Je, kuna madhara gani kiongozi kutoa hotuba kichwani?

SALAM KWENU NDG WANA JAMVI HBR ZA WEEKEND NA POLE KWA MAJUKUMU.

Kwanza niende moja kwa moja kwenye swali langu Nimeshuhudia viongozi mbalimbali wakiwemo marais kuandaliwa hotuba au kuandaa wao wenyewe mambo ya msingi waliyoyapanga kuyawasilisha ktk Hadhira na kuyaandika ktk Karatas au vifaa vya kisasa kama IPad hivyo Kiongozi huwa Anasoma pale na kukazia hicho alichokikusudia, Lakini wapo Baadhi ya viongozi Akiwemo mkuu wetu wa nchi nimemfuatilia Mara nyingi hotuba yake unakuta haijaandikwa mahali popote Huzungumza mwanzo hadi mwisho kutoka kichwani.Sasa watalam wa mambo haya ya hotuba na mambo mengine tujuzane Je!!

Kuna faida gani ya Aina hii ya hotuba Isiyoandikwa mahali? na Hasara za Aina hii ya Hotuba ya kichwani ni Zipi??

KARIBUNI SANA

!
!
hakuna madhara kama kiongozi huyo ana Brains
 
Naamm na nirahisi kujua anatoka wapi na wapi anaelekea na kuepuka kurudia rudia mambo Yale Yale ktk mazingira tofauti nafikiri hivyo
 
Kwa mtazamo wako naiona mantiki ya hotuba iliyoandaliwa na kuwekwa mahali kuliko ile ya kutoa kichwani moja kwa moja
 
Hasara mojawapo ni kuumiza hisia za watu wengine kwa maneno makali na kuzorotesha mahusiano ya ndani na utangamano wa kimataifa.
Basi kuna ttzo kubwa siyo kama tunavyolichukulia kwa upande wa mkuu wetu wa kaya anapaswa kubadilika
 
Inategemea uwezo wa kiongozi, na aina ya hotuba (Speech). Kama ni Policy Speech ni vizuri akasoma, lakini kama ni Political Speech anaweza Kutoa kichwani.
Viongozi kama Nyerere, Jakaya, Makamba SR,wanauwezo mkubwa wa kuongea bila kusoma.
umeeleza vizuri Lakini sasa kwa mkuu wangu habagui aina ya speech ile ni Policy au political vyote ni kutoa kichwani hilo ni ttzo
 
Hotuba itokayo kichwani bila kusoma ina faida na hasara kwa kutegemea mtoa hotuba mwenyewe.
FAIDA.
-kuwa huru na unachosema bila mipaka, mifano, vinogesho n. k.
-muongeaji akiwa mahiri hachoshi hadhira
-hutoa fursa ya mwili (body language) kwenda na hotuba
-mtoa hotuba huwa ni kama "anaongea na familia yake" kwa urafiki na bashasha tele
HASARA
-muongeaji kuhama mada kila muda na kuwafanya watu /hadhira kuwa na kazi ya ziada kuutafuta mtiririko au dhumuni
-Lugha itakuwa si rafiki sana kwa wote (mzungumzaji anakuwa huru kuchanganya lugha au misemo)
-utunzaji wake kiofisi utahitaji uchambuzi na uboreshaji utakaoendana na hitaji
-kutokana na kuhama lugha moja hadi nyingine baadhi ya wasikilizaji kutoelewa lugha fulani. Hivyo ujumbe kutofika kwa wakati
Hivyo ni baadhi tu ya mambo ambayo nimeyabaini.
 
Faida yake unaweza kuimba free style maana freestyle huandiki mahali,

Hasara yake unaweza kuongea utumbo wasikilizaji wakakuacha na mic..
Aiseee umeeleweka vzr sana kumbe mkuu wetu anapaswa kujua hafanyi freestyle ni Kuhusu maisha ya watu
 
Mbona viongozi wengi tu duniani wanatoa hutuba kichani bila kusoma, au ulitaka watumie matako kutoa hotuba
 
Mbona viongozi wengi tu duniani wanatoa hutuba kichani bila kusoma, au ulitaka watumie matako kutoa hotuba
matako umesema wewe na Mimi sijakataa kuwa hakuna viongozi wanaotoa hotuba kichwani Swali lilikuwa jepesi tu Tujadili hapa Yapi madhara ya aina hii ya speech?? Na faida zake ni zipi?? Mbona kama umepanic au uko kwenye list??
 
Hotuba itokayo kichwani bila kusoma ina faida na hasara kwa kutegemea mtoa hotuba mwenyewe.
FAIDA.
-kuwa huru na unachosema bila mipaka, mifano, vinogesho n. k.
-muongeaji akiwa mahiri hachoshi hadhira
-hutoa fursa ya mwili (body language) kwenda na hotuba
-mtoa hotuba huwa ni kama "anaongea na familia yake" kwa urafiki na bashasha tele
HASARA
-muongeaji kuhama mada kila muda na kuwafanya watu /hadhira kuwa na kazi ya ziada kuutafuta mtiririko au dhumuni
-Lugha itakuwa si rafiki sana kwa wote (mzungumzaji anakuwa huru kuchanganya lugha au misemo)
-utunzaji wake kiofisi utahitaji uchambuzi na uboreshaji utakaoendana na hitaji
-kutokana na kuhama lugha moja hadi nyingine baadhi ya wasikilizaji kutoelewa lugha fulani. Hivyo ujumbe kutofika kwa wakati
Hivyo ni baadhi tu ya mambo ambayo nimeyabaini.
haya ndo mawazo na uchambuzi wa great thinker nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom