Je, kuna ubaya endapo baadhi ya shughuli za ‘kiimani’ zinazoingiza mapato na faida kwa wamiliki wake zikasajiliwa na kupewa TIN number pamoja na EFD?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,750
2,000
Biashara ina tafsiri pana sana.

Baadhi ya shughuli zinazoitwa za ‘kiimani’ zinashabihiana kwa kiwango cha 100% na shughuli zingine za kibiashara ambazo husajiliwa na kupewa TIN number, leseni ya biashara pamoja na mashine za EFD.

Mfano:
1.) Mtu anaponunua maji kwa shs. 500/=, kisha ‘akayabariki’ na kuyauza kwa shs. 5,000/= kwa kila chupa, je, hii si biashara?

2.) Kiongozi wa imani anapofungua ofisi na kuchaji shs.100,000/= ili kumuona na kumuombea ‘mteja’ wake wa kiimani, na mwisho wa siku akaingiza pesa nyingi kuliko aliyotumia na kupata kipato/faida, ana tofauti gani na daktari anaefanya hivyo na kulipa kodo ikiwemo ‘ income tax’?

3.) Kuna bidhaa nyingine nyingi ambazo ‘wajasiriamali’ wa kiimani huziuza na kutengeneza faida, kama
‘Annointing oil’, ‘Vitambaa/leso za upako’, nk. nk

Sasa je, ni kwanini TRA isishtakiwe kwa uhujumu uchumi?
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,140
2,000
Kuna bidhaa nyingine nyingi ambazo ‘wajasiriamali’ wa kiimani huziuza na kutengeneza faida,
Faida inayopatikana hutumika katika kuendesha shughuli zingine za taasisi husika ya dini kama vile kulipia maji na umeme kwa maana nao pia ni binadamu na wana mahitaji kama wewe.

Kumbuka siku hizi ruzuku kutoka ughaibuni imepungua sana mkuu.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,750
2,000
Faida inayopatikana hutumika katika kuendesha shughuli zingine za taasisi husika ya dini kama vile kulipia maji na umeme kwa maana nao pia ni binadamu na wana mahitaji kama wewe.

Kumbuka siku hizi ruzuku kutoka ughaibuni imepungua sana mkuu.
Exactly kama ilivyo kwenye biashara zingine zinazolipa kodi, pia hutumia sehemu ya faida kulipia bill za umeme na maji.
 
Sergei Lavrov

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
7,240
2,000
Naunga mkono hoja! Fikiria mtu kama pornboy🤔

Lile sio kanisa ni kitegauchumi hivyo anapaswa kulipa kodi. Si yeye tu bali makanisa yote, madhehebu yote, misikiti yote hadi waganga wa kienyeji
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,750
2,000
Naunga mkono hoja! Fikiria mtu kama pornboy🤔

Lile sio kanisa ni kitegauchumi hivyo anapaswa kulipa kodi. Si yeye tu bali makanisa yote, madhehebu yote, misikiti yote hadi waganga wa kienyeji
Na kama anakidhi vigezo basi wapewe TIN number walipe kodi
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,140
2,000
Sijasema wasikusanye mapato na kupata faida, ninachohoji ni kwanini hawalipi kodi ilihali wanavigezo vyote vya biashara?
Taasisi za dini sio taasisi za biashara ndio maana hawalipi kodi. Mkuu, alafu kumbuka taasisi imara za ndini ni nguzo uhimu sana katika kujenga jamii yenye kujaa amani na upendo.
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,140
2,000
Exactly kama ilivyo kwenye biashara zingine zinazolipa kodi, pia hutumia sehemu ya faida kulipia bill za umeme na maji.
Taasisi imara za dini hujenga jamii/taifa imara ndio maana viongozi wa dini ni sehemu ya kamati ya usalama ya wilaya, mkoa na taifa na sio viongozi wa biashara ambao sio sehemu ya kamati ya usalama ya pahala popote pale.
 
FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
20,750
2,000
Taasisi za dini sio taasisi za biashara ndio maana hawalipi kodi. Mkuu, alafu kumbuka taasisi imara za ndini ni nguzo uhimu sana katika kujenga jamii yenye kujaa amani na upendo.
Dini sio taasisi ya kibiashara ndio, ila Kama wanajishughulisha na michakato inayoangukia katika kundi la biashara, then kuna biashara ndani yake
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom