Je Kuna Umuhimu Wowote wa ................?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kuna Umuhimu Wowote wa ................??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Mar 1, 2011.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Wapenzi wa JF, kwa heshima na taadhima ninawasalimu wote.

  Nimejikuta ninawaza jinsi mimi kama mtoto wa kike ndani ya familia yetu ambaye nina majukumu ya not only to take care of my own family i.e. mwanangu kipenzi pamoja na familia ya wazazi wangu i.e. wazee na wadogo zangu- by the way mimi ni mzaliwa wa kwanza kwetu).

  Nimejikuta nikitingwa na mawazo ya umuhimu wa sisi wazazi wa leo (wote wake kwa waume) kung'ang'ania kutafuta au kupata mtoto wa kiume kwanza (Ingawa hali hii inaanza kidogo kubadilika now days but to many families it is an issue).

  Nahisi inakuwa na logic sana iwapo wazazi mna jiwweza na mnabiashara ambazo mna uhakika kuwa mtoto wa kiume tu ndiye atakayeweza kuziendeleza i.e. kwa kuwa yeye huwa haondoki kwenye familia- akioa anaongeza familia na si kupunguza kama mtoto wa kike.

  Lakini najiuliza iwapo mzazi/wazazi hawana asset yoyote ambayo wanahisi wanawezakumrithisha mtoto wa kiume kwa manufaa ya familia hapo baadae. Experience imeonyesha kuwa watoto wa kiume huwa wana attachment ndogo sana kwa wazazi wao (especially pale wanapoanza kujijengea familia zao) kuliko watoto wa kike. Watoto wa kike wanatend kujali wazazi zaidi ya wale wa kiume...........

  Je kuna umuhimu bado wa kukazania mtoto wa kiume? Yaani je bado kina mama tunastahesabiwa wanawake wa shoka kama tunauzao mkubwa wa watoto wa kiume zaidi ya wa kike?? Je nafasi ya mtoto wa Kike hasa katika kumwendeleza kielimu inastahili kupuuzwa?

  Ninajiuliza sipati jibu, ninakuomba msaada ewe kaka, dada, baba na mama, mjomba, shangazi, Babu na bibi yangu......
  Aksanteni, karibu tuchangie........
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  sijakuelewa...............sasa ka tutang'ang'ania wa kike tu hapo baaadae itakuaje nani mbegu za kuzalisha wa kike wengine watatoka wapo mana nadhani kizazi cha wakiume kitapotea.
  nendeeeni mkazaliane na kuijaza dunia
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  MJ1
  Nakusoma vizuri mno na hata mimi nashangaa sana kusikia watu wanavyong'ang;ania kuzaa watoto wa kiume na kudharau watoto wa kike.
  Binafsi kama wewe mimi ni mzaliwa kwa kwanza tena mwanamke.Baba yangu anaheshimu sana mtoto wa kike na wanawake na hata kujali kuwekeza kwa watoto wa kike. Inalipa kwa kweli.

  Kuzaa watoto wa kiume ni nzuri lakini isiwe kama ndio lazima sana.Tujali watoto wote bila kubagua.Ukikosa mtoto wa kiume basi usisikitike sana.Wekeza kwa mtoto wa kike itakupa faraja.
   
 4. NellyBizz

  NellyBizz Member

  #4
  Mar 1, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi wacwac wangu kwa mtoto wakike coz ndo wanachakachuliwa mapema.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mwanajamii one,
  Kwangu haijarishi mtoto awe wa kike au wa kiume. Kwa bahati mbaya sana wazazi wetu hata kwetu watoto wa kiume, walio wengi hawakutufundisha tujifunze tabia ambazo ni za lazima in the enterprise world. Ndio maana kwetu waafrika wengi mali za kurithi huwa hatuendi nazo mbali sana.
  Kwahiyo pengine wewe uanze toka mapema kumfundisha mtoto awe wa kike au wa kiume kujifunza kwa ukaribu, what it takes to make it in the corporate world.....I believe we have equal opportunities...but we lack the good combination of the ingredients of success( talent, passion, and hard work). Bila kujua namna ya kuenda nazo zote hizo sambamba, haijalishi mtu ni wa jinsi gani, itakuwa ngumu kufanya mambo tofauti.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Mar 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kwani watoto wa kike hawawezi kurithishwa na kurithi mali za wazazi/familia yao? Kama kuna watu wanaofikiria hivyo basi hizo fikra zao ni mbovu, haribifu,na zenye kudumaza jamii!!!!!!
   
 7. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #7
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapana ndugu yangu simaanishi tung'ang;anie wa kiume la hasha...nazungumzie zile extremes ambako mwanamke hudharaulika na hata kuachika kwa kuzaa watoto wa kike peke yake..................au ile extreme ya Baba kutoka nje ya ndoa in the name of looking mtoto wa kiume......... Mtoto ni mtoto whether wa kike au wa kiume.
   
 8. Jahmercy

  Jahmercy Member

  #8
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Huu ni ubaguz na udhalilishaji wa kijinsia, watoto wote ni sawa iwe wa kiume au wa kike.
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante WOS nashukuru kwa kunielewa vema. Yaani Dada acha tu ie ninareflect attitude aliokuwa nayo Baba yangu yaani ninamwona kabisa anavyotahayari but as you know mzazi ni mzazi hawezikiri kuwa alikosea na mimi kama mtoto au rather to put it in this way ... binti yakek siwezimsuta but mh.....yataka moyo kusema ukweli.
  Mzee wangu mimi ni msomi si kiviiile but amesoma na alishashika nyadhifa nyingi tu kubwa kubwa I can tell you he went far to the extent ya kumuintroduce mdogo wangu (wa Kiume) kama first born and mie it was like I wasnt exist kabisa (not to sy the mistreatment) sasa hivi ninaonekana wa maana.mh.

  Just thinking how many people in Tanzania still have such mentality.
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Mwj'1,

  ...hao wanaong'ang'ania mtoto wa kiume wanafuata matamanio ya nafsi tu. Mtoto ni mtoto, ...muhimu awe ni mwenye afya njema, na awe mwenye upendo na huruma kwa wazazi na ndugu zake. Haijalishi ni wa kike au wa kiume.
   
 11. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Watoto wa kike ni bomba sana hasa linapokuja swala la kuwaangalia wazazi wao, japo huko tunapoelekea wazazi watabaki kama walivyo na mali zao na watoto watatafuta vya kwao maana kila kinachoendelea magharibi ya mbali tunakopi, mara ndoa za mkataba ,mara an open marriage mara divorce after 1 yr in marriage, sasa itafika mtu anamrithisha mali zake mtu baki ambae ameona anamjali uzeeni na watoto wanaendelea na maisha.
  Wanaume wengi mpaka washikwe mashati na wake zao waambiwe twende tumpelekee mama yako kitenge, au nyumba ya wazee tupake rangi ila hua hawakumbuki wenyewe ni wachache wenye kukumbuka hayo, labda tu waoe mwanamke mbinafsi
   
 12. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #12
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  NellyBizz mawazo yako yanarepresent mawazo ya watu wengi yaani kwenye jamii yet believe me wengi (including my Daddy) thinks in that way......... but have you research watoto ambao wanatokea kujali sana wazazi wao zaidi...........?

  Ninachoamini ni kuwa sometimes dreams juu ya mtoto wa kiume haziwi kama tunavyodream and we end up to saidiwa/tunzwa na watoto wa kike.........So extremes za No watoto wa kike si nzuri........We should think Twice
   
 13. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  sory...nilipotea njia..!!
   
 14. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Duh pole mpendwa wazee wengi wako hivyo ila nowadays inapungua kama si kuisha na wanawake wameamka si wadogo kwa wakubwa, waliokuwa hawapendi shule wamerudi shule,wasichana mashuleni wanaongoza tu, na bado mpaka mungu awaonyeshe kwamba na sie pia tunaweza. sie baba yetu alipenda wasichana sana na wavulana walikuwepo naona ni mtazamo wake tu
   
 15. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #15
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mbu aksante kwa uelewa huu.................but am telling you vijijini sehemu nyingi bado adoration to the Baby Boy ni kubwa sana na hii inadhihirishwa na swali linaloulizwa mara tupatapo habari za ujio wa kiumbe kipya duniani......mtoto gani?? Au reaction aipatayo Baba mwenye watoto wa kike tupu. Mbaya zaid recently kumekuwa na tendency ya kuoanisha uzao wa kike na tania kama za ulevi eti walevi wengi hutungisha watoto wa kike au wenye tabia ya kupekura pekura wako likely kupata watoto wa kike zaidi ya wa kiume..............
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  siku hizi wazee wengi wanalelewa na watoto wa kike!watoto wakiume wanatafuta maisha na familia zao na kusahau wazazi,wakienda nje ya nchi ndio kuoa na kupata uraia wa huko ughaibuni!pia malezi ya watoto wa kiume kwa sasa ni magumu madawa ya kulevya,short cut za maisha zinawaharibu sana watoto wakiume!huwezi amini ktk biashara nyingi watu wanaona ni bora kuajiri binti kuliko mvulana kuhofia wizi na kuhonga!
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Aksante Via Mobile kwa kuwa miongoni mwa wachache wanaoligundua hili. Ni kweli kabisa kuwa bado kuna wenye uelewa kuwa Mtoto ni wa kiume na kuwa ukipata wa kike unaikuzia familia nyingine(Watakaomuoa). So wa aina hii hawaoni umuhimu wa watoto wa kike na hata kuwaendeleza huwa ni kwa shida kiasi flani.

  Mimi nilikuwa ninaambiwa live....pocket money ya nini?? wakati hufiki popote utaishia kuzalishwa tu kama si kuolewa soon after sekondari?? Na hata nilipomaliza high school kabla matokeo hayajatoka nilikwishajudgiwa kuwa sitaiingizia hasara familia kwa kunipeleka private colleges au government ones ambazo kutakuwa na cost sharing..................nilipewa live nijiandae kuolewa na kama nina mchumba basi nimwambie ajiandae kuleta posa iwapo sitafaulu kiasi cha kupata udhamini wa serikali!!

  Na hapo si kwamba mzee hakuwa na elimu?? La hasha alikuwa msomi tu kwa kiwango chake ambacho kilimwezesha kushika hizo nyadhifa za juu. But mentality aliyokuwa nayo juu ya watoto wa kike mh...........Sasa najaribu kufikiria wale ambao hawakubahatika kupata upeo huo na ambao bado wamesheheni mentality za Mtoto ni wa kiume.....
  Nikiyakumbuka hayo ninatamani nimwulize mzee wangu but ninaelewa position yangu kifamilia.
   
 18. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hakuna umuhimu.
  Mtoto yoyote anaweza kuja kumsaidia mzazi wake.
  Tena huwa naona watoto wa kike wana huruma zaidi ingawa hata yeye anaweza asiwe msaada kwa mzazi wake.
  Nina anko wangu alikataliwa na baba yake akajisomesha mwenyewe na kila kitu. Alivyopata kazi mzee wake ndio akajirudi na familia yao wote wakawa wanamtegemea yeye.
  Tushukuru mungu kwa mtoto yoyote utayempata.
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Pole sana MwanajamiiOne kwa kuwa na baba mwenye dhana za namna hiyo. Mvumilie tu kwa sababu huna uchaguzi kwenye shauri la yeye kuwa baba yako.

  Ila naomba nikuulize kama hutajali. Yaelekea kuwa wewe umesoma na sasa unajitegemea na nahisi hauko kwenye ndoa (naomba radhi kama nimekosea). Baba yako bado ana mtazamo na fikra za kama alizokuwa nazo hapo zamani wakati wewe unakua? Na sasa anakuchukuliaje wewe na ana mtazamo gani kwa ulipo kimaisha?
   
 20. LD

  LD JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hebu tuangalie historia inatuambia nini juu ya mtoto wa kike na wakiume. Hebu tutumie Biblia kama reference yetu ktk hili.

  Utaona tangia enzi za Adamu na Eva, hadi walivyoondelea mpaka kina Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Tukija mpaka hata kipindi cha Agano jipya, utaona mtoto wa kiume alikuwa anapewa nafasi kubwa katika jamii. Tena walikuwa wanatumia lugha hii watoto wakiume waliitwa WANA na wa kike BINTI. Kwa hiyo utasikia ana wana wawili na binti mmoja.

  Akizaliwa mtoto wa kike bila kuwepo wa kiume na ikatokea hata baba akafariki, lazima ifanyike njia azaliwe mwana (kiume) wakumuinulia huyo mwanaume aliyefariki jina.

  Mtoto wa kiume ndio mrithi, ndio mwenye kuendeleza ukoo, ndo wa kuhifadhi jina la nyumba husika!!
  Na hata Mungu alianza kumuumba Adamu ndo akamuumba Eva!!

  Nafikiri dunia iliumbwa hivo,iliumbiwa kumtazama mwanamke kama kiumbe dhaifu na kinachotegemea sana uwepo wa mwanaume!! Na mimi binafsi naona pamoja na yote mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume hata siku moja!!

  Haina maana tusisome au tusifanye kazi hapana, na jamii inatakiwa imsaidie mtoto wa kike ajikomboe kutokana na ujinga, na aweze kusimama kwa miguu yake pale inapobidi. Mwanamke tangia mwanzo ameumbiwa roho ya huruma na upendo na ndio maana sio rahisi mtoto wa kike kuwatupa wazazi wake hata kama hawakumtendea mazuri.

  Kwa hiyo sasa watoto wote wana nafasi yao katika familia. Nafasi ya mtoto wa kiume ipo na ya wa kike ipo.Ingawa pia inategemea huyu mtoto atakuwa vipi na tatokea mtu wa aina gani katika ukubwa wake!!!!!
   
Loading...