora mtu ajiwekeze yeye mwenyewe kwa miaka ya baadaye?
 
Ngoja waje kukupa muongozo...

Nadhani hata lile tendo pia siyo hitaji muhimu sababu tumepewa mikono na akili...

Cc: Mahondaw
 
Back
Top Bottom