Je, kuna madhara gani kiongozi kutoa hotuba kichwani?

Hotuba itokayo kichwani bila kusoma ina faida na hasara kwa kutegemea mtoa hotuba mwenyewe.
FAIDA.
-kuwa huru na unachosema bila mipaka, mifano, vinogesho n. k.
-muongeaji akiwa mahiri hachoshi hadhira
-hutoa fursa ya mwili (body language) kwenda na hotuba
-mtoa hotuba huwa ni kama "anaongea na familia yake" kwa urafiki na bashasha tele
HASARA
-muongeaji kuhama mada kila muda na kuwafanya watu /hadhira kuwa na kazi ya ziada kuutafuta mtiririko au dhumuni
-Lugha itakuwa si rafiki sana kwa wote (mzungumzaji anakuwa huru kuchanganya lugha au misemo)
-utunzaji wake kiofisi utahitaji uchambuzi na uboreshaji utakaoendana na hitaji
-kutokana na kuhama lugha moja hadi nyingine baadhi ya wasikilizaji kutoelewa lugha fulani. Hivyo ujumbe kutofika kwa wakati
Hivyo ni baadhi tu ya mambo ambayo nimeyabaini.
 
madhara ni kutoa maneno Kama yupo kilabu cha pombe
Hahahahaaa. Mkuu itakuwa pombe za kuteka hizo. Siyo bia au wine and the like! Pale lazima uongee kwa madaha huku unasindikiza hotuba yako isiyo rasmi kwa mafunda kadhaa ya bia. Bila kusahau kizungu kwa chaaaatii...!
 
Back
Top Bottom