Je, kuoa ni kupoteza uhuru? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, kuoa ni kupoteza uhuru?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, Aug 21, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Mlioko kwenye ndoa naomba mnijibie swali hili, maaana huwezi jua ukali wa posi kama hupigi pasi.
  Inshort natarajia kujiunga na taasisi yenu soon.
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Karibu sana sana kwenye taasisi hii
  Sio kweli bana maana hakuna kitu kama hicho. Uhuru upo na ni namna tuu sasa ya kuutumia inabadilika. Maana huwezi ukaacha kukaa na marafiki zako kwa kipindi wala kukimbia starehe ulizokuwa umezoea. Sema tuu unajipangia namna ya kubalance majukumu ya familia na starehe zako
   
 3. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 796
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli kabisa; uhuru plus upweke hupotea na badala yake unapata kitu kilichobora zaidi ambacho ni home/family!
   
 4. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Karibu sana kwenye chama, ila si ajabu wengine tukakutana mlangoni tukiwa tumerudisha kadi.
   
 5. De Javu

  De Javu JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Well said Mr. Rocky, lakini pia na huyo mwenzako upeo wake wa ku balance ndio unapata hiyo conclusion ya kupoteza au kutopoteza uhuru.
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  hapana, kuoa si kupoteza uhuru! Kuoa ni kupata mke...
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Kama unataka kuendelea kuitazama keki yako na kuifurahia basi usiile!

  Hata hivyo uwe tayari kupoteza si uhuru tu bali vitu kibao. The bottom line ni kuwa unapokea 50% kutoka kwa mwenzio na wewe lazima ukate kiasi hicho hicho...

  Kama huko tayari unaweza kujaribu utowashi!!
   
 8. Z

  Zedikaya Senior Member

  #8
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Oa tu kwani hakuepukiki,ila wanawake ndio wana nafasi ya kuvunja au kuendeleza ndoa zao zaidi.

  mwanamke aliyeolewa anapaswa kuwa mnyenyekevu ,mwenye subira ,asiyependa makuu kwa mmewe na mwenye kufanya maombi kwa Mola wake wakati wote kwa ajili ya ndoa yake,

  kwa kufanya hivyo ndoa itadumu lakini yule mwanamke anayejifanya askari kwa mwenzie yaani kazi yake ni upelelezi na uchunguzi halafu akachukua jukumu la kutoa adhabu ndoa hizo ndio zimekuw ndoano.

  Pia wanaume msiweke rehani uhuru wenu kwa wake zenu kwa uoga.

  Zaid linda heshima yako na utu wako .....
   
 9. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu swala la ndoa na la ki-individualism zaidi kwa kila ndoa ipo tofauti kwa sababu human behaviour never be the same! Zaidi itategemeana na utakeye muona!
   
 10. Z

  Zedikaya Senior Member

  #10
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zilanga,naunga hoja pia
   
 11. chavka

  chavka JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Karibu ndugu ila kiukweli lzma utakutana na mabadiliko ya kijamii
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,266
  Likes Received: 22,024
  Trophy Points: 280
  Jsaud mbona unanitisha? Nini kinachokusumbua? Au na wewe ulipata bondia kama yule jamaa yetu wa Musoma aliyeamua kujitundiks baada ya kuona hana ujuzi wa kukwepa, kupangua na kurusha ngumi?
   
 13. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,959
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kuoa ni kupata na kupoteza! Unapata mke/mme, mwenzi wa maisha, rafiki wa karibu, na mtu wa kufarijiana, kuombeana, kusaidiana naye siku kwa siku.

  Kuoa ni kupoteza pia. Kama unataka ndoa iwe ya furaha kati yenu, ni lazima ukubali kupoteza. Moja ya vitu unavyopoteza ni uhuru. Kama kuna vitu ulizoea kufanya kabla ya kuoa lkn mwenzio havipendi lazima ukubali kuvipoteza. Eg. Km ulikuwa unahang out na friends (male or female) mpaka usiku wa manane lkn mwenzio hapendi, itakubidi ubadilike ili usije ukaiweka rehani ndoa yenu.

  Huwezi kuoa na ukaendelea kuwa na kiwango hicho hicho cha uhuru, lazima ukubali kupoteza kwa manufaa ya ndoa.
   
 14. Kibirizi

  Kibirizi JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Siku zote anayefurahia ndoa ni mwanamke, kwani siku zote mwanamke hawi na furahi mpaka mpaka aolewe na kwa mwanamme ni kinyume chake yaani anakuwa ana furaha siku zote isipokuwa anapoingia maisha ya ndoa, yaani kama ulikuwa unakwenda disco ukiingia kwenye ndoa inakuwa mwisho, ulikuwa una company na wadada sasa basi, ulikuwa huru kuiweka simu popote ilimradi ipo kwako sasa hakuna kitu kama hicho tofauti na hapo utaleta kesi, nyumbani kujaza nyomi la washikaji sasa basi, marafiki wa jinsia tofauti kukutembelea hiyo ndio mwiko kabisa, popote ulipo lazima mkeo ajue tofauti na hapo yatafika hadi kwa wazazi. Vile vile wahenga husema mwaume anapozidiwa akili na mwanamke hutangaza ndoa.

  Dumb man + clever woman = mariage.
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua kinachotufanya tuhisi tumepoteza uhuru ni ile kuongezeka kwa majukumu. Ulikuwa unakaa baa unakunywa na kula huko huko ila sasa una mwenza huwezi kukaa baa unywe na ule huko huko. Unakuta ile ya kunywa na kula unaitenga inaachwa home. So umekaa baa umekunywa umetosheka unajiendea tuu home.

  Na unapojikuta tena na mtoto anaongezeka utajikuta tuu hata wewe mwenyewe unajipunguzia safari za baa.

  Na vile vile inategemea na aina ya mwanamke uliyempata. Kama ni mwelewa na anajua umuhimu wako kuhang out na friends hawezi kupingana na wewe wala huwezi kupoteza uhuru wako.

  Ila ukimpata ambaye huo ni msamiati na hapendi uchelewe au uhang out na friends imekula kwako
   
 16. Imany John

  Imany John Verified User

  #16
  Aug 21, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,776
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  angalia thread angu!
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Majibu mengi hapa yanaleta swali lingine...faida ya ndoa ni nini?
   
 18. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu mm cjaoa, acha tusubiri wafugaji waje watupe maujuzi.
   
 19. Z

  Zedikaya Senior Member

  #19
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonesha wanaume ndio wamekuwa wahanga wa hizi ndoa, kwan wanaonekana kujutia ndoa zao, why?
   
 20. Z

  Zedikaya Senior Member

  #20
  Aug 21, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dump man+clever woman=marriage,ni kama utani hivi lakin ina ukweli mkubwa ndani yake kwan nimejionea jamaangu aliyekuwa akipelekwa pelekwa tu hadi ndani ya ndoa ,duu
  pia wanawake wengi huingilia uhuru wa wanaume kwa maslahi yao zaidi ili mwanaume amtumikie tu yeye ndio walivyo jambo ambalo huleta mivutano na mwanaume kuona yuko sehem isiyo sahihi,
  tusilazimishe jaman kama mtu hakuitaji siyo lazima kumng'ang'ania eti watoto,nk
  angalien namna ya kupata furah auitakayo bila kumkwaza mwenzio
   
Loading...