Je Kuna haja ya CCM kuchaguliwa tena mwaka 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Kuna haja ya CCM kuchaguliwa tena mwaka 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Josh Michael, Jul 8, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa kila Mtanzania makini na mwenye moyo wa dhati kwa Taifa hili atakuwa na maswali yafutayo:
  1. Katika hali ngumu za maisha ambazo kila kukicha watu maskini wa taifa hili wanaendelea kusota kwa kukosa chakula, malazi na elimu, Je CCM ambao wakati wa uchaguzi wa mwaka 2005 waliwahidi Watanzania maisha bora wameshindwa kutimiza au wametimiza maisha bora kwa kila Mtanzania?? Jibu unalo wewe mwenyewe Mtanzania??

  2, CCM katika ahadi zake ilisema kuwa itatengeneza ajira milioni moja Je Ajira hizo zimepatikana au watu wamepata ajira???

  3. CCM katika ilani yake ilisema kuwa itaboresha na kupunguza vifo vya wakina mama je Leo Mama Zetu wanakufa kwa kukosa huduma za afya vijijini au wakati wa kujifungua kwa kukosa huduma za afya??

  4. CCM katika ilani yake ilisema kuwa itaongeza wigo wa Elimu ya juu je katika hilo wameweza au wamefanikiwa?? Je uongezeko hilo linaendana na ushindani katika sekta ya elimu na kuboresha vitendea kazi kwa walimu na na walimu ambao wanafundisha katika vyuo vyetu.

  5. Katika Ilani ya CCM walisema kuwa watajenda barabara nchi Nzima Leo hii wameweza kujenga na hili unaweza kulinganisha na kipindi cha Mkapa?? Jibu unalo wewe mwenyewe katika kutazama maeneo unayotoka au kwenda na kuona kama kweli wameweza au lahasha??

  6. Katika Kutoa mikopo ya elimu ya juu, CCM walisema kuwa Hakuna mtoto yoyote yule atayekosa elimu kwa ajili ya ada na kulipiwa ada katika vyuo vikuu, Lakini leo hii kuna maelfu ya watoto wa wakulima wamekosa au kufukuzwa katika vyuo hivi kwa ajili ya kushindwa kulipa ada na gharama nyingine.?? Jibu unalo wewe mwenyewe

  7 Katika kupambana na ufisadi CCM inasema kuwa Rushwa ni adui wa haki Je leo Hakuna hata mtu mmoja aliwahi kuvuliwa hata uchama au ukada wake kwa ajili ya ulaji au utoaji rushwa kubwa kuna watu wengi wapo na wanaendele kuwapo katika Chama japo wamehusika na kuliingizia taifa hasara kubwa kama EPA, Kagoda, Richmond, Meremeta, na madudu mengine katika taifa na kuacha maskini wanateseka na watoto wetu kukosa sehemu hata elimu nzuri kwa ajili ya maisha yao baadae. Je CCM wanatekeleza Ilani yao??

  8. Je CCM katika Ilani yake walisema kuwa watatoa Mitaji kwa ajili ya wafanya biashara na wakina mama Je Hizo pesa zimekufikia wewe kama mtu wa kawaida na kutumia katika njia nzuri au zilikwenda tu kisiasa na kufanya kampeni kwa ajili ya kuona kama kweli zimeleta ahueni katika maisha yako ya kila siku???

  9. Ilani ya CCM wanasema kuwa wataendeleza yake yote mazuri na kufanya mwafaka kati yake na CUF kwa kumaliza yote na matatizo ya Zanzibar je leo hii bado mwaka mmoja wameweza kumaliza tofauti zao na kukaa kama Taifa moja Jibu la Swali hili unalo na Jibu jingine analo Prof Lipumba na Seif Sharif Hamad??

  10 Je Kwa ujumla Maisha yake yameboreka au ndio umaskini umeongezeka katika Taifa letu?? Je kuna haja ya kuwachagua tena viongozi kama hawa?? Je kuna nia ya dhati katika kuwambia ukweli na kwa kuwauliza wakati huu na kuona kuwa wamefanya nini au ndio wao wanaendelea kusema kuwa TUTAFANYA HIVI?? JE hizi kauli za TUTAFANYA HIVI ZITAISHA LINI?? Maswali na majibu unayo wewe mwenyewe

  11. Je Taifa kama Tanzania lipo katika njia nzuri ya kwenda au kupiga hatua katika maendeleo kwa sera hizi au mwenendo huu. Majibu unayo wewe mwenyewe.
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nipe chama mmbadala na nitajie at least watu 20 watakaounda baraza lao la mawaziri!.

  Mpaka leo naamini hamna chamba mmbadala wa CCM. Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM na sio nje.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Walikuwa wapi kipindi chote, Upinzani wa kweli unaweza ukawa wewe pamoja na jirani yako kwa kipindi hiki, Unaweza kuwa na kuchagua Chama Mbadala na kuwakabidhi maisha yako, Kuliko ilivyo sasa hivi..!! Unaweza kuwafanya na kuunda serikali nyingine kwa wakati huo ukifika na kufanya yale ambao CCM leo wameshindwa?? Je utaendelea kuona mambo haya ya ufisadi unaendelea mpaka lini??
   
 4. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Hivi FairPlayer, haya mawazo ni ya kwako kweli. Ukiangalia viongozi wengi wa CCM wapo hapo kwa miaka mingi sana, kuna watu wako tangu Mwinyi akiwa Rais wa Nchi hii. Unataka kuniambia kuna hata watu 20 ambao ni smart watakao patikana ndani ya CCM ikiwa imetokea kuvyunjwa kwa Baraza la Mawaziri na bila hata ya kumchagua waziri yeyote ile aliye kwenye baraza la sasa???

  TANZANIA BILA YA CCM INAWEZEKANA, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180

  Nakubaliana na wewe mkuu
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna haja ya kufanya uamuzi mzuri sana kama watanzania wataamua kuwachagua viongozi hawa hawa ni vizuri pia, Kama wataona kuna watu wengine wanafaa hata ndani ya CCM nalo ni vizuri, Lakini hali ni mbaya sana katika Taifa hili, Kama ni Mgojwa basi yupo ICU, Hakuna mwenye sauti ya kweli na maamuzi dhabiti katka Taifa letu kwa sasa. Hivi tunakwenda wapi ndugu zangu?? Hivi hakuna mtu makini au watu makini?? Hivi tutabaki tunaongea mpaka lini?? Hivi rasilimali zetu ambazo kila kukicha zinatoroshwa na watu wachache tutafanya nini??
   
 7. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Natamani kulia kwa ajili ya Taifa hili kwa sasa, Sasa zimebaki politics tu mzee wangu, Kuna haja ya kuchukua uamuzi mgumu sana katika kipindi cha uchaguzi mwakani
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Uamuzi mgumu kwa ajili ya watoto wetu kama tutaona kuwa ni bora kubaki na mambo ya leo basi nalo ni vizuri sana
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  CCM hii ambayo imeanza kuwa Chama kinachojihusisha na IBADA za dini moja nimeanza kuichoka. Dini ziwe huru kufanya mambo yao. Kama walikuwa wana-under estimate wakristo 2010 wataelewa vizuri kama wataendelea na mpango wa kuanzisha Mahakama za Kadhi na kuzilipia ulikuwa sahihi au la!
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi sana hata leo Wakristo na waislamu kukwaruzana kwa ajili ya CCM na ilani yake, Je kama ndio ilani kwanini wasiwape Mahakama hiyo?? Mbona sisi Watanzania tunazidi kuwa pilitica za ajani kama hivi jamani??
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Uamuzi mgumu uanza mwaka huu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,kama unavyojua hakuna muda uliobaki wa matayarisho na bado utasimamiwa na wakurugenzi ambao wote ni wafuasi wa CCM,kuna kazi kubwa sana kufikia demokrasia ya kweli
   
 12. C

  COMRADE44 Senior Member

  #12
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  "A positive thinker " ---Could'nt be more negative.What a pity.
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jul 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Waislamu wamesema kuwa Mahakama za Kadhi ni sehemu yao ya ibada sasa serikali inahusianaje na hiyo ibada? Mahakama za kadhi ni haki za waislamu, hilo halina ubishi. Ubishi uko kwenye kutoa fedha kwa ajili ya dini moja. Mahakama ziendeshwe na zinaowahusu. Mbona hili ni rahisi wala halihitaji kwenda shule?
   
 14. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hayo ni mawazo hafifu, kusema hakuna anaeweza kuliko ccm, yeyote anaweza kuongoza, wapo wengi vile tu huwajui ndugu yangu, muhimu ni we need changes, more than 40yrs its enough to weigh someones capability. thanks
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu hili swali nadhani aliwahi kuulizwa Nyerere, kama akipewa nchi nani atakuwa waziri wakati hakuna hata mtu aliyeonekana kuwa na uwezo. Lakini alimanage. Sitaki kuamini kuwa hakuna chama ambacho hakina watu wanaonweza kuunda serikali, wakati wana pool ya mamilioni ya watanzania. Labda sijakuelewa maana yako mkuu.
   
 16. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kuna wakati mwingine tuangalie kwa makini na tuwe wawazi. Ile dhana ya kuwa CCM ina wenyewe haipo tena. Ndio maana hata mafisadi wameweza kuiteka sasa. Kwa hiyo efforts zikifanyika kuisafisha CCM no doubt kuwa , CCM safi inaweza kuchaguliwa.
   
 17. Lengeri

  Lengeri Senior Member

  #17
  Jul 8, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  baraza la mawaziri lapaswa kuundwa na watu makini. Angalia hili la sasa kila siku utasikia kituko, juzi bungeni Kawambwa anamuuliza mbunge kama kwenye jimbo lake ipo hoteli anayoweza kushukia, baraza la mawazri lilikaaa na kupitia bajet kabla ya kwenda bungen lakini mkwara wa siku mbili wa maaskofu wakanywea.

  kazi ya uwaziri lazima ziwe na watu makini tuwe kama malasysia zinatangazwa na watu wanaomba wanakuwa screened na mwenye uwezo ndo anapewa si kumpa mtu uwaziri kama asante kama Rais Kikwete alivyompa Masha incompitent kabisa lakin asante ya deep green
   
 18. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2009
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Hapakuwa na haja ya kuichagua CCM hata mwaka 2005 na hakuna haja ya kuichagua tena 2010. Wale mawaziri wa CCM ambao hawana fikra za ufisadi
  wanaweza kuunda chama mbadala au wakajiunga na chama cha upinzani kimojawapo.
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuwasafisha pekee yao haitoshi maana ni wahalifu kama wahalifu wengine na tena wanaendelea kutesa huko na huko tena hata jana Spika alisikika akisema kuwa Mafisadi hawafungwi hivi kweli ndugu zangu inakuaje serikali ambayo inawaacha wahalifu kama hivi
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  CCM asilia sawa,ondoa CCM mtandao/maslahi hawafai
   
Loading...