JE kuwasuka nywele watoto ni sahihi?

JE kuwasuka nywele watoto ni sahihi?

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,130
Watoto wadogo wanasukwa,ama kwa nywele zao ama kwa rasta,ikumbukwe watoto wanakuwa bado hawajakomaa na mwili kila sehemu unahitaji kuwa relaxed kuruhusu ukuaji,inaaminika kuwa watoto wanaposukwa wakiwa hawajakomaa uso wao ma kichwa vinakomaa.
UKWELI USIO NA UBISHI.
1.zile nywele zinawauma kama ambavyo tunawasikia wakubwa wakilalama zinawauma ama wakati wa kusuka ama baada ya kusuka
2.zile nywele zinawawasha pia kama wanavyolalama wakubwa.
kwa maoni yangu watoto wachaneni tu nywele na si kuwasuka.
 
Watoto wanaosukwa nywele huwa wanakuwa na uso mgumu sana, yaani wanaonekana wamezeeka kiasi kwamba ukimkuta ana miaka 16 kama yule wa prof Kapuya kwa kuwa alisuka mapema unaweza ukafikiri ana miaka 70
 
Watoto kusukwa nywele ni sahihi...sema inategemea unawaongelea wa umri gani.
 
Kusuka kawaida tu mbona si tatizo..kama mtoto anaweza kuhimili kuketi asukwe then i dnt see any problem with it!
 
Watoto wanaosukwa nywele huwa wanakuwa na uso mgumu sana, yaani wanaonekana wamezeeka kiasi kwamba ukimkuta ana miaka 16 kama yule wa prof Kapuya kwa kuwa alisuka mapema unaweza ukafikiri ana miaka 70
Unaongelea aina gani ya msuko? Maana misuko iko mingi sana...hebu funguka ueleweke
 
Kusuka kawaida tu mbona si tatizo..kama mtoto anaweza kuhimili kuketi asukwe then i dnt see any problem with it!
Good...tatizo mleta mada anasema watoto wanasukwa kwa rasta ila ajasema ni watoto wa kuanzia umri gani hawaruhusiwi
kusuka na ni mtindo gani ambao hawaruhusiwi kusuka
 
Wadogo kabisa, miaka mitatu na kuendelea mpaka 15.
Mhhh ni kawaida kusukwa wangu namsuka and she looks so cute...na wakati mwengine ananiomba nimsuke rasta coz anatamani nywele ndefu arusheshe 🙂 sasa unashauri nywele ziwekweje?zikatwe?
 
Watoto wanapaswa kuchanwa nywele au kuzikata, kusuka mtoto licha ya kumuumiza husababisha iq yake kushuka
 
Kusuka kawaida tu mbona si tatizo..kama mtoto anaweza kuhimili kuketi asukwe then i dnt see any problem with it!

Hii hoja haijali hata haki za mtoto,je kama hawezi kusema anaumia?Wewe huwezi kutumia akili ya kikubwa kuwa kusuka kunaumiza?Ina mana wewe mtoto unaweza kumpa sahani ya wali,akamaliza,ukamwongeza nyingine ale eti hajasema ameshiba na anaendelea kula.
Lazima utumie ukomavu wako kureason na si kutumia hisia za mtoto ambaye hajitambui.
 
Wadogo kabisa, miaka mitatu na kuendelea mpaka 15.
Ukiniambia kuanzia miaka 3 hadi 6 hapo naweza kubaliana na wewe...lakini kuanzia miaka 7 wanasuka tu.
Sema inategemea anasukwa na nani na ni msuko upi.
 
Hii hoja haijali hata haki za mtoto,je kama hawezi kusema anaumia?Wewe huwezi kutumia akili ya kikubwa kuwa kusuka kunaumiza?Ina mana wewe mtoto unaweza kumpa sahani ya wali,akamaliza,ukamwongeza nyingine ale eti hajasema ameshiba na anaendelea kula.
Lazima utumie ukomavu wako kureason na si kutumia hisia za mtoto ambaye hajitambui.
Si kweli kabisa!!nani alokwambia kusuka kunaumiza!na umesikia wapi mtoto hajui kureason!!mtoto wa miaka 3 anaongea maneno yote akayamaliza!na anajua akishiba na kama hapendi kitu hizo hypothesis zako unazitolea wapi?mbona hazina ukweli wowote!
 
Unayoyaongea ni sahihi...lakini tambua au fahamu mtoto kuanzia miaka 7 anajitambua na anaweza kusema sitaki kusuka au msusi ananivuta sana nywele na ninaumia. Ila huyo wa miaka 3 unayemsema ni kweli anaweza kugeuzwa kama mdoli na akakaa kimya tu au hata akalia.
 
Mhhh ni kawaida kusukwa wangu namsuka and she looks so cute...na wakati mwengine ananiomba nimsuke rasta coz anatamani nywele ndefu arusheshe 🙂 sasa unashauri nywele ziwekweje?zikatwe?

Mtoto anaweza kumkimbilia nyoka acheze nae japo nyoka huwa hawadhuru watoto ama kulikimbilia gari,je utamwacha kwa kuwa anaonekana anapenda?Lazima utumie akili yako na si ya mtoto asiyekomaa na hana uwezo wa kusema ndiyo ama hapana ama kutambua athari tunazozijidili hapa.
 
Mhhh ni kawaida kusukwa wangu namsuka and she looks so cute...na wakati mwengine ananiomba nimsuke rasta coz anatamani nywele ndefu arusheshe 🙂 sasa unashauri nywele ziwekweje?zikatwe?

Hahahahaha mkwe wangu usimsuke rasta lol....anapendeza tu vile simple na mwenyewe alivo so cute.....mwanangu atafaidi lol
 
We unataka tuwakate wtt wakike nywele zao?

Wengine wtt wa miaka mitatu nywele mpk mabegani, tutazichana vp?

Ukisuka kwa kuwabana sifkiri kama zina neno.

Labda hao wanobandika zile za rasta wakawasuka kama watu wazima.
 
Si kweli kabisa!!nani alokwambia kusuka kunaumiza!na umesikia wapi mtoto hajui kureason!!mtoto wa miaka 3 anaongea maneno yote akayamaliza!na anajua akishiba na kama hapendi kitu hizo hypothesis zako unazitolea wapi?mbona hazina ukweli wowote!
Ni kweli usemacho lakini si watoto wote wenye umri wa miaka 3 wanaweza kujielezea au kusema hiki ni sawa na hiki si sawa ila baadhi ya watoto hasa hasa hawa wa familia bora + international school hao wanajitambua kidogo kama si sana.
Lakini hawa wakwetu wa uswahilini ni wawili kwa kumi
 
We unataka tuwakate wtt wakike nywele zao?

Wengine wtt wa miaka mitatu nywele mpk mabegani, tutazichana vp?

Ukisuka kwa kuwabana sifkiri kama zina neno.

Labda hao wanobandika zile za rasta wakawasuka kama watu wazima.
Mtoto kuanzia miaka 3 hadi 12 siyo vizuri kuwasuka kwa rasta...bali wanasukwa kwa uzi black au brown.
 
Back
Top Bottom