Je, kuna ukweli kuhusu Phobia na Mental Disorders?

Je, kuna ukweli kuhusu Phobia na Mental Disorders?

Ni balaa, maana wasiojali wapo wengi,Mimi kufagia na kudeki ni dakika sifuri tu, maana siwezi kuvumili naona vumbi kwenye kona ya chumba na mimi nipo.
Kuna kipindi nilikua taasisi fulani kozi ya mwezi mmoja sasa nikaona chupa za maji zimezagaa sana pale maana wanachukua intake ya watu kuanzia 100 hadi 300 na wanakaa mwezi mzima sasa chupa zinatupwa hovyo, ilinikera nikaamua kwenda mjini kuongea na Jamaa fulani huwa wanakusanya chupa na gari kubwa kwa ajili ya ku recycle, nikachukua namba nikamwambia nitakupigia jamaa alifurahi, bahati mbaya yule Boss wa ile taasisi nilipanga nimwambie akasafiri na mimi muda ukawa umeisha.
Saafi🫡
 
Mimk hata kupita kwenye darajq naogopa hadi mtu anishike mkono, kuendesha gari naogopa, kutembea kwenye ngazi za umeme siwezi naona naanguka kabisa. Hiyo ndiyo phobia nadhani
Yes..huwa hivyo jengo refu siwezi kaa kwenye kingo zake au kusimana
 
Mimk hata kupita kwenye darajq naogopa hadi mtu anishike mkono, kuendesha gari naogopa, kutembea kwenye ngazi za umeme siwezi naona naanguka kabisa. Hiyo ndiyo phobia nadhani
Ila phobia kiboko ni ya kuogopa 🐍 sidhani kama kuna mtu hana
 
Nakumbuka nishawai kutambaa kwenye daraja nikiwa mdg, Huwa sipatani na madaraja kusimama pembezoni mwa majengo marefu na issue ya nyoka
 
Nakumbuka nishawai kutambaa kwenye daraja nikiwa mdg, Huwa sipatani na madaraja kusimama pembezoni mwa majengo marefu na issue ya nyoka
Hiyo ya daraja ni uncle wangu aisee yaani ana miaka 35 ila daraja la Magufuli alipiga amefunga macho! Yeye ndio anazimia kabsa 😃 Phobia bhana
 
Juzi Jumatatu nilipata taarifa kuwa kuna swahiba yangu alikuwa amelazwa pale hospitali ya Kanda ya Bugando ikanibidi niende kumjulia japo hali. Nilifika salama na tukazungumza mengi sana kuhusu maendeleo ya afya yake, tukacheka na kufurahi sana, namna bora ya kumpa uchangamfu mgonjwa maana alikuwa ana dozi yake ya sindano takribani 10 hivi.
View attachment 3569127
Sasa pembeni ya kitanda cha swahiba alikuwepo dogo kama miaka kati ya 18 mpaka 20 hivi, tokea nilipofika huyu dogo alikuwa anaongea kisha anasita na kuweka tusi huku akisindikizia na ishara ya kidole cha kati. Matusi hayakuwa mepesi kwani alikuwa anatoa matusi heavyweight.
View attachment 3569128
Ikanibidi niulize kuwa mbona ndugu wa kijana hawamuelekezi kuwa anakosea? Au kukemea tabia hiyo? Nikaambiwa kuwa kijana anaumwa ugonjwa wa Tourette syndrome, kimoyo moyo nikajisemea hizi mambo za Instagram pamoja na TikTok.
View attachment 3569129
Nikajisogeza karibu na dogo, nikamsalimia na kumpa pole ila nikapokelewa na tusi la mzazi wangu wa kike pamoja na kidole cha kati. DAAH nikajipa moyo kuwa labda kweli ugonjwa wake ni mkali sana kiasi hicho. Nikamjibu nashukuru sana, dogo akajaa tena kwenye mfumo ananipa tusi jingine kubwa zaidi. Ahh Kimoyomoyo nikasema huyu dogo ni wangu.
View attachment 3569130
Katika ulimwengu wa leo uliosheheni sayansi na teknolojia ya hali ya juu, kuna jambo moja la kushangaza: ongezeko la kile kinachoitwa matatizo ya kisaikolojia na kihisia. Zamani, mtu alipokuwa na hofu ya kitu, aliambiwa “jikaze!” kama unaogopa giza basi ndio utatumwa kufuata chumvi gizani ukutane na Nsyuka vizuri ama Shumileta kabsa.
View attachment 3569131
Huyu dogo alikuwa mpuuzi sana, kwa sababu moja niliamua kuanza naye LIGI ya kutusi huku nikipiga kwenye mshono. Nilimpiga tusi moja dogo akaguna na kukaa kimya kabsa, nikamuuliza, huu ugonjwa wako wa Tourette umeanza lini?
View attachment 3569132
Janja akaniambia kuwa yeye hana ugonjwa wala disorder yoyote zaidi disorder ya Tourette syndrome, ila ni vile ameishi na kukulia sana kwenye mazingira ambayo matusi ni Kiunganishi ila pia ni Kivumishi kikuu. Na alipofika Bugando, alikutana na Daktari mmoja raia wa Italia ndiye aliyemwambia kuwa anasumbuliwa na Tourette Syndrome.
View attachment 3569133
Katika dunia ya sasa je, kweli tunapiga hatua mbele au tunazidisha mambo yasiyo na msingi? Leo unaweza kukutana na mtu mwenye hofu ya kutazama maji, yaani maji?! mwingine anaogopa majani au matawi ya miti, na mwingine kabisa ana hofu ya nywele!
View attachment 3569134
Wataalamu watasema tunagundua na kuelewa zaidi afya ya akili kadiri siku zinavyosonga, jambo ambalo ni jema kabisa. Lakini kwa upande mwingine, jamii imeanza kuzoea tabia fulani hadi kushindwa kutofautisha kati ya ugonjwa halisi na mazoea ya mazingira.

Mfano hai ni yule kijana hospitalini anayedaiwa kuwa na Tourette, lakini ukikaa naye kwa dakika chache unagundua kuwa anachofanya ni matokeo ya mazingira aliyokulia—mahali ambapo matusi ni lugha ya kawaida kama “salamu”. Mwishoni dogo nilichapa tusi moja nikaona anatoa machozi nikamwambia hata mimi pia nina Tourette Syndrome..
View attachment 3569129
Swali linabaki: je, tunatibu matatizo halisi au tunatengeneza majina mapya kwa tabia za kawaida? Wakati mwingine inaonekana kama dunia imeamua kuvaa miwani ya “diagnosis” kila mahali. Ukikohoa mara mbili—labda una “something syndrome”! Ukiwa haupendi watu wa upinde basi unapewa jina Homophobia, Ukifanya kazi na ukachoka—inaweza kuwa “emotional burnout disorder”.
View attachment 3569128
Ni muhimu kutambua kwamba afya ya akili ni jambo nyeti na halipaswi kubezwa. Hata hivyo, tusipokuwa makini, tutafika mahali ambapo kila tabia ya kawaida itahitaji jina la kitaalamu. Na hapo ndipo dunia itakapogeuka kuwa ucheshi mkubwa—ambapo kuogopa jua kutakuwa kawaida kuliko kufurahia mwanga wake.
Ujinga ujinga tu

USSR
 
Mbona kama umedanganya? Huwezi kulazwa kwasababu ya Tourette's bali kwa sababu ya kujidhuru kupitia Tourette's. Pia Tourette's ni ugonjwa wa kinyurolojia, sio kiakili.

Kuhusu uwepo wa magonjwa ya kiakili; Yapo, ila hatuyatilii maanani kwasababu ya kukosa maendeleo.

Kama viungo unavyoviona na kuvishika hupata changamoto, kwanini akili isipate wakati nayo inahitaji matunzo maalum na binadamu hatujakamalika?

Tunaishi kwenye ukanda masikini, hatuna uhuru wa kujali kuhusu afya ya akili. Nguvu zote tunaweka kwenye utafutaji.

Nitakupa mfano. Watanzania wengi wanaishi na hofu kali ya mapepo(Demonophobia) na hofu kali ya uchawi(Wiccaphobia) kama madhara ya kushikilia sana imani za kidini/kishirikina.

Sakata la kupoteza nyeti ni uthibitisho tosha. Pia kuna mauaji ya wabibi wanaodhaniwa kuwa washirikina, visa vya chuma ulete na misukule, mambo ya laana za ukoo, kafara nk.
 
Phobia yangu ni moja tu , kuichakata na kuichakata na kupata UKIMWI🤔
 
Ni kweli mkuu! Ukisoma vizuri utaelewa mkuu! Dogo hakuwa na Tourette syndrome bali ni alikuwa amezoea tu kwenye maisha yake!
 
Back
Top Bottom