Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Leo nimeona umuhimu wa kutoa elimu ya nini maana ya dhana "kutanua wigo wa Kodi" (broadening tax base).Nini maana yake?inajumuisha mambo gani?haijumuishi mambo gani?Faida zake kwa serikali,ikumbukwe "kutanua wigo wa kodi" ina maana zaidi ikitafsiriwa kichumi na sio kisiasa:
Nini maana ya kutanua "wigo wa kukusanya kodi" (broadening tax base)?Tafsiri yake kiuchumumi ni kuhakikisha kila chanzo cha kiuchumi katika nchi kinatozwa Kodi stahiki kwa namna ambayo haipendelei sekta,mtu nk.
Je,kutanua wigo wa kodi kunajumuisha mambo gani?kunajumuisha kutokadiria Kodi kwa upendeleo ili kuruhusu ushindani wa haki kwa waagiza mizigo na Wafanyabiashara,kutoegemea bidhaa au sekta moja katika kutoza kodi, mtu au bishara ilipe kodi kutokana na ukubwa wa mapato yake nk.
Je,kutanua "wigo wa kodi" hakujumuishi mambo gani?dhana hii haijumuishi yafuatayo; misamaha ya kodi,ubaguzi na upendeleo nk.
Kutanua wigo wa kodi kuna manufaa yafuatayo kwa serikali; usawa katika ulipaji wa kodi, mapato ya uhakika na makubwa nk.
Mambo muhimu ya kuzingatia kila tunapojadili dhana ya "kupanua wigo wa kodi" ni kuwa kodi yoyote mpya inayotambulishwa kwenye nchi inalipwa na mtu/biashara na kutoka kwenye chanzo cha kiuchumi katika nchi. hivyo basi ili kupendekeza aina mpya ya kodi lazima ujue mlipaji ni Mwananchi/biashara na chanzo chake ni shughuli ya kiuchumi inayokubalika (halali).
Ili serikali yetu ifanikiwe katika zoezi hila la kutanua wigo wa walipa kodi ni lazima kufanya na kuhimiza yafuatayo;
Kwanza,Kutambua wananchi wote nchini na kuhakikisha sekta zote zinatambulika (rasmi na isiyo rasmi).Kuhakikisha kila Mtanzania kaorodheshwa na kupewa kitambulisho cha uraia kutoka NIDA.
Pili,kila Mwananchi wa Tanzania kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi ili ushuru na Kodi mbalimbali za serikali (direct tax) zinazomhusu ziwekwe kwenye akaunti yake (TIN) hii itaongeza motisha kwani atapata rekodi kamili ya mchango wake kwa Taifa na atakuwa na sababu ya kuhoji na kudai huduma bora zaidi kutoka serikalini.Na kwa siku za mbele kila Mwananchi aweze kujikadiria kodi yake kila mwaka.
Tatu,matumizi ya TEHAMA katika ukusanyaji wa taarifa na malipo ya kodi na tozo mbalimbali za serikali.
Nne,udhibiti wa mianya ya kodi, bado biashara nyingi hazilipi kodi stahiki. Na hapa panahitaji ukali kwani hili kundi "linamiliki" wanasiasa na media kuwatetea na kueneza propaganda.Na hapa mianya ipo kwenye kodi zote yaani za ndani na forodha.
Tano,RUSHWA.
Zaidi ya yote inahitajika uzalendo wa hali ya juu pale ambapo chanzo kipya cha mapato kinapendekezwa kijadiliwe kwa hoja kwa manufaa ya Taifa pasipo kuleta siasa za ulaghai.
Nawasilisha.