Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,011
- 9,876
Msanii wa Mashairi ya kuongea,’Spoken words poerty, Malle Hanzi, ameandika kuhoji sheria ya makosa ya mtandao ilivyo. Amehoji hili baada ya Msanii wa kuchekesha kushitakiwa kwa kosa la kutumia laini isiyo sajiliwa kwa jina lake.
Amehoji kama kutumia laini isiyosajiliwa kwa jina lako kuna tofauti na kuendesha gari lisilosajiliwa kwa jina lako
Ameendelea kuhoji kuwa, Je, linakuwa kosa hata kama hakuna jinai yoyote uliyotenda kwa kutumia kitu kisicho chako au ni kosa tu kutumia kisichochako? Amefaninisha na gari kuwa unaweza kukamatwa kwa kupewa kosa la kuendesha gari lisilo lako hata kama haujavunja sheria au kusababisha ajali?
Je, inatosha kushtakiwa kwa kutumia laini isiyo na jina lako hata kama haujafanya uhalifu wowote na laini hiyo? Je, ikiwa mtu umeishiwa salio hautaruhusiwa kutumia simu ya rafiki yako au mpenzi wako kwa muda huo?
Amemaliza kwa sentensi ya kishairi kuwa “Kuna muda tunatunga sheria mpaka sheria zenyewe zinatushangaa”