Je, kuzaa ni hitaji la msingi katika ndoa?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,104
Reaction score
55,514
Wengi tunakimbilia kuzaa tukiamini huko mbeleni, watoto tunaowazaa watakuja kutusaidia.

Hii inatokana na kutokuwepo kwa kambi za wazee katika huu ukanda wetu, inayopelekea ufikapo uzeeni kukosa mtu wa kukusaidia pale utakapohitaji msaada.

Tumekuwa tukiwazaa watoto, na kuwagharamia kila kitu kwa gharama kubwa, iwe chakula, mavazi, elimu n.k.

Ila wakishakuwa wakubwa, wanakuwa na miji yao na wengine wanakuwa hawana msaada kwa wazazi wao, na kuishia kuwatelekeza.

Sasa najiuliza, kuna umuhimu gani wa kuzaa na kujinyima vitu mbalimbali ikiwapo uwekezaji mbalimbali, kwa ajili ya kumgharamikia mtoto asiyekuja kuwa na msaada na wazazi?

Imekuwa, kuwa na watoto katika familia ni mzigo mkubwa sana inayoathiri uchumi wa wana familia.

Hii imeathiri maisha yetu ya kila siku, ndio maana wengi wetu hatuendi kutalii mbuga za wanyama au kwenda nchi mbali mbali, kwa sababu ya fedha kuwekeza kwa watoto.

Sasa najiuliza, kuwa na watoto kwenye ndoa ni hitaji la msingi?​
 
Unaandika kama mtu aliyekatwa kichwa, wewe usingezaliwa kwenye hiyo ndoa ya baba yako na mama yako ungekuja hapa kuhoji kama kuna ulazima wa kuzaa watoto?
 
Mfano, wewe uliomba wakulete duniani?
 
Wengi tunakimbilia kuzaa tukiamini huko mbeleni, watoto tunaowazaa watakuja kutusaidia.

Hii inatokana na kutokuwepo kwa kambi za wazee katika huu ukanda wetu, inayopelekea ufikapo uzeeni kukosa mtu wa kukusaidia pale utakapohitaji msaada.

Tumekuwa tukiwazaa watoto, na kuwagharamia kila kitu kwa gharama kubwa, iwe chakula, mavazi, elimu n.k.

Ila wakishakuwa wakubwa, wanakuwa na miji yao na wengine wanakuwa hawana msaada kwa wazazi wao, na kuishia kuwatelekeza.

Sasa najiuliza, kuna umuhimu gani wa kuzaa na kujinyima vitu mbalimbali ikiwapo uwekezaji mbalimbali, kwa ajili ya kumgharamikia mtoto asiyekuja kuwa na msaada na wazazi?

Imekuwa, kuwa na watoto katika familia ni mzigo mkubwa sana inayoathiri uchumi wa wana familia.

Hii imeathiri maisha yetu ya kila siku, ndio maana wengi wetu hatuendi kutalii mbuga za wanyama au kwenda nchi mbali mbali, kwa sababu ya fedha kuwekeza kwa watoto.

Sasa najiuliza, kuwa na watoto kwenye ndoa ni hitaji la msingi?​
Ndiyo mkuu.

Lengo la Kuzaa siyo watoto waje kukusaidia, Bali ni kutimiza malengo ya kuijaza Dunia na kuweka Mhuri kwamba tumewahi kuwepo duniani.. Maana wote tukiwaza kutokuzaa, basi miaka mia moja tu Ijayo Dunia itabaki bila watu..

Nchi za Magharibi ambapo Wananchi wake waliamua kutokuzaa ama kuzaa Mtoto mmoja tu, Kwa Sasa Serikali zao zinahaha kuhamasisha watu wazae.. Wamejawa na hofu ya Vizazi vyao kutoweka.

Kuzaa ni Baraka, kuzaa ni heshima, kuzaa ni kuweka Hazina..
 
Nafikiri kuzaa ni hitaji Ila unabidi kuzaa watoto ambao unao-wamudu na kimkakati .

Maana dunia ya sasa IPO simplified I term of technology , hivyo inahitaji watu wachache Ila ambao wapo well occupied and visionary.

Ikiwa utaangalia Sana waweza kuzaa mtoto aje aendeleze kile ulichonacho na siyo mtoto aje awe ur game changer.

Kwakuwa I have some experience MTU mmoja alizaa 17 kids Ila hakuwapa Elimu wala skills zozote at the end wototo wote 17 wamekuwa broke financially na unproductive.

Kuhusu hofu ya kusaidiwa uzeeni kikubwa ni kufocus ukiingia uzee uwe na affordability ya kupata BIMA na msaidizi ambaye atakuwa in ur payroll all over the living days.
 
Mleta mada in really life!!!
IMG_20250531_171223.jpg

Huwa inasikitisha zaidi pale unapojua pia yupo binti wa mtu anamvulia nguo anamzini.
 
Mfano, wewe uliomba wakulete duniani?
Wewe unaliona hilo likiwezekana?

Kwamba wakati wanafanya tendo manii ziende kwenye fahamu za mama yako na baba yako kuwaambia “mimi sitaki kwenda huko dunian”,unaona ikiwezekana hii?
 
Sio tu la msingi, ni hitaji hadi la ukita na paa. Unaingia kwenye ndoa iweje sasa? Kuzaa ndo matokeo tarajiwa na. 1
 
Kuzaa katika ndoa ni kama maua kwenye bustani si lazima uyapande ili bustani iwepo, lakini yakiwepo huifanya bustani ipendeze zaidi. Hivyo kupata watoto ni jambo la heshima na baraka, lakini si sharti kwa ndoa/wanandoa.
 
KUZAA NI KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME BURE TUU!HAKUNA UMUHIMU WA KUZAAZAA,tena kwenye ndoa hakuna umuhimu kabisa ya kuwa na watoto kwani watoto watawazuia wewe na mkeo kula bata😎
 
Hapo uliposema '' wanakuwa na mji wao '' ni jambo la kufikirisha sana ,tena ni ujinga nkubwa...Leo mtoto wake akishakuwa basi anakuwa na mwenza wake ,wanakuwa karibu kuliko wewe ,kikubwa familia yake imekula sio wewe mzee..

Kimahesabu , mtoto mpaka amalize chuo ni miaka 22 na kuendelea ,sasa wewe miaka 20 unapambania mtoto ambaye hajaanza kijitegemea hapo lazima sura yako ipate makunyazi ..Mpaka akishaanza kujitegemea wewe ushapotea kabisa ,umeshakuwa mzee hauna tena bata unasubiria kufa tu.
 
Ndiyo mkuu.

Lengo la Kuzaa siyo watoto waje kukusaidia, Bali ni kutimiza malengo ya kuijaza Dunia na kuweka Mhuri kwamba tumewahi kuwepo duniani.. Maana wote tukiwaza kutokuzaa, basi miaka mia moja tu Ijayo Dunia itabaki bila watu..

Nchi za Magharibi ambapo Wananchi wake waliamua kutokuzaa ama kuzaa Mtoto mmoja tu, Kwa Sasa Serikali zao zinahaha kuhamasisha watu wazae.. Wamejawa na hofu ya Vizazi vyao kutoweka.

Kuzaa ni Baraka, kuzaa ni heshima, kuzaa ni kuweka Hazina..
Na ikitokea wanandoa wakawa hawana uwezo wa kupata watoto, je hiyo ndoa ivunjike?
 
Wengi tunakimbilia kuzaa tukiamini huko mbeleni, watoto tunaowazaa watakuja kutusaidia.

Hii inatokana na kutokuwepo kwa kambi za wazee katika huu ukanda wetu, inayopelekea ufikapo uzeeni kukosa mtu wa kukusaidia pale utakapohitaji msaada.

Tumekuwa tukiwazaa watoto, na kuwagharamia kila kitu kwa gharama kubwa, iwe chakula, mavazi, elimu n.k.

Ila wakishakuwa wakubwa, wanakuwa na miji yao na wengine wanakuwa hawana msaada kwa wazazi wao, na kuishia kuwatelekeza.

Sasa najiuliza, kuna umuhimu gani wa kuzaa na kujinyima vitu mbalimbali ikiwapo uwekezaji mbalimbali, kwa ajili ya kumgharamikia mtoto asiyekuja kuwa na msaada na wazazi?

Imekuwa, kuwa na watoto katika familia ni mzigo mkubwa sana inayoathiri uchumi wa wana familia.

Hii imeathiri maisha yetu ya kila siku, ndio maana wengi wetu hatuendi kutalii mbuga za wanyama au kwenda nchi mbali mbali, kwa sababu ya fedha kuwekeza kwa watoto.

Sasa najiuliza, kuwa na watoto kwenye ndoa ni hitaji la msingi?​
Kuzaa mtoto kwa kuweka matumaini atakuja kukusaidia baadaye ni ujinga, ni kuzaa kwa biashara ya kutunzana.
 
Back
Top Bottom