Je! Kuvuta Sigara ni Dhambi?

Sigara inalewesha?
 

I'm just wasting my time with you. Huna la maana ya kuzungumza, so I'm not replying again!
 
Safi nimependa mkuu
 
Sigara inalewesha?
Ndio Sigara inalewesha ndio maana inavutwa.
Ipo Dhambi ya Ulevi ambayo imesemwa.
Ulevi ni pamoja na
1. Kunywa kilevi kinachouzwa sokoni kupita kiasi. ni ulevi.
2. Kunywa kilevi, (hata iwe kwa kiasi kidogo) kisichopimwa na wataalam wa Afya kama pombe ya Gongo. ni ulevi.
3. Kunywa pombe wakati wa kazi (ndio maana serikali imeamrisha kufungua mabaa kuanzia saa kumi jioni ) ni ulevi.
4. Kutumia kipato cha huduma nyinyine na kukinywea pombe ( mfano nyumbani wanakosa chakula wewe unanunua bia baa na kunywa ) ni ulevi.
5. Kutumia vilevi hatarishi kama madawa ya kulevya, Bangi, Sigara, Petroli, Mirungi nk. ( hivyo hata ukitumia kidogo sana wewe ni mlevi tu) ni ulevi.
Nk
Hivyo kuvuta sigara ni ulevi kwa maana kwamba ni kihatarishi cha afya yako.
 
Naomba mada iendelee tafadhar......mana mpka sasa hakuna aliemjibu mleta mada
 
Chochote kilicho hatari kwa afya na,maisha yako si vizuri kukiendekeza...

Unaweza sema dhambi...


Cc: mahondaw
 
2.kuendesha gari kunahatarusha Hali yako na jirani yako kwa maana hiyo nayo Ni dhambi .
Binadamu tunapenda kujitungia maandiko yetu
Nani kasema kuendesha gari ni dhambi ?
Mbona unajitungia maneno na kuhukumu wengine ?
Kuendesha gari kunahatarishaje hali ya jirani yako.
Kama unaendesha bila leseni basi ni sawa na ni dhambi kweli, kama una leseni haina shida.
 
Kiukweli sigara ni dhambi kwa sababu Neno la Mungu linasema kwamba;

Hamjui kuwa nyinyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu ambalo ndilo ninyi. (1Kor.3:16,17)

Sasa kama mimi na wewe ni mahekalu ya Roho mtakatifu; tutasalimikaje tujiharibu kwa sigara?

Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala nyinyi si Mali yenu wenyewe. (1Kor.6:19)

Kwa mafungu haya mawili, moja kwa moja uvutaji wa sigara ni uasi kama uasi mwingine.
 
Kuendesha gari bila leseni ni dhambi kwakuwa, umeikaidi mamlaka.
 
Sigara inalewesha?

Mkuu, sigara haileweshi, lakini wavutaji sugu wakikosa fegi, wanaonyesha 'withdrawal symptoms', yaani wanajisikia vibaya, kichwa kinaumiza na mikono zinatetemeka, yote kwa sababu ya kukosa dozi yao ya nicotine!
 
sio dhambi ila ni hatari kwa afya ya mwili., dhambi hutokana na uvunjifu wa amri kumi.
 
Ni dhambi kwasababu uvutaji wa sigara unaharibu mwili aliokupatia mwenyezi Mungu huku ukiwa unatambua kabisa uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako.
 
Niliwahi kumsikia shehe mkuu (Mufti) aliyepita akikiri kuwa alikuwa anavuta sigara alipokuwa kijana!
 
Hamna utetezi hapa
 
tumsifu YESU KRISTU mkuu.
 
Niliwahi kumsikia shehe mkuu (Mufti) aliyepita akikiri kuwa alikuwa anavuta sigara alipokuwa kijana!

Tuseme tu, kuwa kwenye ujana wake mufti alikuwa amepotea. Baadaye akapata hidaya (mwongozo) na akaokoka!
 
Kama hutumii usiwasemee wanao tumia, Bora nimuache mke wangu kuliko kuacha Sigara.

Nikiwa na stress inanituliza na kuniliwaza, nikiwa na furaha hasa nikishiba ndio burudani haswaa.

Hapa yenyewe navuta, najua lote ili naenda Dukani bila shida kabisa.

Nimekubali kufa na kifo cha mapaff haina shida Maana Mungu ni mwema. Wewe binadamu damu unaishi hujui utakufa kwa tatizo lipi? Kama dhambi bora niingie motoni.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…