Je Kuna Umuhimu Wowote wa ................??

......Hii tabia ya kuona mtoto wa kiume ni bora kuliko wa kike mie inanikera sana, tena utakuta watu ni wasomi lakini bado tu wana wanachambua jinsia ya mtoto.
Mie mwenyewe nilijionea nilipopata mtoto wangu, rafiki za mume wangu walipokuja kumuona mtoto kila mtu anamwambia mume wangu eti ana bahati kwa kuwa kapata mtoto wa kiume....... cha ajabu hata kuna wamama nao wanasema hivyo hivyo....aiseeeee walikuwa wananiudhi kweli kweli halafu ni watu walioelimika haswa.
Watu hawajui kwamba siku hizi mtoto ni mtoto ilimradi awe mzima wa afya, mpe elimu bora ili aje kuwa na future nzuri maishani mwake.

Aksante Pretty
Ni kweli kabisa hata sie kina maam tumeshaambukizwa huu ugonjwa but in reality mtoto ni mtoto.
 
wajameni, Nina tangazo.

Ninatafuta mtoto wa KIKE, na natafuta wa 'kutafuta' naye. Matunzo yote juu yangu, aliye tayari ani PM tafadhali.

Aksante MJ1 kwa hoja nzuri kabisa. (karibu tunakusubiri huku)


Kaizer hahah unanichekesha
Haya nakuja
 
Dah! Hivi kuna mtu bado anazo hisia za kupendelea mtoto wa kiume zaidi kuliko wa kike?

Siamini kabisa!!!
Obuntu hii inadhihirishwa na pongezi tunazozipata tunapotoka leba............. na hata waume zetu wanavyorespond. Some people bado wana upendeleo huo
 
Naungana na wenzangu kuwa mtoto ni mtoto,akijengewa uwezo kwa misingi sahihi kama kwa kupata elimu,misingi ya kidini na maadili mema anaweza kuwa wa manufaa si tu kwa familia bali hata kwa taifa lake........ni kweli MJ1 kuwa sisi watoto wa kike tuko karibu zaidi na familia zetu kwa hali na mali.....nafikiri ni wakati muafaka watu wabadili mtizamo na kujifunza kuwa ukimwezesha mtoto wa kike umewezesha si tu familia bali hata jamii na kizazi kijacho.
 
Sasa mwanajami1 siumesha jua nini sababu ya familia kuhitaji mtoto wa kiume. anaongeza hapunguzi na kuhusu swala la kuwa karibu na wazazi hiyo ni maumbile mungu kawapa imani. ninyi mioyo yenu ina huruma. na pia mwanaume anamajukum yakulea familia yake na wazee. wewe umesema una mtoto una mzazi mwenzio ankusaidia kulea hebu jaribu kushekecha hapo utapata jibu zuri. au ndo tayari ile haki inayozungumzwa kilakukicha inawapa mwanya wakuamini kuwa kweli nanyi hamna tofauti na wanaume? kuna maswala ambayo ni necha huwezi kubadili kama ulaya na magharibi wanvyo idanganya dunia huko kwao yamewashinda, nafasi ya kumuendeleza mtoto wakike ni hakiyake aendelezwe kielim bila kubaguliwa na hakizote apewe lakini zina mipaka yake naimani mwanajami1 unajua Africa na Asia ni tofauti maana yangu kusemna kuna mipaka yake kwakuwa sisi tuna tamaduni zatu. huwezi wewe binafsi yako ukawa kama mwanaume mbele ya wazee wako kuna utofauti hapo japo unawalea lakini kuna sehem fulani mwenyewe huwezi kuikeuka mfano huwezi kuwa nje ya nyumbani kwa muda mwingi kila siku. huu ni mfano mmoja lakini mwanaume ni kawaida akisha fikia umri flani nazani naeleweka. ispokuwa kuna familia zinafanya makosa kutowashirikisha wanawake kenye mfumo wa kiuchumi haya ni makosa.
LAKINI NIMAONO YANGU
Mh hapana kasopa si kuwa tunataka kujilinganisha na wanaume la hasha bali ukiangalia kwa mapana utaona kuwa hali hii huchangia hata kuwepo kwa ubaguzi baina ya watoto wa jinsia hizi mbili ambapo preference ya ME hupelekea yeye kupata huduma muhimu zaid ya KE mfano elimu au hata matibabu na mahitaji mengine kwani lengo ni kumwendeleza asiharibu lile tegemeo la mzazi.

But from your point of view you are rite
 
wajameni, Nina tangazo.

Ninatafuta mtoto wa KIKE, na natafuta wa 'kutafuta' naye. Matunzo yote juu yangu, aliye tayari ani PM tafadhali.

Aksante MJ1 kwa hoja nzuri kabisa. (karibu tunakusubiri huku)

duh! Hii iende kule kwenye matangazo madogo madogo.
 
Gaga;Watoto wa kike ni bomba sana hasa linapokuja swala la kuwaangalia wazazi wao, japo huko tunapoelekea wazazi watabaki kama walivyo na mali zao na watoto watatafuta vya kwao maana kila kinachoendelea magharibi ya mbali tunakopi, mara ndoa za mkataba ,mara an open marriage mara divorce after 1 yr in marriage, sasa itafika mtu anamrithisha mali zake mtu baki ambae ameona anamjali uzeeni na watoto wanaendelea na maisha.
Wanaume wengi mpaka washikwe mashati na wake zao waambiwe twende tumpelekee mama yako kitenge, au nyumba ya wazee tupake rangi ila hua hawakumbuki wenyewe ni wachache wenye kukumbuka hayo, labda tu waoe mwanamke mbinafsi[/QUOTE]

Mtoto ni mtoto tu, kweli hilo sikatai. Ya kusema watoto wa kike wanakuwa karibu na wazazi zaidi kuliko wa kike ni kwa sababu mwanaume akiowa anakuwa na familia za pande mbili, anataka asaidie upande wa mwanamke na upande wa kwao. Hapo hapo ni jukumu la mwanaume kuitunza na kuilinda familia yake (mke na watoto). Japo wewe mke upo kama msaidizi kwa mume, mwanaume anakuwa na majukumu zaidi kuliko wewe mke. Sikatai katika ulimwengu wa leo mke na mume wanasaidiana katika kuitunza familia, ila mwanaume analazimika zaidi kuwa kichwa cha nyumba kwa ku-provide zaidi kwa familia hata kama pay ya mume na mke zinalingana.

Wewe mwanamke unaonekana kusaidia familia yako zaidi kwa sasababu una mume anatake care familia. Mwanaume hawezi kusema lolote juu ya wewe mke wake kwenda kuisaidia familia yako (Ukweni) na yeye kutoa mchango katika kuisaidia ukweni, Ila ni rahisi kama mambo hayako sawa kujibana katika kuwasaidia wazazi wake . Hii ni kutokana na Upendo alionao kwako wewe mke wake na kwa sababu ya ile haibu (Ukweni) lazima tu asaidie.

Kwangu mimi wazazi hawezi kuomba kitu nikasita kutowa msaada, huwa nafikilia jinsi gani walivyokuwa msaada kwangu mpaka kunifikisha hapa nilipo. Kuwa, walijibana sana pengine kushinda njaa mie niende shule. Nakumbuka pia kama mimi navyojibana kutoa huduma kwa wanangu ndo hivyo na wao walikuwa katika kuhakikisha napata mahitaji. Siwasaidii wanangu ili waje wanisaidie bali kuwapa msingi wa maisha bora ya baadaye. Wasijesema sikuwatendea haki. Ni kwa wote wa kike na wa kiume hilo sibagui.

Kusaidia ni moyo hakujalishi ni wa kike au wa kiume. La msingi ni ku-provide kwa wote bila kujabi payback.
 
Nimekuja hapa kuwasalimu na kuwapongeza wazazi wenzangu tuliojifungua watoto wa kike!

Mwanajamii1 nakusalimu.
 
WoS, binafsi nawapenda sana watoto wa kike, ukiwalea vizuri u'll come to love & admire them sana tu ... they are smart, understanding, lovely, etc ... hawana usumbufu sana kama hawa wakiume! Lakini this has alot to do with malezi ... kama malezi yenu wazazi (baba na mama) sio mazuri then ni bora tu mzae wa kiume ... hawa wakike mtawakimbia wenyewe kwa hizo vurugu zao za utoto / ujana na kuchakachuliwa!!

Ninapenda sana niwe nao wengi, kuna furaha ya ajabu huwa ninaipata ninapocheza na mtoto wangu wa kike ... but mke wangu naye anapenda awe na wakiume!
 
kuna mbaba flani aliniambia mke wake kajifungua,salama na tena amezaa faida.
Baada ya kumpa hongera nikamuuliza kuna kuzaa hasara?akanjibu manake amezaa kidume watoto wa kike mara nyingi huwa ni hasara.
Aliniudhi ile ni aje.
 
Back
Top Bottom