Je Kuna haja ya CCM kuchaguliwa tena mwaka 2010

Nipe chama mmbadala na nitajie at least watu 20 watakaounda baraza lao la mawaziri!.

Mpaka leo naamini hamna chamba mmbadala wa CCM. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na sio nje.

Wewe utakuwa waziri wa mambo ya nje; so tunaanzia hapa; au hujiamini? any one can be a waziri au kuna kozi yake; hiyo spin ya kizamani sana hiyo; mwambie na jirani anaweza kuwa ndiye Meya ila sio meya wa CCM etc
 
Nafikiri Maaskofu na wasomi wa Kanisa katoliki wameyaona haya yote ndo maana wametoa mwongozo, nafikiri wanastahili support ya Wabongo wote wapenda maendeleo na wanaopenda kuona nchi yao inapiga hatua ndefu za maendeleo.
 
Kwa kila Mtanzania makini na mwenye moyo wa dhati kwa Taifa hili atakumbuka ahadi nyingi zilizotolewa na CCM...mfano:

... CCM katika ilani yake ilisema kuwa itaboresha na kupunguza vifo vya wakina mama je Leo Mama Zetu wanakufa kwa kukosa huduma za afya vijijini au wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma za afya??
.
...sasa inasemekana mwakani kila familia itagawiwa vyandarua viwili kwa ajili ya kupambana na gonjwa la Malaria.Vyanadarua hivyo vitawekwa dawa maalumu ya kuua mbu amabayo rangi yake ina Kijani cha mbali!!
 
Hizo zote zitakuwa ni Kampeni tu mzee wangu hakuna jipya kabisa kwa hilo na tu basi wazee wa kuwahadaa wanatanzania ni hatari sana
 
CCM kwa ujumla mi chama ambacho kimeshapoteza sifa ya kuendelea kuongoza nchi hii. Tatizo ni kwamba chama gani kingine kitaweza? Ni wazi kwamba ndani ya CCM kuna watu safi wanaopinga udhalimu unaofanywa na wenzao ndani ya chama. Sasa hawa inabidi waachie ngazi waanzishe chama mbadala nasi wana wa nchi hii tunaoipenda nchi yetu tutawapgia kura ili waingie madarakani. Hawa kama kweli wana moyo wa kizalendo, wakati wa kujitoa CCM ni sasa, wasingoje mpaka washindwe kwenye kura za maoni (kwani wamepaniwa kweli kweli na mafisadi wa CCM). Au mnasemaje?
 
Ili kuinusuru nchi yetu katika lindi la umaskini ni vyema watu waadilifu tu ndio wagombee nafasi mbalimbali 2010.Hata hivyo uadilifu upo wa aina nyingi.Je uadilifu tutakaoutaka 2010 ni upi?Karibuni.
 
..wengi hugombea wakiwa waadilifu, sasa wakipata nafasi ndiyo wanageuka na kuanza ufisadi.

..wapiga kura tunapaswa kuwakataa wagombea ambao tayari wanajulikana kwamba ni mafisadi.

..wapiga kura pia tuwakatae wabunge ambao wameshindwa kutatua matatizo ya wananchi majimboni.
 
Hao Watanzania waadilifu utawatoa wapi? kwa watanzania ninaowajua mimi waadilifu ni wachache mno!

Hata ambao hawajaiba ni kwasababu hawajapata nafasi ya kuiba.
 
CCM kwa ujumla mi chama ambacho kimeshapoteza sifa ya kuendelea kuongoza nchi hii. Tatizo ni kwamba chama gani kingine kitaweza? Ni wazi kwamba ndani ya CCM kuna watu safi wanaopinga udhalimu unaofanywa na wenzao ndani ya chama. Sasa hawa inabidi waachie ngazi waanzishe chama mbadala nasi wana wa nchi hii tunaoipenda nchi yetu tutawapgia kura ili waingie madarakani. Hawa kama kweli wana moyo wa kizalendo, wakati wa kujitoa CCM ni sasa, wasingoje mpaka washindwe kwenye kura za maoni (kwani wamepaniwa kweli kweli na mafisadi wa CCM). Au mnasemaje?
Kweli sifa zote walipoteza siku nyingi sana
 
Hili la Maaskofu wa kikatoliki ndilo litakalonifanya nisubire waseme chaguo lao la mungu halafu niwaepuke kama ukoma! hawajengi hawa sana sana wanaleta divisions kwenye jamii.
Kuna haja ya kuwaunga mkono kwa hilo na waraka wao ni mzito mzee wangu hivyo kuna haja ya kuwasupport na kuhamashisha kwa kila hali
 
CCM Kama tulivyo zoea itarudi madarakani kwa mbinu zake zote na kwa gharama zozote. kadri siku zinavyozidi kwenda ndio nazidi kukosa imani kabisa na CCM, kuna vitu ambavyo huwezi tegemea kama mtu yule uliyekuwa na matumani nae ( kama mizengo Pinda) anaweza kusimama bungeni na kusema " haiwezekani Rais kuwa Fisadi) baada ya kusema hayo anasema " kama tatizo ni mgodi wa Kiwila, basi tutarudisha hisa zote serikalini". kimsingi muheshimiwa pinda haoni kama hilo ni tatizo.

Wanajamii wenzangu tusaidiane kuelimisha jamii yetu hasa kuhusu masuala ya demokrasia na haki wananchi kwa ujumla. naimani ipo siku CCM itakaa pembeni hata kwa miaka 5, wapate fundisho la kudumu na waache kutufanya watanzania wajinga kila kukicha.
 
CCM haichaguliwi maana haina haja ya kuchaguliwa ,ile inatokea danganya kwa wadanganyika, hivi mpaka leo hamjasituka kuwa CCM inajiweka madarakani kwa nguvu na usaliti wa kufuata mkondo wa kupigiwa kura ,CCM ni wasaliti wakubwa wa haki za binadamu ,CCM ndio wanaovunja Katiba ya Nchi hii na ndio wao wanaoongoza ,ushindi wao ni wa kidikteta ,mkitaka msitake watatawala ,sasa kuchaguliwa kupo wapi ?
 
Sasa wewe unafikiria ufanye nini juu ya haya mambo ya CCM na watu juu ya masuala ya aibu kwa Taifa letu
 
Nipe chama mmbadala na nitajie at least watu 20 watakaounda baraza lao la mawaziri!.

Mpaka leo naamini hamna chamba mmbadala wa CCM. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na sio nje.

Wewe, hii ni ajabu kweli, kwanini watu 20 tu? mbona Watanzania wenye uwezo wa kutawala ni wengi? ofisi zote za umma na wafanyakazi mbalimbali wa mashirika ya umma na binafsi wengi wao ni watanzania.

Labda useme wengi wa walioshindwa na waliokuwa wagumu wa kubadilika ndio wanaoshikilia nafasi muhimu Tanzania (simply kwa sababu hawako tayari kubadilika, ili nawe pia uweze kuonyesha uwezo wako kamili kuitumikia nchi), waone kina Kingunge, Mapwachu, Kahama na wengine wengi walioamini wakishindwa wao basi wanaoweza ni wake zao au watoto wao tu. Naona haikopi kuwa hata ww waweza kuwa mwana wao ndio sababu huoni hao watanzania wanaofikia 20.

Ningekushauri katika hao 20 uanze kujihesabu wewe katika nafasi yako unayolitumikia taifa, kwani utawala sio lazima ukashike nafasi ya Masha au Membe. Kila mtu atatumika kwa nafasi yake, ikiwa ni pamoja na wale waliosafi ndani ya ccm. Mbona wengi tu wanatumikia serikali hii hii ya ccm japokuwa wao sio wana ccm? Hapa kubwa ni taifa! ila wenzetu mnatutisha pale mnapoamini ni bora kiti apewe Mbwa kuliko mtanzania mwenzio kisa anamini katika itikadi tofauti!
 
Yeye anajua lazima mtu awe waziri ndiye kiongozi. Hajui wao wapo kuna wafanyakz kibao na makatibu wakuu kibao na pia kama mtu akishinda uchaguzi anaweza kuchagua serikali toka kokote kule
 
Lazima tukubali yale mazuri ya CCM na pia wakubali na mabaya nayo wamefanya sio mazuri tu!! Hivyo unaweza kubadili kabisa mtazamo huu kwa taifa letu na watu wakawa na furaha baada ya kupata watu wadilifu katika taifa
 
Hafai kuchaguliwa tena, after all hazingatii good hygiene, anasalimia watu kwa mkono uliokuna nyayo ambazo zinaweza kuwa zina fungus for all we know...
07_09_cys5hz.jpg

8E9U8974.JPG

8E9U8927.JPG
 
Last edited:
Kuna haja ya kukataa na kuwa makini sana na kuzingatia tamko la Kanisa Katoliki la kusema na kwa kuwa mzee mzima anaona kuwa muda huu ndio mada ya mahakama ya kadhi imepamba moto ndio amekwenda huko but ni kosa kubwa sana kutokuwa na tamko kutoka mdomoni kwao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom