Je Kuna haja ya CCM kuchaguliwa tena mwaka 2010

"Je Kuna haja ya CCM kuchaguliwa tena mwaka 2010'' Ni swali gumu sana na kulijibu unatakiwa kuwa makini sana,kwangu mimi naweza kusema ndiyo au hapana lakini sasa tuangalie miaka 45 CCM imefanya nini?
Elimu.Mwalimu alijua umuhimu wa elimu na ndo maana elimu ya juu ilikuwa free kwa kila mtu ili mradi tu amefaulu vizuri,CCm ya sasa elimu imeifanya kuwa mtaji wa kisiasa na kuwagawanya wtu katika makundi kama samaki wakati watoto wao wakisoma nje.
Huduma za Jamii;hili ni tatizo, hosptali hazitoshi, madakitari wengi ni wala rushwa, mama wajawazito wanajifungilia katika mazingira mabovu, maji na umeme ni vitendewali baadhi ya maeneo.
Mgawanyo wa rasilimali zilipo; Hili ni tatizo tena kubwa, Mpaka sasa tunaambiwa kuwa mtanznia anaishi chini ya dola moja kwa siku wakati watu wengine wanatanua kwa kutumia kodi/rasilimali za wanachi/walipakodi, mgawanyo hauko sawa, gap kati ya maskini na tajiri ni kubwa sana.MAFISADI NDO UMEKUWA WIMBO WA TAIFA, AIBU GANI HII NYIE WATALA NA WATAWALIWA??
Miondombinu;mpaka sasa bado tunatumia barabara za vumbi, reli ni ile tuliyojengew na wajerumani, sasa sisi tunaweza kujivunia nini mpaka??
Kulingana na hayo machache, mimi sioni sababu ya CCM kuendelea kushika hatamu hapo mwaka 2010, ni jambo la busara kukaa pembeni na kuangalia chama kingine kikishika hatamu na kujifunza, hapo ndo tutakapo pata maendeleo ya kweli.
2010 CCM KAA PEMBENI HATA KWA MIAKA 5 TU ILI UJIFUNZE.
 
Nipe chama mmbadala na nitajie at least watu 20 watakaounda baraza lao la mawaziri!.

Mpaka leo naamini hamna chamba mmbadala wa CCM. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na sio nje.

wasipotokea hao wapinzani kutoka CCM?

Haya mawazo ni sumu kuliko ufisadi wowote ule Tz, na waliochoka tu ndio husema hivi
 
Back
Top Bottom