Je kuna tukio lilishawahi kukupa depression

Je kuna tukio lilishawahi kukupa depression

Niliwahi kutuma mzigo wa dagaa kutoka mwanza kwenda dod0ma kwa mteja mmoja.. zilikuwa gunia tano za dagaa ..
Kipindi ule mzigo ukiwa njiani, yule jamaa akanaipigia simu kuwa amehairisha kuchukua mzigo wangu na wakati tulikuwa tumekubaliana nae kuwa atachukua mzigo wote. Nilipata stress za ghafla na depresion juu. Nilipambania ule mzigo na mwisho wa siku niliishia kupata hasara
Kufanya biashara ukiwa na njaa NDO matokeo Yale, UNATUMA mzigo mkubwa namna hii BILA HATA malipo ya awali acha wateja WA aina hiyo uzianwateja wanaolipa HUWEZI kosa wateja wanaokuamini wakilipa watumie mzigo ni RAHISI sana mteja kughairi SABABU lapata alternative ya Bei NAFUU wewe UNATUMA gunia Tano uko wapi nikuongeze depression
 
Habar wana JF natumaini wote wazima poleni pia na majukumu yanayo wakeep busy .

Nilisha wahi kupewa nisimamie mradi wa misitu ya serikali mwaka fulani, lakin kwa bahati mbaya zilidaka moto kwenye heka 150, zilipona heka 40 ambazo ndo zilikua kwenye matazamio ya uzalishaji , na ndo ilikua kama kazi yangu ya kwanza kukabidhiwa mradi niwe kama incharge, baada ya hapo nlipitia msoto mkubwa sana cjawahi experience mpaka nilihisi kupata depression
ilifika kipindi nakaa hata siku mbili sili chakula pia siongei nnacho waza kichwani nna wezaje kurudisha fidia ya pesa iliyo tumika kuanzisha huo mradi, lakini mungu mkubwa yaliisha.

JE ni kitugani kilikuletea msongo wa mawazo kupita kiasi ?

Depression is REAL
Labda tujuzane dalili za Depression ni zipi?
Usikute tuliwahi kupatwa na depression pasipo kujua.
 
Tukio la rafiki yangu wa karibu kufariki,nilihisi kuwehuka
Pole sana mdogo wangu..
hichi ndiyo nachopitia kwa sasa, nimepoteza my very closest friend almost 5 months now kwa ajali, wamefariki kwa pamoja yeye na binti yake angekuwa first year sahii,

kinachoumiza ni kuwa watu wako wa karibu they expect you to move on, na wanashangaa kwanini bado una huzuni unaulizwa kwani ni mzazi wako..!?
 
Kufanya biashara ukiwa na njaa NDO matokeo Yale, UNATUMA mzigo mkubwa namna hii BILA HATA malipo ya awali acha wateja WA aina hiyo uzianwateja wanaolipa HUWEZI kosa wateja wanaokuamini wakilipa watumie mzigo ni RAHISI sana mteja kughairi SABABU lapata alternative ya Bei NAFUU wewe UNATUMA gunia Tano uko wapi nikuongeze depression
Ulishawahi kufanya biashara ya dagaa?
 
Mwaka 2023 mmmh jaman achen wafanyabiashara vichwa viwake moto mim nilikua nafanya biashara ya viazi natoa shamba mbeya kule naleta mkoa niliopo eeh kama kawaida anayenisaidia kunitafutia usafiri kanitafutia usafiri Sasa ni ivi huwaga napenda kama kusafirisha nisafirishe na watu wengine tunachukuaga kontena Zima Sasa yule jamaa akanipakilia Kwa gar ya pekee nilikua naongea na dereva vizur mpaka alipokaribia kufika akazima simu Sasa yule naye sijui alikua amelewa akasahau kuchukua namba za gar na siku zote Huwa ananitumiaga namba za gar ukisikia kuteleza ndo huku
Tulijaribu kumtafutaa wwe nikachoka ila alinipa anguko la kimataifa 🙏
 
Mzee naandika muda huu hapa nina depression sio ya kitoto

Nimekosa pesa january hii nikaingia mikopo ya mtandaoni nikakopa nikalipa nikakopa tena mpk ikafika 560,000/= mzee jamaa kumbe ile kuwapa access ya kucheki call logs wamechukua namba zote za simu wakaanza kunizushia na kunipakazia tuhuma za kufedhehesha.
Hiyo jana ndio wamefanya hivyo bila shaka asubuhi hii wanaendeleza kazi.
Usiwalipe kmmk washenzi sana hawanaga uvumilivu
 
Mwaka 2023 mmmh jaman achen wafanyabiashara vichwa viwake moto mim nilikua nafanya biashara ya viazi natoa shamba mbeya kule naleta mkoa niliopo eeh kama kawaida anayenisaidia kunitafutia usafiri kanitafutia usafiri Sasa ni ivi huwaga napenda kama kusafirisha nisafirishe na watu wengine tunachukuaga kontena Zima Sasa yule jamaa akanipakilia Kwa gar ya pekee nilikua naongea na dereva vizur mpaka alipokaribia kufika akazima simu Sasa yule naye sijui alikua amelewa akasahau kuchukua namba za gar na siku zote Huwa ananitumiaga namba za gar ukisikia kuteleza ndo huku
Tulijaribu kumtafutaa wwe nikachoka ila alinipa anguko la kimataifa 🙏
Pole sana miss
 
Pole sana mdogo wangu..
hichi ndiyo nachopitia kwa sasa, nimepoteza my very closest friend almost 5 months now kwa ajali, wamefariki kwa pamoja yeye na binti yake angekuwa first year sahii,

kinachoumiza ni kuwa watu wako wa karibu they expect you to move on, na wanashangaa kwanini bado una huzuni unaulizwa kwani ni mzazi wako..!?

Asante

Pole sis..
Msiba usikiwe tu kwa mwingine,mtu anaweza kuwa sio mzazi lakini akaumiza sana akifariki
 
Back
Top Bottom