Enny
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 962
- 130
Kuna dada nafanya nae kazi na mtu wa nyumbani, kuna kipindi aliniambia amepata mchumba na aliomba ruhusa kwenda kujitambulisha kwa wazazi wake. sasa ni miaka miwili, jana nilimuuliza vipi mnafunga lini ndoa (harusi) na yule mchumba wako? akanijibu mmmmh bado najaribu kufikiria. Maana huyu mchumba wangu naona kama ananitumia sana. Kila mara amekuwa wa kuomba msaada ya hapa na pale amekuwa akitoahela kumsaidia lakini anaona sasa imezidi, alikuwa anaishi peke yake sasa kaenda kuleta mama yake, mdogo wake, mtoto wake aliyezaa na mwanamke mwingine na mtoto wa dada yake wakati anajua kipato chake ni kidogo sasa imekuwa taabu sana mara anatumia meseji hawana unga, mara hata mboga ya kula leo hamna , sasa kodi imeisha mara hana anahangaika asaidiwe, madeni anayo mengi mpaka anajiuliza hivi wakioana itakuwaje? Nikamjibu awasiliane na wazaziwake awaulize ushauri maana sikutaka kuingia moja kwa moja kumjibu. Sasa nimeleta hapa najua manaweza kutoa ushauri wenu wa kwa hili.