Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 15,167
- 16,256
nimesikia amefiwa na baba yake tukuyu, kama ni kweli basi natumia nafasi hii kumpa pole yeye na ndugu wote
mimi kidogo namfahamu mwakasege
Ni mnyakusa wa Tukuyu baba wa watoto wanne 3 wasichana na 1 mvulana na ni mme wa mke mmoja. Ni mtaalamu wa uchumi na mipango aliysoma chuo kikuu cha Dar. Alianza kazi kama afisa mipango ktk wilaya ya Arumeru akiishi ktk nyumba za carmatec Duluti, baadaye aliacha kazi serikalini na kujiunga na KKT makao makuu kama afisa mipango na uchumi. Miaka ya tisini alianza kufundisha mafundisho hayo ya kiroho. Kumbuka yeye ni MWALIMU sio nabii wala mchungaji, baadaye aliacha kazi KKT na kujihusisha na shughuli binafsi alifungua ofisi yake inayoitwa TASOET inayojihusisha na ushauri wa uchumi na mipango pia serikali ya awamu ya tatu kampuni hii ilikuwa miongoni mwa kampuni zilizohusika na Debt advocacy ili serikali ipunguziwe madeni. Pia amekuwa akijihusisha na uandishi wa vitabu vidogo vidogo vya mafundisho ya kiroho cha kwanza kikiwa ''Jifunze kusamehe na kusahau'' pia amekuwa akichapiza vigazeti vinavyoitwa MANA kula ukue kiroho, pamoja na uuzaji wa audio na video tapes za mahubiri yake. Amekuwa akiandaaa mikutano yake kupitia timu huru ya NEW LIFE CRUSADE COMETTEE ni timu huru kwa sababu ina wanakamati toka madhahebu yote ya kikristo ktk mikoa yote ambayo anafanya semina, mbali na maombezi semina zake zinahusu ukuaji wa kiroho na jinsi ya kuishi kama mkristo. Pia amekuwa akiandaa safari za Israel ''visit to the holy land'' pamoja na marriage retreat hukohuko. Yeye sio mchungaji na hana kanisa wala dhehebu ni muumini wa kanisa la KKKT kanisa la kijenge. Kwa sasa anaishi Njiro Redio. Hivyo ni kwa ufupi jinsi mimi nnavyomfahamu, mwalimu Christopher Mwakasege
Asante mkuu unaweza kuwasiliana nao kwa kupitia ...
Christopher & Diana Mwakasege
P. O. Box 2166,
Arusha, TANZANIA.
Phone: +255-27-2504289
Fax: +255-27-2504289
Email: tasoet@nexusdigital.co.tz.
Natumaini nitakuwa nimekusaidia wewe na ndugu yako anaehitaji maombi.
Ahsante bwana Pukudu maana umesema ukweli na ukweli mtupu kumhusu huyu mtumishi wa MUNGU. Mwakasege ni moja ya wahubiri wachache ambaye akikwambia acha dhambi na ukimwangalia matendo yake(japo kwa nje maana ni mungu anayejua ya sirini) utakubali kwamba kaul zake zinaongozwa na ucha mungu. Ni tofauti sana na wahubiri wengine ambao wanavyohubiri na ukiangalia matendo yao inatia shaka wazi wazi.
Kinachofurahisha kuhusu huyu jamaa ni kwamba jumapili anaingia kanisani kama waumini wengine tu.
HAJIKWEZI KWA HALI YOYOTE, NA ANAKUWA MYENYEKEVU SANA KWA WACHUNGAJI.
wANAJARIBU KUMPA VITI VYA MBEELE KANISANI, japo yeye asingependa iwe hivyo.
Anasikiliza kwa utulivu mahubiri ya wachungaji wake kama vile hajui kitu.!
Mungu mbariki sana mtu huyu.
Nchi ya Tanzania inahitaji sana watu wa namna ya mtu huyu, maana ndo wanaosababisha nchi hii angalau iwe na amani iliyopo, na ana uwezo wa kusoma alama za nyakati za kiuchumi wa taifa hili na za kiroho.
Mungu mbariki mtu huyu tena.
Wewe unasema hivyo coz hujawahi kukutana na wachungaji/manabii wanaoua kujikweza na kujisifia mahubiri mazima na kutoa amri za kipuuzi kwa waumini. Kama Mwakasege ni mnyenyekevu lazima tuseme kwani ndivyo anavyoonekana. Kuhus roho yake hiyo ni juu yake na Mungu wakeNakubaliana na sifa ulizompa mtumishi huyu wa Mungu - lakini naona kama vile umesifu kama vile UNAMWONA HADI MOYONI.......
wakati anapofanya huduma yeye mwenyewe.......naamini anakaa kiti cha mbele ... au??? Hivyo kukaa kiti cha mbele wakati upo kwenye huduma ni kitu cha kawaida na UNAPOMKARIBISHA MTU AKAE KITI CHA MBELE KWENYE HUDUMA YAKO ... ni kawaida pia - so Wachungaji wana haki zote kumkaribisha wakiwa kwenye huduma zao - Pia kukaa kiti cha mbele haiongezi wala kupunguza utukufu mtu alio nao mbele za Mungu na kukaa kiti cha mbele sio kukosa unyenyekevu, au kukaa kiti cha nyuma sio unyenyekevu ... ile ni "seat" tu - mambo yote yako moyoni.
Umesema anakuwa mnyenyekevu sana kwa Wachungaji ..........sasa kwa Mtumishi (Mwalimu mkuu) kama yeye ........... what do you expect??? MIMI NADHANI SIFA AMBAYO UNGEMPA ... BILA KUMSEMEA ROHO MTAKATIFU AU MUNGU AJUAYE MIOYO YETU NI KUWA ANAFANYA KAZI YA MUNGU KWA BIDII BILA KUCHOKA ........................MENGINE NI HAPO TUTAKAPOSIMAMA MBELE ZA MUNGU AMBAYE ATAPIMA NA KUHUKUMU KILA MTU.....
Nakushauri na wewe uige na ufanye alivyo yeye ............ila YESU awe kielelezo chako zaidi.
Hayo ni mawazo yangu tu ..................ubarikiwe na Bwana Yesu
Huyu ni mbabaishaji tu anaepata kula yake kupitia migongo ya waliokata tamaa. Hana tofauti na kina Anthony Lusekelo na wengineo. Asanteni!
Mungu akusamehe ndugu yanguHuyu si ndiye yule tapeli aliyesema Haiti wamepata maafa kwa sababu ya uchawi? Na yeye tapeli mchawi tu.