Je, kutumia jina bandia ni chanzo cha maudhui yasiyo na tija mtandaoni?

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
3,270
3,560
Wazungu wanao huu msemo, "How you do one thing is how you do everything."

Na sisi makazini na majumbani tunauishi huo msemo. Ukichelewa intavyuu, mabosi wanahisi hata kazini utachelewa tu, na kazi zako zitachelewa pia. Ukidanganya sana kazini, hata kwenye mahusiano utachepuka sana.

Turudi kwenye mada. Uhakika Bro sio jina langu halisi ukilinganisha na Mshana Jr au Robert Heriel Mtibeli. Nimewataja hao wawili maana wana majina na picha zao halisi. Basi kuna namna hawa wenye kuamua kujitambulisha wao kama wao watakuwa na sifa hiyohiyo hata kwenye kuwasilisha mawazo yao. Na tumeyaona mengi tu.

Kwa wenye kukataa kuandika majina yao, hata mawazo wanayotoa utakuta sio yao. Hawajitambulishi wao kama wao bali wanaamua kuchukua fake ID na kutoa fake ideas walizojinasibisha nazo. Kulingana na ID.

Uchunguzi unaonesha pia kuwa, kuna watu wenye kutumia mbinu za kujinasibisha na characters fulani ili tuwachukulie siriazi kuliko walivyo.
Mfano; 1. Kujiita Uhakika Bro, uonekane wa uhakika.
2. Kutumia avatar ya mrembo uonekane mrembo
3. Kutumia avatar ya Einstein, uonekane una akili mingi
4. Kutumia avatar ya mtu wa ajabuajabu kisha kutumia ID hiyo kufanya mambo ya ajabuajabu
Etc etc nk

Shida ya ID feki: Ni pale mtu anapoamua kuficha mawazo yake halisi na kuweka yoyote tu. Yaliyo mainstream, au yatakayosound cool. Bila kujali yeye halisi binadamu anawaza nini.

Hatari iliyopo: Ni kuufundisha visivyo mfumo. Mfumo utachukua uongouongo na kuhisi kuwa huo ndio uhalisia wa wabongo wanataka nini. Kitu ambacho ni hatari.

Kwa kusema mfumo, nnaongelea Artificial Intelligence. Si ajabu mtu anaweza kutumia data zilizopo humu FamiiForums kuutrain mfumo kwa ajili ya Watanzania au mfumo wowote utakaotaka kuitawala Tanzania utatumia data za humu.

Sasa kama data nyingi haziakisi uhalisia wetu si majanga. Mfano mfumo uamini kuwa asilimia kubwa ya majina ya watanzania ni ya ajabuajabu. Mtu huko akiprompt 'I want to give my boy a Tanzanian name, could you suggest one?' Unashangaa inarudisha mzabzab au ye34nbe ona sasa.

Mifumo inayotupatia majibu sahihi imechukua majibu ya blogs, researchs na site kama quora na howtogeek labda na stackoverflow au reddit.

Hata kama sio mfumo. Kataa usikatae, wote tunaathiriwa na mawazo ya kila mmoja humu ndani kwa kiasi fulani. So hata sasa upo mfumo unajijenga na kutengeneza kitu kama 'hive intelligence' ya wanaJF. Maamuzi ya taifa kesho yanaathiriwa na michango yetu kwa akili ya nchi nzima.

Ushauri: Hata kama unatumia Id feki jitahidi kuandika wazo lako binafsi kama mtu, sio kama AI fulani.

Swali la kipimajoto: Je, unahisi ni kweli wanaotumia majina yao halisi tena na picha zao halisi humu JF wapo halisia 'authentic' zaidi ukilinganisha na wenye Id na avatar za kubumba?

Au tusaidiane, twendeni kule stories of change tukaangalie watu na mawazo yao. Je, walioweka mawazo ya toka moyoni na waliotype ukasuku wangapi wana ID halisi VERSUS wa ID feki🤔.
 
Ni kama destuli kwa jamiiforum watu kutokutumia majina yao halisi, ningekuelewa ungekuja na hoja ya multiple Ids ila hiyo hija yako haina mashiko unless we ni mgeni au unataka kuifanya jamiiforum kama Instagram au Facebook
 
Kuna member mmoja humu mimi kama LOTH HEMA nampenda na nammudu kihoja, ana umaarufu fulani hivi kwa ID yake moja maarufu, ila anazo zingine kama mbili akizitumia tumeshamjua kwa namna ya uwasilishaji wa hoja zake na tumemzoa hata akija na ID zingine tunambaini. Kasheshe imekuja kwa members wengine nao kuiga kuwa ID nyingi huku wasijue kuwa walishafahamika mitindo yao ya uwasilishaji wa hoja. Kuwa na ID nyingi humu ni upuuzi mtupu
 
Naona title ya habari imebadilika, natoa maoni tena kwa title hii nyingine. Hizi ID zimewalevya members kiasi cha kutojitambua wanapotoa maoni yao hawajui yana impact kwa wasomaji. Humu watu wanasoma taarifa mbalimbali na kufanya maamuzi. Sasa kama taarifa zenyewe zinaandikwa kifekifeki zikilindwa na id fake umakini utakuwa wapi? Anyway kama members wanatumia id fake basi michango yao iwe halisi
 
Ni kama destuli kwa jamiiforum watu kutokutumia majina yao halisi, ningekuelewa ungekuja na hoja ya multiple Ids ila hiyo hija yako haina mashiko unless we ni mgeni au unataka kuifanya jamiiforum kama Instagram au Facebook
Je jambo hilo linasema lolote kwenye kuhusianisha kwamba kama ni desturi yetu kuukana uhalisia wa majina yetu.

Na je ndo hivyohivyo katika kuukana uhalisia wa mawazo yetu yaani unafiki. Kuwaza vingine na kuandika kingine?
 
1. Fake IDs kwa kiasi kikubwa wanaandika uhalisia wa mawazo yao particularly when it comes to criticise the dictatorial regime kama za kwetu
Mmh! Kuna haja ya kuchunguza.

Lakini nnaiona pointi yako. Kuhusu wanaandika uhalisia kuna walakini. Na kuna pande mbili; anaweza kuwa anaogopa mamlaka asiwajibishwe kimakosa na anaweza vilevile kuwa anaogopa ni wazo/oni bovu asiwajibike nalo kihalali.


2. Real IDs hawawezi kuandika uhalisia wa mawazo yao especially against a dictatorial regime. Ni wachache, watu kama akina Lisu. Lisu yuko peke yake tanzania nzima kusema mawazo yake against the government and you can remeber the consequencies he went through
Mfano ni on point. Sema siku zote mambo mengi yasiyofaa huidhinishwa kwa kigezo tu cha security reasons. Spending za ajabu, action zisizo na mantiki hushinda kwa sababu za kiusalama. Sikupingi. Na itathibitisha kwamba ni taifa la waoga. So sad.
 
Kwa jf ilikua inasaidia sana miaka ile mambo mazito yanaibuliwa humu, ila kwa sasa imebaki kama destuli tu.
Hii hoja imeibuliwa mara nyingi sana. Na ina mashiko.

Ushauri tu ni kwamba watu waandike mawazo yao binafsi fake ID or real whatever.

Labda kuna inaowabidi kweli kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom