Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,148
- 10,571
Juzi Jumatatu nilipata taarifa kuwa kuna swahiba yangu alikuwa amelazwa pale hospitali ya Kanda ya Bugando ikanibidi niende kumjulia japo hali. Nilifika salama na tukazungumza mengi sana kuhusu maendeleo ya afya yake, tukacheka na kufurahi sana, namna bora ya kumpa uchangamfu mgonjwa maana alikuwa ana dozi yake ya sindano takribani 10 hivi.
Sasa pembeni ya kitanda cha swahiba alikuwepo dogo kama miaka kati ya 18 mpaka 20 hivi, tokea nilipofika huyu dogo alikuwa anaongea kisha anasita na kuweka tusi huku akisindikizia na ishara ya kidole cha kati. Matusi hayakuwa mepesi kwani alikuwa anatoa matusi heavyweight.
Ikanibidi niulize kuwa mbona ndugu wa kijana hawamuelekezi kuwa anakosea? Au kukemea tabia hiyo? Nikaambiwa kuwa kijana anaumwa ugonjwa wa Tourette syndrome, kimoyo moyo nikajisemea hizi mambo za Instagram pamoja na TikTok.
Nikajisogeza karibu na dogo, nikamsalimia na kumpa pole ila nikapokelewa na tusi la mzazi wangu wa kike pamoja na kidole cha kati. DAAH nikajipa moyo kuwa labda kweli ugonjwa wake ni mkali sana kiasi hicho. Nikamjibu nashukuru sana, dogo akajaa tena kwenye mfumo ananipa tusi jingine kubwa zaidi. Ahh Kimoyomoyo nikasema huyu dogo ni wangu.
Katika ulimwengu wa leo uliosheheni sayansi na teknolojia ya hali ya juu, kuna jambo moja la kushangaza: ongezeko la kile kinachoitwa matatizo ya kisaikolojia na kihisia. Zamani, mtu alipokuwa na hofu ya kitu, aliambiwa “jikaze!” kama unaogopa giza basi ndio utatumwa kufuata chumvi gizani ukutane na Nsyuka vizuri ama Shumileta kabsa.
Huyu dogo alikuwa mpuuzi sana, kwa sababu moja niliamua kuanza naye LIGI ya kutusi huku nikipiga kwenye mshono. Nilimpiga tusi moja dogo akaguna na kukaa kimya kabsa, nikamuuliza, huu ugonjwa wako wa Tourette umeanza lini?
Janja akaniambia kuwa yeye hana ugonjwa wala disorder yoyote zaidi disorder ya Tourette syndrome, ila ni vile ameishi na kukulia sana kwenye mazingira ambayo matusi ni Kiunganishi ila pia ni Kivumishi kikuu. Na alipofika Bugando, alikutana na Daktari mmoja raia wa Italia ndiye aliyemwambia kuwa anasumbuliwa na Tourette Syndrome.
Katika dunia ya sasa je, kweli tunapiga hatua mbele au tunazidisha mambo yasiyo na msingi? Leo unaweza kukutana na mtu mwenye hofu ya kutazama maji, yaani maji?! mwingine anaogopa majani au matawi ya miti, na mwingine kabisa ana hofu ya nywele!
Wataalamu watasema tunagundua na kuelewa zaidi afya ya akili kadiri siku zinavyosonga, jambo ambalo ni jema kabisa. Lakini kwa upande mwingine, jamii imeanza kuzoea tabia fulani hadi kushindwa kutofautisha kati ya ugonjwa halisi na mazoea ya mazingira.
Mfano hai ni yule kijana hospitalini anayedaiwa kuwa na Tourette, lakini ukikaa naye kwa dakika chache unagundua kuwa anachofanya ni matokeo ya mazingira aliyokulia—mahali ambapo matusi ni lugha ya kawaida kama “salamu”. Mwishoni dogo nilichapa tusi moja nikaona anatoa machozi nikamwambia hata mimi pia nina Tourette Syndrome..
Swali linabaki: je, tunatibu matatizo halisi au tunatengeneza majina mapya kwa tabia za kawaida? Wakati mwingine inaonekana kama dunia imeamua kuvaa miwani ya “diagnosis” kila mahali. Ukikohoa mara mbili—labda una “something syndrome”! Ukiwa haupendi watu wa upinde basi unapewa jina Homophobia, Ukifanya kazi na ukachoka—inaweza kuwa “emotional burnout disorder”.
Ni muhimu kutambua kwamba afya ya akili ni jambo nyeti na halipaswi kubezwa. Hata hivyo, tusipokuwa makini, tutafika mahali ambapo kila tabia ya kawaida itahitaji jina la kitaalamu. Na hapo ndipo dunia itakapogeuka kuwa ucheshi mkubwa—ambapo kuogopa jua kutakuwa kawaida kuliko kufurahia mwanga wake.