Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Ukisoma kitabu cha Daniel. Kuna kipindi Daniel wakati yupo huko Uajemi aliamua kufunga kwa wiki tatu. Hakuoga, hakunywa pombe(divai), hakula nyama wala msosi wowote mzuri. Sasa kumbe malaika aliyekuwa ametumwa kuleta majibu wakati analeta akakutana na mkuu wa ufalme wa Uajemi, wakaanza kupigana kwa siku 21. Malaika akaelemewa hadi alipokuja Mikaeli, malaika mkuu kumsaidia. Kwa hiyo yeye akapeleka ujumbe na kumuacha Mikaeli akimalizana na mkuu wa Uajemi na waambata wake.
Sasa huyu mkuu wa ufalme wa uajemi aliyeweza kupambana na malaika na kumzidi nguvu hadi Malaika mkuu akaja kumsaidia ni nani? Inawezekana alikuwa ni binadamu? Au ni aina ya shetani?
Je, kila taifa lina shetani wake wa kuliongoza?
Hapa ni Daniel sura ya kumi kuanzia mstari wa 11 lakini ishu yenyewe ni huo mstari wa 13.
11 Akaniambia, Ee Danieli, mtu upendwaye sana, yafahamu maneno nikuambiayo, ukasimame kiwima-wima; maana kwako nimetumwa sasa. Na aliponiambia neno hili, nalisimama nikitetemeka.
12 Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
13 Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.
14 Sasa nimekuja kukufahamisha mambo yatakayowapata watu wako katika siku za mwisho; maana maono hayo ni ya siku nyingi bado.
15 Na alipokwisha kusema nami