harder king
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 3,970
- 6,898
Habari za weekend wana JF
Poleni na majukumu ya wiki na karibuni kwenye harakati za weekend za kutumia sehemu ya kile ulichopata kwa hizi siku5
Nije kwenye mada.
My story; hii sio simulizi bali ni kitu kinachoniandama karibu kila siku.
Ipo hivi zaidi ya miaka mitatu iliyopita nilimpotenza babu na bibi ambao ndio waliokua walezi wetu baada ya anguko la familia yetu ya(baba na mama) kutengana na kutuacha kwa wazazi wa baba ambao walitulea kwa kwa maadili mema kabisa..
Ila wazazi wetu halisi walikuja rudiana kabla wazee wao(babu na bibi) yetu kuondoka duniani, baada ya sisi kufikia umri wa kujitegemea na kuwapigania mpaka wakarudiana.
Miezi mitatu iliopita nilimpotenza tena baba yangu kipenzi.
Tatizo ni kwamba tangu baba atutoke nimekua nikionana nae ndotoni tena sasa sio yeye tu mpaka babu na bibi..tena kwenye maisha ya kawaida kabisa tuliyowai kuishi nao pale kijijini,hizi ndoto zimeniandama hadi nashindwa kuelewa kama ni tatizo au ni hali ya kawaida?
Kingine ni kwamba siku nikilala nikiwa nimekunywa mbili tatu hili tatizo la kuota sikutani nalo kabisa labda mara chache sana linijie alfajir.
Sasa kingine kilichonisukuma kuja kuwauliza humu ni baada ya jana kwenda nyumbani nikiwa sijagusa maji kabisa..
Nilikaa nikichek movie mpaka saa7 usiku ndio nikaenda kulala,na nilifanya makusudi nikijua nikichelewa kulala sintaotA chochote..
Kweli sikuota ila nilikuja kushtuta saa9;30 alfajiri na usingizi ukakata.
Lakini ilipofika saa11 nilipitiwa na usingizi ulioambatana na ndoto, daah!
Nilimuota tena baba na hawamu hii afya yake imedhohofu,,ni kama nilikua nimetoka safarini na nimefika kijijini kuwaona wazazi
Nilipofika kabla sijaingia seblen nikawaona ndugu wa baba kama wawil wamekaa seblen,lakin ghafla alitokea mtu nyuma yangu akataja jina la baba akitaka kujua kama ameamka.
Lakin walimjibu bado hajaamka,mara nikamuona baba anatoka chumbani akiwa amechoka na afya yake ikiwa mbaya na ghafla akaanguka pale sebleni, wakati huo mimi bado nimesimama nje nikiwa kama sijielewi.
Wale ndugu walijitaid kumuinua lakini ilishindikana.niliingia ili kumuinua baba alinipa mkono kama ishara ya kutaka nimuinue bila kutoa sauti,nilimuinua lakini kabla hajasimama vizuri tuliteleza tukaanguka maana sakafu ilionekana kama ilimwagiwa maji baba akiwa amekaa chini nilikumbatia kwa uchungu nikiwa nimepiga magoti sakafuni huku nikiwa na maumivu makali moyoni juu ya hali ya baba yangu nikamwambia kwa nguvu umepatwa na nini baba yangu !.
Ghafla nikazinduka usingizin ,Cha kushanga ile hali ya kuumia baada ya kuona hali ya baba ndotoni bado nilikua nayo..mapigo yamoyo yalikua juu ad nikawa nayasikia.Nilipoikumbuka ile ndoto machozi yalitoka kwa kasi.kiukweli tangia haya mauzauza ya kuotaota yanianze sijawai kuumia kama nilivyoumia leo.
Nilipoangalia mUda kumbe sikulala Hata dakika 20 tangu ule usingizi na ndoto ziniianze.
Nikaamka nikajiandaa kwenda kanisani japo mimi sio mhudhuriaji mzur wa ibada ila niliona niende kabla ya kwenda kazini maana sikuwa na amani kabisa.
Wana JF hilo ndilo tatizo linaloniandama sijui kama kuna waliowai kukutana na kitu kama hiki na kama wapo wanisaidie cha kufanya pia kama umewai kusikia kwa waliopitia ninayoyapitia uniambie walisaidikaje.
Nb.mm sio muhumini wa imani za kidunia(kichawi,waganga wa jadi) tangu nitambue mema na mabaya.. naomba mtakaonisaidia msiingie huko sana..
Natanguliza shukrani!