Nimebarikiwa na testimonyPole sana ndugu. Heri yako wewe inakutokea ndotoni tu. Kuna mtu wangu wa karibu sana aliwahi kutokewa na tatizo kama lako lakini tofauti yake ni kwamba yeye mzazi wake aliyekuwa amefariki miezi kadhaa nyuma alikuwa akimtokea live kabisa (kwa maelezo yake) akiwa barabarani, darasani n.k. na kumwita, kuongea nae, kumnyooshea mkono kisha kutoweka ghafla. Hiyo hali iliendelea kumtokea kama mara nane hivi ndani ya miezi mitatu. Bahati nzuri kuna mzee mmoja hivi mchungaji (kwa sasa ni marehemu) ndiye siku moja alikwenda nyumbani alipokuwa akiishi huyo ndugu yangu na kumwombea "kirafiki kabisa" kwa mwenyezi Mungu na tangu siku hiyo hilo tatizo halikumrudia tena na leo hii ni zaidi ya miaka kumi. Mchungaji alisema hayo ni mashetani yaliyokuwa yakija yakiwa katika sura ya marehemu na kumtesa huyo ndugu yetu. Kwa hiyo nionavyo kama wewe ni mkristo au muislam tafuta kiongozi wako wa dini akuombee tu jambo hilo. Binafsi ni moja ya mambo ambayo yalinishangaza sana na ndiyo maana nionapo watu wanabisha au wanakuwa na mashaka juu ya uwepo wa Mungu pamoja na madhambi yangu yote uwa napata woga sana. Natumaini mwenyezi Mungu ataibariki hii testimony yangu kwa wasomaji wote maana sijawahi kupata mahali pengine pa kuitolea au ujasiri wa kuiweka wazi kwa watu wengine.